Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,881
- 46,631
Wapishi wa nyama katika migahawa, Bar, hotel, sherehe na hata majumbani hakikisheni nyama zinaiva vizuri na kuwa laini kabisa. Iwe nyama ya kuchemsha, kuchoma au kukaanga nyama inatakiwa iwe laini kabisa uweze kuichambua au kuitoa kwenye mfupa au kuitenganisha kwa kijiko, uma au mkono mmoja tu.
Iwe nyama ya ng'ombe, mbuzi, kuku wa kienyeji au kitimoto nyama inatakiwa kuivishwa na kuwa laini kabisa. Iwe utumbo, mbavu, paja, mguu au sehemu yoyote ile inatakiwa iive iwe laini.
Haipendezi na Inakera sana kula nyama huku unavuta kwa mikoni miwili kama manati au unatafuna kama bigijii, Inakera kula nyama huku zinabaki kung'ang'ania katikati ya meno na kukuhitaji kumaliza toothpick kikopo kizima kusafisha mabaki ya nyama kwenye meno.