NSSF Ubungo acheni longolongo! Lipeni wateja wenu mafao yao!

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
774
196
WanaJF,

Utendaji kazi wa baadhi ya watumishi NSSF Ubungo haulidhishi kabisa! Nimekuwa nikifuatilia kulipwa mafao yangu toka mwezi 7, 2019 mpaka leo hii sijalipwa napigwa kalenda tu bila hata kujali kuwa mtu huyu anatokea wapi! Manake si kila mtu anaishi na kufanya kazi Dar es Salaam. Watu wengine waliokuwa wakiishi Dar es Salaam baada ya mikataba yao ya kazi kuisha au kufukuzwa kazi, kutokana na hali ngumu ya kimaisha inayokuwepo kwa kutokuwa na kazi au ajira mjini, walisharudi shamba (Kibaha, Vikindu, Bagamoyo, Mkuranga na wengine mikoani) na sasa hivi kinachowaleta mjini ni huko kufuatilia mafao yao ambayo nayo sasa hivi imegeuka kuwa kazi ngumu kweli kuyapata!

Kuna baadhi ya watumishi ambao mara kwa mara nikienda katika hizo ofisi kufuatilia madai yangu nimekuwa nikielekezwa niwaone. Nikikutana na hawa watumishi huniambia faili lako halionekani, mara andika barua ya kujieleza kwa nini kuna gaps nyingi katika michango yako, mara barua uliyoiandika imepotea andika nyingine! Kitu kingine cha kushangaza hutoa namba zao za simu na kutaka wapigiwe kwa ajili ya kufanya appointment! Nini maana yake?

Leo asubuhi tarehe 28/4/2020 wanachama wengi tu wanaodai mafao yao wamezuiliwa kuingia ndani na bwana mmoja anaitwa Ally kwa kuambiwa kuwa sasa hivi hapo NSSF Ubungo kuna meneja mpya anayeitwa Fungo, katoa maelekezo kuwa watu wote ambao pesa zao hazijawekwa benki kama walivyoahidiwa na wale wote wanaodai mafao yao wajiandikishe hapo nje na kuacha namba zao za simu!

Kwa kuwa tumeambiwa tuache namba zetu za simu na kuambiwa meneja mpya Bwana Fungo atatupigia simu, naomba hiyo iwe kweli tupu na ifanyike haraka. Pia namwomba Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio naye aliangalie tatizo hili kwa jicho lake la tatu kwani utendaji kazi wa baadhi ya watumishi ndani ya shirika hasa pale Ubungo siyo mzuri! Kwa nini kiutendaji NSSF isiwe kama ilivyokuwa kwa PPF? Kuna shetani gani ndani ya NSSF?

"Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi,
wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi Mungu, na kuitafakari mchana na usiku. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa. Lakini waovu sivyo walivyo; wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu, wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu. Maana Mwenyezi Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi." Zaburi 1:1-6. Ujumbe huu umfikie Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bwana William Erio, meneja mpya wa NSSF Ubungo Bwana Fungo na watumishi wote watendao haki kwa wanachama wa NSSF.
 
Mzee akipewa mafao yake kipindi hiki anakaa ndani vizuri kabisa
Hicho ndicho kinachotakiwa kufanyika haraka. Kuchelewesha malipo kunawafanya wanaodai mafao yao kuanza kutoka nje na kwenda kukopa na kujiongezea matatizo kibao! Sasa hivi na janga hili la korona sijui itakuwaje!
 
WanaJF,

Utendaji kazi wa baadhi ya watumishi NSSF Ubungo haulidhishi kabisa! Nimekuwa nikifuatilia kulipwa mafao yangu toka mwezi 7, 2019 mpaka leo hii sijalipwa napigwa kalenda tu bila hata kujali kuwa mtu huyu anatokea wapi! Manake si kila mtu anaishi na kufanya kazi Dar es Salaam. Watu wengine waliokuwa wakiishi Dar es Salaam baada ya mikataba yao ya kazi kuisha au kufukuzwa kazi, kutokana na hali ngumu ya kimaisha inayokuwepo kwa kutokuwa na kazi au ajira mjini, walisharudi shamba (Kibaha, Vikindu, Bagamoyo, Mkuranga na wengine mikoani) na sasa hivi kinachowaleta mjini ni huko kufuatilia mafao yao ambayo nayo sasa hivi imegeuka kuwa kazi ngumu kweli kuyapata!

Kuna baadhi ya watumishi ambao mara kwa mara nikienda katika hizo ofisi kufuatilia madai yangu nimekuwa nikielekezwa niwaone. Nikikutana na hawa watumishi huniambia faili lako halionekani, mara andika barua ya kujieleza kwa nini kuna gaps nyingi katika michango yako, mara barua uliyoiandika imepotea andika nyingine! Kitu kingine cha kushangaza hutoa namba zao za simu na kutaka wapigiwe kwa ajili ya kufanya appointment! Nini maana yake?

Leo asubuhi tarehe 28/4/2020 wanachama wengi tu wanaodai mafao yao wamezuiliwa kuingia ndani na bwana mmoja anaitwa Ally kwa kuambiwa kuwa sasa hivi hapo NSSF Ubungo kuna meneja mpya anayeitwa Fungo, katoa maelekezo kuwa watu wote ambao pesa zao hazijawekwa benki kama walivyoahidiwa na wale wote wanaodai mafao yao wajiandikishe hapo nje na kuacha namba zao za simu!

Kwa kuwa tumeambiwa tuache namba zetu za simu na kuambiwa meneja mpya Bwana Fungo atatupigia simu, naomba hiyo iwe kweli tupu na ifanyike haraka. Pia namwomba Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio naye aliangalie tatizo hili kwa jicho lake la tatu kwani utendaji kazi wa baadhi ya watumishi ndani ya shirika hasa pale Ubungo siyo mzuri! Kwa nini kiutendaji NSSF isiwe kama ilivyokuwa kwa PPF? Kuna shetani gani ndani ya NSSF?

"Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi,
wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi Mungu, na kuitafakari mchana na usiku. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa. Lakini waovu sivyo walivyo; wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu, wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu. Maana Mwenyezi Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi." Zaburi 1:1-6. Ujumbe huu umfikie Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bwana William Erio, meneja mpya wa NSSF Ubungo Bwana Fungo na watumishi wote watendao haki kwa wanachama wa NSSF.
Nimefuatilia fao la uzazi la mke wangu hadi nimekata tamaa. NSSF wanakera sana.
 
Erio kapigwa chini sasa huyo Fungo ni timing tu maana ni mpenda rushwa anapigwa chini

Back
Top Bottom