Norah Mzeru: Rais Samia ametuheshimisha wanawake, Serikali na CCM katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa madarakani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,031
974
MHE. NORAH WAZIRI MZERU, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Asifu Utendaji Kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kuheshimisha Wanawake, Serikali na CCM Katika Kipindi cha Miaka Mitatu Aliyokaa Madarakani.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni Jasiri, Mzalendo na Mchapakazi, ni lazima Watanzania tumuunge mkono maana hatuna Rais mwingine isipokuwa ni Rais Samia Suluhu Hassan.

"Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa Wanawake na wanaume katika jamii hasa kupigania haki za Wanawake na kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kiuongozi kupitia nafasi alizowateua kumsaidia" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Nimpongeze Sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani katika kipindi chake cha Uongozi tumeshuhudia Mabadiliko makubwa kwa upande wa Wanawake.
Ukiangalia Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kumekua na ongezeko kubwa la Wanawake katika Uongozi, hii ni hatua kubwa Sana na tunapaswa Sana kumpongeza RAIS wetu kwa kustawisha Wanawake" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Sisi kama Wanawake jukumu letu ni kuhakikisha tunamsemea mwanamke mwenzetu vizuri na kumuunga mkono kwa kazi kubwa anazozifanya" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Tuna Rais msikivu Sana, mwanamke mwezetu, ametuheshimisha Sana na tuna kila sababu ya kumpongeza na kuhakikisha tunampa ushirikiano mkubwa Sana na sisi twende naye hadi 2030 ili aendelee kutuvusha zaidi sisi Wanawake" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-14 at 13.36.06.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-14 at 13.36.06.jpeg
    131.2 KB · Views: 3
Ebu atuambie atakae elewa hiyo heshma ilio zungumziwa kuwaheshimisha wanawake...🤨
Au ngoja nisubirie kusoma coment labda nitaelewa.
 
Back
Top Bottom