Nisikilize: Mkeo si ndugu yako

Siku ukiwa haupo duniani hao watoto wako wakaenda kuishi kwa hao unaowaita ndugu utakuwa unalia huko uliko.Mke ana nafasi yake,ukiwa hoi au umelazwa atakayeshinda na wewe usiku kucha ni mke wako ndugu watakuja kukutazama na kisha warudi kwa familia zao.Mpende na mthamini mke wako
 
Mke sio Ndugu yako Kwa sababu ni zaidi ya Ndugu.
Mkeo ndiye Mwanadamu pekee ambaye alikuwa kiapo kukupenda japo sio Ndugu yako.

Wakati Ndugu zako wakisimama na familia zao. Mkeo ndiye atasimama na wewe.

Wakati Ndugu zako wakiwatelekeza Watoto wako. Mkeo ndiye atakayewatunza.

Kuhusu kukengeuka Kwa mke hata Ndugu zako wanaweza kukengeuka.
Huwezi mpima MKE Kwa mzani wa kukengeuka.

Ndugu zako haohao ndio wanauwezo WA kuwadhulumu Watoto wako Mali pale utakapokufa.

Ndugu zako haohao ndio wanaweza kukuloga au kuloga Watoto wako ili wabaki kuwa na Maisha Duni.

Mkeo sio Ndugu yako, Ila ni zaidi ya Ndugu.

Mkigombana na Ndugu au na mzazi unaweza ukalala na Kupata usingizi kabisa, na chakula ukala ukashiba.
Lakini gombana na Mkeo uone hicho chakula au usingizi kama utaupata.

Hapa unazungumzia Mapenzi na upendo wa Mume na Mke.

Mtibeli,

Umenena vyema
 
Acha kudanganya watu na mnafundishwa ubinafsi na wazazi wenu.

Mzazi wako atakuambia sijui wapende ndugu zao ambao yeye ni watoto wake wa damu ...jaribu kuvunja familia na mkeo uliyepata nae watoto kisa ndugu zako halafu baadae hao wanao wakija kupata tabu ndo utaelewa.

Ndugu zako wanaishi huko wanakula na wanakaa sehemu nyingine, wewe na mkeo kama kulala njaa ni wote kama kupata ni wote.

Hakuna ndugu anakufikria akishakuwa na familia ,usijaribu kuharibu familia kisa ndugu zako ngoja uwe mzee ndo utaelewa utakuja kubaki lonely ,ndugu wana maisha yao wewe umevunja ndoa yako kisa kutetea ndugu wapita njia.


Ndugu zako wa damu ( ni watoto wa wazazi wako ) na wana haki ya kuwatunza wazazi wao sio wewe kama ihsani ila sio wewe kuwa makini ,wewe wekeza kwa watoto wako wapate malezi bora kupitia mke bora acha kufundishwa ubinafsi na wazazi wako...Hao watoto wako ndo watakuja kukutunza wewe baadae na ni rahisi kukusaidia kama mzazi .!
 
Mke anafanya vitu vya hatari dhidi yako kama kukubebea mimba , kaangalie wangapi wanakufa kweny kujifungua usiwe kolo unafundishwa ubinafsi na wazazi wako.

Dunia ya sasa ndoa zinakuwa nguvu kwa vile hizi jinsi mbili(mke&ke) zinafundishwa kuchukiana bila ya sababu ili mradi kuvuruga hii chemist iliyobarikiwa ...Basi kama hivyo Babo ako asingekuwa na mke ?

Fanya kazi hata mapacha wanagombana kila mtu na maisha yake , finally watoto wako ndo wapendwa wako ..Je hao watoto utawapata kwa kuzaa na dada ako wa tumbo moja ?
 
Wanaume nisikilize mimi, ukikutana na mwanamke mzuri muoe zaa nae watoto jenga familia pamoja naye.
Anaweza kuwa rafiki yako bora, msiri wako, mfanya biashara wako mshirika.

Na Unaweza kumuona kama mshirika wako wa karibu kwenye maombi pindi utakapomua kwani wanandoa huanza kufanana wakidumu pamoja.

Lakini usisahau nguvu iliyowaunganisha inaweza kuingia kutu kulingana na muda na kubadilika kwa moyo.
Mke wako sio ndugu yako wa damu na upendo wake unaweza kubadilika kuwa chuki ndani ya usiku mmoja.

Nisikilize mimi mpendwa kaka yangu, kwenye Wakati wa mahaba, kwenye kilele cha mafanikio yako, mkumbuke kaka yako aliesimama na wewe wakati haupo imara na umkumbuke dada yako aliekusafisha wakati ukiumwa sana.

Wakumbuke pia waliotumia muda wao kukuambia usitupe maji ya baridi kwenye mgongo wako, mikono yako na kukuandalia maji moto yaliyoilea ngozi yako.

Usiwafungie milango watoto wanapokuja mbele ya uzio wako wakiwa na miguu yenye vumbi na nguo zilizochanika wakitaka msaada wako.

Usizibe pua yako ikiwa wananuka harufu mbaya, usizibe masikio yako ili usisikie matumbo yao yakiunguruma kutokana na kukosa shibe.

Wakaribishe kwa mikono mikunjufu fungua milango yako waite wale juu ya meza yako na watendee kadri ungependa utendewe.

Yajayo ni kama upepo yanaweza kuwa hayatabiriki kabisa unaweza ukajikuta upo kama ayubu wa kwenye biblia ukiwa mtupu mwenyewe kwenye kisiwa cha matatizo.

Dada yako aliyekuokota ukiwa unaumwa hujiwezi Kama mtoto asiye na matumaini atakutafuta akusaidie tena.

Ndugu yako katakushika mkono katika mapito yako yote kwakuwa nguvu iliyowaunganisha kwenye damu itazongwa na upepo lakini kamwe haiwezi kutenganishwa.

Peter Mwaihola
Elvinah Obuya, The Standard Kenya.

View attachment 2724940
Sijakata kuwakumbuka kaka na dada zako lakini huyo mke ambae sio ndugu yako si mnazaa watoto ambao wanakua ndugu zenu naona tungefocus zaidi kwa hao ndugu zetu wapya tuliowatengeneza(watoto) kabla ya kaka na dada ambao na wao pia wamepata wenza wao nakutengeneza ndugu zao wapya (watoto wao)
 
K
Ungeanza kwa kutoa sababu kwa nini tukusikilize wewe na sio Mwenyezi Mungu. Una hekima ipi kumzidi Mungu?

Kiwani nani alikudanganya mkeo ni ndugu yako? Kwa kuwa umerejea habari za maombi nani nitakujibu kwa maandiko:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ ..... Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Maandiko hayajawahi kesema mke ni ndugu, bali mke wako ni WEWE!! Ninyi ni mtu mmoja, hivyo upoamini ndugu kuluko mkeo ni sawa na kujichukia na kujidharau mwenyewe. Ka hiyo hao ndugu hawabadiliki? Unamdharau mwenza wako anayeitunza afya yako ili upate nguvu za kutafutaahizo mali? Unambeza mkeo ambaye huyo ndiye anayekuzaliwa watoto na kukutengenezea familia? Ni heri basi ungezaa na hao ndugu zako ujenge nao ukoo.

Badilika sasa, vinginevyo ndoa itakushinda. Acha kabosa akili mbovu ya kumuona mkeo ni adui, kwqni unalolitamani ndilo hilo hilo litakuwa sehemu ya maosha yako. Be a man, a true husband.
ama bado kuna ubishi tutazame VAR
nakubaliana na wewe 100%, lakini hoja mada kama izi za kumwona mke sio sehemu mwili wako mume na msaidizi wako, zinaibuka kwa kasi sababu ya yanayoendelea na tuyaonayo kwenye ndoa za siku izi.
sasa kwa mtazamo kama huu ndoa itadumu vipi? unaleta adui kwa jina la mke, kuna ndoa hapo? badili mtazamo kwanza
 
Kweli mkuu, sisi majobless tunachekwa mpaka na ndugu wa damu kabisa. Nikioa nitamfanya kama ndugu yangu, tukitengana maana hili lipo nitaoa tena naye nitampenda kama ndugu yangu maana nikizeeka nitakuwa na mke wangu. Ndugu wa sahvi hamna kitu hasa kama unapitia shida.
Hata niwe na hela vipi mke wangu ni kila kitu ila sio ndugu ni wanafiki nikiwa tajiri na nikiwa masikini .

Popote ulipo bby love piga kifua sema kuwa kama mwanaume nimepata .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom