Nishati Safi ya Kupikia, Mwarobaini tunao na ni Bora kuliko Gesi

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,725
19,851
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati ambazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeiweka mwisho sababu ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri, na hili linaweza kufanikiwa ikiwa tutafanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.

Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.

NB: Ushauri wa kuachana na LPG (Mitungi ya Gesi ya Sasa Majumbani) itaacha wengi ambao ndio Biashara yao kwenye hasara ila kwa kurekebisha hilo Serikali inaweza kushauriana nao au kuwawezesha kwa mikopo wawekeze kwenye matengenezo na marekebisho ya vifaa vya Umeme; kwahio badala ya kuagiza majiko kutoka nje assembly plants zinaweza zikawa nchini jambo ambalo litakuza ajira na kuwapa wigo waliopo kwenye biashara ya LPG kunufaika na Umeme - Badala ya Mihan, Oryx, Taifa gesi tutakuwa na Mihan, Oryx, Taifa Cookers
 
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati zifuatazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeliweka mwisho sababu hii ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri na hili linaweza kufanikiwa kama tukifanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.

Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.
Sera ndio inaandaliwa bila shaka wamekusikia watafanyia kazi
 
Makamu wa Rais amesema Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele cha juu kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia hapa nchini kwenye ajenda ya Taifa ya maendeleo pamoja na kuongeza rasilimali kuhakikisha ajenda hiyo inafanikiwa. Amesema Rais amefanya maamuzi makubwa ikiwemo kuunda Kamati ya Kitaifa itakayosimamia utekelezaji wa ajenda hiyo, kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi na kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi za Serikali zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwa siku.

Hapo kwenye Bold ndio point yangu kubwa huenda tunapotea kabla hatujaanza kwa kutoa ruzuku ili watu wanunue gesi (In short ni kutumia Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambao ni mataifa ya mbali) na wasambazaji ambao ni wafanyabiashara wachache...
 
Kama wamezindua mkakati wa Kitaifa wa Nishati safi,hicho kikosi kazi kiliundws mwaka Jana,saizi watapitia na kuunda sera rasmi na sheria ambapo wadau ndio mtoe maoni
 
Ukweli upo wazi kuwa watu waishio mijini iliyopimwa kama Dodoma wanaweza kusambaziwa umeme na hata gas kiurahisi.
Miji nyingine kama Moshi maana ilijengwa na mkoloni inaweza kuwa sawa kwa hii style.
Tukija miji nyingine ni kanjanja. Kwanza bararaba inaingia chooni, Gholofa linaangaliana na bati la mgerumani na mwingereza.
Tukisema tutengeneze kwanza miundo mbinu, tutachukua miongo kama miwili kufanikisha hilo.
Kazi kwa ma Engineer wetu wakae watengeneze masterplan mpya kuwezesha kufikia watu wote.

Vijijini watu wameanza kwa wingi kubadili mtindo wa wamaisha pole pole. Ingawa kwa kusuasua maana kuifikisha gas kijijini ni ghalama kubwa. wachache wanajitahidi inafika na inasubiri shughuli kubwa iwepo ndo itumike.
Baadhi ya nyumba ndo mtindo wa maisha wa kila siku maana nyumbani unakuta bibi na msaidizi wake basi. Wageni wanapokaribia kuja wanatuma pesa za kununulia kuni za kuchemsha maji ya kuoga na vyakula vya fasta.
Hapo jikoni ndo kunatumika na mara nyingi ni mkaa.
 
Kama wamezindua mkakati wa Kitaifa wa Nishati safi,hicho kikosi kazi kiliundws mwaka Jana,saizi watapitia na kuunda sera rasmi na sheria ambapo wadau ndio mtoe maoni
Tunajua duniani mambo yanavyokwenda na stake-holders (wadau), lobbyist n.k. inategemea wananufaika vipi na current status quo..., kuna watu wamewekeza kwenye gesi LPG na wameweka mabilioni kama sio matrilioni ya pesa..., ili kufuata njia hii ambayo ina faida kubwa kwa mteja (mwananchi) ambaye ni un-informed inabidi mtu wa kusimamia hili awe mzalendo wa kweli...., Bila hivyo amini nakwambia utaona tunaanza kupigia promo mitungi ya gesi tofauti tofauti.....
 
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati zifuatazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeliweka mwisho sababu hii ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri na hili linaweza kufanikiwa kama tukifanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.

Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.
Naunga mkono hoja! Majiko ya induction cooker yapo mpaka ya 12 Volts na yana weza kuwa powered na solar pannel. Pia Watanzania wanatakiwa wawezeshwe kwenye Bio Gas systems zinazozalisha Ges kutokana na mabaki ya Chakula, mimea na vinyesi vya wanyama.... mitungi ya LPG bado ni mzigo kwa familia nyingi na hata hawa mama Ntilie. Ipo haja hawa mama Ntilie wapewe Biogas system waweze zalisha ges ya kupikia kutokana na mabaki ya vyakula na mboga mboga wanazopika katika kazi zao
 
Attachments

  • IMG_9839.jpeg
    IMG_9839.jpeg
    27.4 KB · Views: 3
  • IMG_9836.jpeg
    IMG_9836.jpeg
    29.7 KB · Views: 3
  • IMG_9837.jpeg
    IMG_9837.jpeg
    33.9 KB · Views: 3
  • IMG_9834.png
    IMG_9834.png
    102.2 KB · Views: 3
  • IMG_9833.png
    IMG_9833.png
    102.7 KB · Views: 3
  • IMG_9830.png
    IMG_9830.png
    89.8 KB · Views: 3
  • IMG_9832.png
    IMG_9832.png
    124.1 KB · Views: 2
Ukweli upo wazi kuwa watu waishio mijini iliyopimwa kama Dodoma wanaweza kusambaziwa umeme na hata gas kiurahisi.
Miji nyingine kama Moshi maana ilijengwa na mkoloni inaweza kuwa sawa kwa hii style.
Tukija miji nyingine ni kanjanja. Kwanza bararaba inaingia chooni, Gholofa linaangaliana na bati la mgerumani na mwingereza.
Ndio maana nikasema njia pekee ni umeme sababu nadhani kutokana na vyanzo vyetu na tukimaliza Bwawa tutakuwa na double capacity kwahio tunahitaji watumiaji na kila sehemu yenye mipango miji kuna plan ya nguzo kufika hivyo umeme kufika....
Tukisema tutengeneze kwanza miundo mbinu, tutachukua miongo kama miwili kufanikisha hilo. Kazi kwa ma Engineer wetu wakae watengeneze masterplan mpya kuwezesha kufikia watu wote.
Suala la Gesi Asilia nadhani tuachane nalo kabisa, miundombinu isipelekwe kwenye kila kaya bali ipelekwe sehemu chache husika (kwenye grid ili kuzalisha umeme) na kwenye masheli / ili kujazia magari CNG
Vijijini watu wameanza kwa wingi kubadili mtindo wa wamaisha pole pole. Ingawa kwa kusuasua maana kuifikisha gas kijijini ni ghalama kubwa. wachache wanajitahidi inafika na inasubiri shughuli kubwa iwepo ndo itumike.
Baadhi ya nyumba ndo mtindo wa maisha wa kila siku maana nyumbani unakuta bibi na msaidizi wake basi. Wageni wanapokaribia kuja wanatuma pesa za kununulia kuni za kuchemsha maji ya kuoga na vyakula vya fasta.
Hapo jikoni ndo kunatumika na mara nyingi ni mkaa.
Point yangu gesi LPG (Taifa, Mihan, Oryx) n.k. tuachane nazo kabisa hizo zinatokea kwenye mafuta (petroli) ambayo sisi hatuna na tunaagiza kwa kutumia Pesa ya Kigeni, kwahio tuachane na hii habari ya gesi kabisa na tuwekeze kwenye umeme percent 100
 
Makamu wa Rais amesema Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele cha juu kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia hapa nchini kwenye ajenda ya Taifa ya maendeleo pamoja na kuongeza rasilimali kuhakikisha ajenda hiyo inafanikiwa. Amesema Rais amefanya maamuzi makubwa ikiwemo kuunda Kamati ya Kitaifa itakayosimamia utekelezaji wa ajenda hiyo, kuanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia ili kuweka ruzuku itakayowawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu bei ya gesi na kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi za Serikali zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwa siku.

Hapo kwenye Bold ndio point yangu kubwa huenda tunapotea kabla hatujaanza kwa kutoa ruzuku ili watu wanunue gesi (In short ni kutumia Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambao ni mataifa ya mbali) na wasambazaji ambao ni wafanyabiashara wachache...
Mama anaupiga mwingi 😁
 
nishati nafuu kwa mtanzania wa hali ya chini ni ipi?
Kwa sasa inategemea mazingira ila ni kuni au mkaa kama wakiupata...., Ila kama tukiamua itakuwa ni Umeme tatizo lipo kwenye Serikali yenyewe ambayo inataka kutoa ruzuku kwenye gesi ingetoa ruzuku hio kwenye umeme
 
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati zifuatazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeliweka mwisho sababu hii ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri na hili linaweza kufanikiwa kama tukifanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.

Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.
Hii ni Story of Change?
 
Mawazo yako ni mazuri sana. Kama ungeiweka kwenye story of change hakika ungepata kura yangu.
 
Naunga mkono hoja! Majiko ya induction cooker yapo mpaka ya 12 Volts na yana weza kuwa powered na solar pannel.
Unajua pia kuna suala la practicability na urahisi yaani urahisi wa kutumia..., sasa kama mtu anaweza kuwasha switch ya umeme na kupika kila mtu atafanya hivyo, kuliko ukianza kumwambia tena mambo ya solar ni mnyororo mrefu sana..., Wenye solar kama wanazo wawauzie Tanesco kwenye grid

Wengine kazi yetu iwe ni kuwasha tu na kupika bila kujali nishati hio inatokea wapi
Pia Watanzania wanatakiwa wawezeshwe kwenye Bio Gas systems zinazozalisha Ges kutokana na mabaki ya Chakula, mimea na vinyesi vya wanyama....
Naam Biogas ni nzuri sana kwa mazingira sababu itapunguza uchafu mwingine kwenda dampo na baadae kutumika kama mbolea..., lakini urahisi wa mtu kufanya hili kuanzia kuzalisha mwenyewe wengi hawatafanya (sababu inahitaji uangalizi) kwahio hawa wengi tuwape option ya gharama nafuu kuliko zote ambayo itakuwa umeme
mitungi ya LPG bado ni mzigo kwa familia nyingi na hata hawa mama Ntilie. Ipo haja hawa mama Ntilie wapewe Biogas system waweze zalisha ges ya kupikia kutokana na mabaki ya vyakula na mboga mboga wanazopika katika kazi zao
Hii hata tukisema tuitoe bure kwa watu wapikie.., haitakuwa bure sababu kodi zetu zitatumika kununulia hii gesi kutoka ughaibuni ili tuje tupewe bure (wanachukua kwa mkono wa kulia na wanakupa kwa mkono wa kushoto)
 
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu.

Nishati zilizopo:
Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa kupikia inategemea upatikanaji na gharama ya Nishati hio. Kwa mtumiaji wa mwisho gharama anayojali ni ya kifedha ingawa kwa mtizamo wa mazingira, gharama ya kifedha inaweza kuwa ndogo lakini athari za hio nishati zikawa ni kubwa zaidi. Kwa mazingira ya Tanzania Nishati zifuatazo zinaweza kupatikana na kutumika ni kama ifuatavyo.

Kuni
Ni nishati chafu, na kutokana na moshi ina athari za kiafya kwa mtumiaji, vilevile athari za kimazingira kama kuni hizo zinapatikana kwa kukata miti na sio kutumia mabaki ya miti.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Miti
Badala ya kutumia kuni moja kwa moja miti hiyo au mabaki ya miti yakifanyiwa carbonization yaani kuchomwa mkaa, nishati hii inakuwa safi kwa mtumiaji kwa kupunguza athari za kiafya ingawa bado kunakuwa na athari ya kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa, jambo ambalo athari yake kimazingira ni kubwa sana.

Mkaa (Carbonization) kutoka kwenye Mabaki ya Mimea, Na Mikaa Mbadala
Sababu hii haitumii miti na kukata misitu athari yake kwa mazingira haipo na vilevile inaweza kusaidia kwa kuondoa mabaki / uchafu ambao hautakiwi na kuubadilisha kuwa nishati. Angalizo; Kutengeneza Nishati hii hutumia pia Nishati, hivyo ukiangalia mtiririko mzima huenda Nishati hii isiwe safi kama inavyodhaniwa kutokana na matumizi ya Nishati nyingine kutengeneza hii Nishati.

Mafuta ya Taa, Methanol na Ethanol
Kwa mafuta ya Taa nishati hii tunainunua kutoka nje hivyo kuna gharama ya manunuzi na katika usafirishaji wake mnyororo mzima ni wa gharama. Watu wanaweza kutengeneza Methanol / Ethanol kama vile wanavyopika gongo ila myonyoro mzima wa upatikanaji wa hio nishati ni gharama.

Gesi Asilia (Biogas) na Gesi ya Mtwara
Gesi asilia mtu mmoja mmoja mfugaji au sehemu kama kwenye mashule wanaofuga au kwenye Magereza wanaweza kutumia Kinyesi na kutengeneza Biogas kwa mapishi yao, hii itasaidia katika kuondoa mabaki (uchafu) na kuweza kubadilisha kuwa mbolea. Gesi asilia ya Mtwara inaweza kutumika kwa ufanisi iwapo tu itafungwa moja kwa moja kutoka kwenye Source, na kupelekwa kwa mabomba (kama vile mfumo wa maji ulivyo) mpaka kwa mtumiaji, ingawa utengenezaji wa miundombinu hiyo ni gharama sana na kama kutakuwa kunatokea uvujaji wa hii Gesi tutakuwa tunachafua mazingira kwa gesi hio (methane) kuingia moja kwa moja kwenye mazingira hivyo badala ya kuwa nishati Safi itakuwa moja ya Nishati Chafu....

Gesi ya Mitungi (LPG)
Hii ndio nishati inayopigiwa chapio na wengi na ndio inayotumika majumbani, lakini ina hasara kuu mbili kwa taifa letu, Moja ni kwamba tunaagiza kutoka nje hivyo inahitaji gharama ya kununua, na mbili hata ikishafika usafirishaji wa kutoka point moja mpaka nyingine bado ni matumizi ya Nishati. Na gharama yake bado ni kubwa kuliko uwezo wa watu ndio maana watu wanatumia Nishati nyingine. Na tukisema tuweke ruzuku kusaidia watu kununua, tatizo bado lipo palepale ukizingatia ni pesa hizo hizo tunazochukua kwa hao wasiojiweza kama Kodi na kuwarudishia kama ruzuku ili wanunue kitu ambacho kinanufaisha mataifa ya nje pindi tunapoagiza hii gesi

Umeme
Hii nimeliweka mwisho sababu hii ndio nishati safi ya kupikia kuliko zote kulingana na mazingira yetu ya Tanzania, kama tutaweza kutumia vyanzo vyetu vizuri na hili linaweza kufanikiwa kama tukifanya yafuatayo:-

  • Watanzania Wengi ndio Wanafikiwa na Umeme kuliko Nishati nyingine yoyote: Miundombinu tayari ipo watu karibia wote wana plug za umeme majumbani kwao hivyo tunaweza kutumia hio nishati kama umeme utakuwa wa gharama nafuu sana, Kama tukisema tushushe bei kwenye gesi tunaweza kushusha bei mpaka ile bei tunayonunulia lakini umeme ambao tunazalisha tunaweza kupaga bei za units bila kutegemea soko la dunia

  • Vifaa vya Umeme Vipatikane kwa Gharama Nafuu / Kutoa Ruzuku; Kama tukiondoa Ushuru au kutoa Ruzuku katika vifaa vya umeme basi ufanisi wa Kupikia umeme utakuwa zaidi ya Gesi; watu watatumia Oven kuokea, Watatumia Rice Cooker kupikia Wali; Flyers kupikia Chips na Jug Kettles kuchemshia Maji n.k.

  • Matumizi ya Induction Cooker; Ingawa kwa kipindi kirefu majiko ya gesi yalikuwa yanapiku majiko ya umeme katika ufanisi (yaani ilikuwa inachukua muda mchache kwa gesi kupata moto unaotaka wakati coil ya umeme inachukua muda mrefu) ila kwa sasa hivi induction cooker ni instant (wakati huo huo) ukiwasha unapata joto unalotaka na moto unawaka pale tu kwenye sufuria pengine pote kunakuwa hakuna moto (hivyo hakuna upotevu wa nishati)

  • Badala ya Kutoa Ruzuku watu Wanunue Gesi za Kunufaisha wengine Tutoe Ruzuku watu Waunganishwe na Umeme na Kununua Vifaa vya Umeme; Nimeona kwenye Habari Serikali imeanzisha mfuko wa Nishati safi…, sasa badala ya kutumia mfuko huo na Kodi zetu kunufaisha wauzaji wa gesi ambapo mwisho wa siku ni mataifa ya nje tunaweza kutumia pesa hizo kuhakikisha kila mtu anaunganishwa na umeme na umeme unakuwa bei rahisi na vifaa vya umeme kuwekewa ruzuku.

Hitimisho
Kwa Mazingira yetu ya Tanzania Nishati ambayo inaweza ikawa safi ya kupikia na ambayo ni practical na tunaweza kuipata kwa haraka na urahisi ni kwa kutumia Umeme, badala ya kuhangaika na kusambaza gesi asilia majumbani kwa watu kwenye mabomba, ambayo itakuwa ni gharama kubwa tunaweza kusambaza gesi hio asilia mpaka kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ili Gesi hio Ibadilishwe kuwa umeme na kuungana na vyanzo vingine (maji, solar, upepo n.k.) na kusambazwa kwenye kila Kaya tayari kwa watu kupikia.
Naongezea Kupikia Umeme ni nafuu kuliko gesi
 
Hii ni Story of Change?
Hapana mkuu hii ni habari tu ambayo ningependa sisi kama watanzania tupitie njia hii ili kufika tunatakiwa kufika..., kwahio ipo huru kwa yoyote kuichukua na kuifanyia kazi katika mazingira yetu..., Ukizingatia sina hati miliki ya haya mambo yote yapo wazi kwa yoyote kuweza kuyaona (mwenye macho)

Ninachoomba ni wengi mtaani labda ambao hawana uelewa wapate huu uelewa ili baadae wakisema wanapewa pesa ili kununua gesi waulize kwanini pesa hizo tusiwekeze kwenye Nishati ya umeme (ambayo kama taifa tunaweza kuzalisha mpaka chenji ikabaki)
 
Naongezea Kupikia Umeme ni nafuu kuliko gesi
Tena ni safi kuliko LPG ambayo tunaagiza kutoka nje (meli zinatumia mafuta) inafika dar inasambazwa kwenye depiots nishati nyingi inatumika kwenye kujaza hio mitungi..., inasafirishwa mikoani kwa kutumia petroli n.k. inawekwa depot..., mwenye kutumia anapigia boda ili amletee delivery (inatumia nishati tena)

Yaani mtitiriko mzima kimazingira huenda sio msafi kama tunavyodhania.... Wakati tukija kwenye umeme kama unatokea kwenye Bwawa au unatokea kwenye gesi asilia tunakuwa tumeokoa mazingira kwenye maeneo tofauti ya mnyororo kabla ya kumfikia mteja
 
Back
Top Bottom