Nyikani tutaiongoza Dunia kulikusanya Kanisa la siku za mwisho

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,880
23,776
Salaam,Shalom.

Wakati Dunia na mifumo yake ikijitengeneza kuhakikisha Dunia nzima unaungana kupata sarafu Moja, utawala mmoja na siku moja ya Ibada Dunia nzima ( JUMAPILI).

Nyikani, Taifa la AGANO, tumekwisha Anza kuifanya KAZI muhimu ya kuikusanya Dunia nzima na Kanisa la mwisho, kabla ya kurudi Kwa kristo mara ya pili, tutaabudu siku ya Saba ya juma (JUMAMOSI) katika HEKALU Moja na mwili mmoja wa kristo bila kugawanyika, tutaunganishwa turudi tena kuwa wamoja kama lilivyokuwa Kanisa la kwanza.

Mwovu alipojua kuwa siku za mwisho,watashuka Malaika, mizeituni miwili kuhubiri INJILI ya ufalme, kulikusanya Kanisa na misingi Ile ya Kanisa la kwanza,yule Ibilisi , akaiga na kugeuza jambo na mission hiyo Kwa faida yake,

Anapanga kuwakusanya mataifa yote kukusanyika Kwa Ibada Moja, kwamba Dunia nzima wapige goti kwake siku ya kwanza ya juma,mnamo 2030-2033,

Mission orijin lazima itatimia, na mission hiyo ni hii iliyokwisha Anza katika Taifa teule , Israel ya Rohoni, Nyikani. Tayari mjumbe wa AGANO amekwisha tangulia mbele kulikusanya Kanisa la Dunia nzima na point au center na mwanzo wa mission hiyo imeanzia hapa.

Dini zote, wakusanyikao Ijumaa, JUMAMOSI na Jumapili na wasio na Dini, watajua yupi ni Mungu mkuu kuliko wote anayestahili kiabudiwa. Mapigo yanayoendelea duniani na DHIKI inayoikumba na inayoendelea kuikumba Dunia, itawakusanya na kuwagawa Wana wa Mungu katika pande mbili kuu pekee, Upande wa Giza na wa Nuru.

Pande hizo zitakuwa kama ifuatavyo, wa Jumapili vs wa JUMAMOSI ,ambapo center Yao Wana wa Mungu (JUMAMOSI )watakusanyikana watakuwa na Taifa lao katika Nchi ya Nyikani.

Tunamshukuru Mungu, Kwa kulichagua Taifa letu kubeba Dunia katika jambo hili muhimu la kuiandaa Dunia, kulikusanya Dunia Kwa ajili ya kutengeneza Ufalme wa Mungu Duniani na kuiandaa Dunia Kwa ajili ya kurudi kristo Yesu Kwa mara ya pili.

Mungu ibariki Nyikani,

Mungu wabariki wote waaminio!!

Aamen🙏
 
Back
Top Bottom