Nini Hatima ya wanakijiji zaidi ya 2000 wa Tondoroni, Kisarawe waliopo katika mgogoro wa aridhi na JWTZ?

Jan 28, 2024
97
133
MGOGORO WA ARIDHI TONDORONI
Kesi ya ardhi namba 85 ya mwaka 2016, iliyowahusisha wanakijiji zaidi ya 700 wa Tondoroni dhidi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Leo(03.04.24)mahakama kuu chini ya Jaji Luvanda imetupiliwa mbali kwa kufunguliwa nje ya muda (Time barred'). Mgogoro huu wa ardhi wa Tondoroni na JWTZ ni miongoni mwa migogoro ya ardhi ya muda mrefu zaidi hapa nchini, ukiwa umedumu kwa zaidi ya miaka 35 na kuendelea kurindima katika viunga vya mahakamani kwa zaidi ya robo karne.

Mwanzo wa mgogoro huu unarudi nyuma hadi mwaka 1986, wakati serikali ilipotoa agizo kwa wanakijiji wa Tondoroni kuondoka kwenye maeneo yao kwaajili ya maslahi ya umma (Under S.3 & 4(1)(a) of Land Acquisition Act (LAA)), huku ikiwaahidi fidia (as per S 11 of LAA). Hata hivyo, ahadi ya fidia haikutimizwa, na kupelekea wanakijiji 144 kufungua kesi dhidi ya serikali mnamo mwaka 1996 wakidai haki yao ya fidia. Katika kesi hiyo, serikali haikupinga madai hayo ya fidia, na mahakama ilitoa hukumu ya kuwataka kulipa fidia ya jumla ya Tsh. 3.5 bilioni. Pamoja na hukumu hiyo, hadi kufikia mwaka 2008, serikali ilikuwa imelipa sehemu ndogo tu ya fidia hiyo, Tsh. milioni 50.

Wanakijiji hao waliamua kufuatilia utekelezaji wa hukumu hiyo mbele ya Jaji Mihayo, ambaye katika hali ya kushangaza, aliamua kwamba serikali ilikuwa imetekeleza hukumu kwa kuwalipa wanannchi hao fidia. Hata hivyo, wanakijiji hao hawakuridhika na uamuzi huo na walikata rufaa katika Mahakama ya Rufani. February 2010, Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Kileo, waliamua kwamba serikali haikuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha malipo ya fidia, na hivyo, serikali iliamriwa kulipa sehemu ya fidia iliyobaki. Case link🔗👉 https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzca/2010/21/eng@2010-01-29/source.)

Ili kuelewa huu mgogoro. Kabla sijaendelea zaidi ngoja nizungumzie historia ya eneo lenye mgogoro kwa ufupi sana. Ipo hivi, inaonekana katika miaka ya nyuma eneo hilo lilikua halina watu na ilikua ni virgin forest tu. Ni mpaka miaka ya 1970s ndio watu walianza kusafisha mapori na kutengeneza maeneo yao ya makazi. Waliendelea kuishi kwa amani mpka ilipofika miaka ya 1980s baada ya vita ya kagera kumalizika na wanajeshi wa Tz kurudi nnchini. Mind you , katika vita ya kagera watu wengi sana waliingia jeshini kwa njia ya kujitolea na ile iliyokua ya lazima kwaajili ya kwenda kupigana vita hiyo. Hii ilipelekea ongezeko kubwa la maafisa wa jeshi na uhitaji mkubwa wa ongezeko la kambi za kijeshi. Kwaio baada ya wanajeshi kurudi, moja ya maeneo serikali iliyachukua kwaajili ya kufanya kambi za kijeshi ni pamoja na Tondoroni kwakutoa tamko la kuwataka wakazi wake wa hame kwajili ya maslahi ya umma mnamo 1986 kama ambavyo tulikwishaona hapo mwanzo (Logically; ili eneo lingekua la serikali before 1986, serikali haikua na haja ya kuissue notice ya compulsory acquisition under S 6 of LAA) .

Tuendelee na story sasa. Baada ya maamuzi ya maakama ya rufani mwaka 2010 hakuna uthibitisho kama serikali iliwalipa wanannchi hao ama laa, lakini wannchi hao waliendelea kubaki kuishi katika maeneo hayo bila ghasia yeyote mpaka mambo yalipobadilika October 2015 baada ya JWTZ kuwavamia wanakijiji hao wa Tondoroni, kubomoa na kuwafukuza katika makazi yao, kwamadai kuwa wanakijiji hao walikua wamevamia katika eneo hilo lililokua linamilikiwa na jeshi.

Uvamizi huu ulisababisha mgogoro kuanza upyaa na kupelekea wanannchi zaidi ha 700+ kufungua kesi namba 85 ya mwaka 2016 katika mahaka kuu Dar Es Salaam, Division ya Aridhi dhidi ya Wizara ya Ulinzi na mwanasheria mkuu wa serikali (AG), wakiitaka mahakama itamke kwamba wao (wanakijiji) ndio wamiliki halali wa eneo hilo la mgogoro na kuitaka JWTZ kuwalipa fidia zao kutokana na uaribifu uliofanywa ikiwemo kuvunja nyumba. Upande wapili serikali ilikuja na hoja mbili ambazo ndo zimekua kiini cha kesi No. 85 ya 2016 . Hoja hizo ni:​
  1. Tondoroni si kijiji tena kwani kilisajiliwa kimakosa mwaka 1993 katika eneo la jeshi na TAMISEMI hivyo kupelekea kufutiwa usajili huo mnamo mwaka 2002 na kutolewa kenye gazeti la serikali rasmi 2014.​
  2. Tasmini zilifanyika kwanzia 1988 - 1999 na wanakijiji wote walilipwa fidia na stahiki zao katika miaka hiyo mpaka 2002 ambapo serikali ilitoa jumla ya Tsh. 712 Milion kwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe (wakipindi hicho) ili kulipa fidia hizo na zililipwa in full na kupewa notisi ya kuhama (notice of vacate).​
Hoja hizi mbili zilimvutia Jaji Makani na kupelekea kuitupilia mbali kesi hii mnamo August 2021. (Full Judgment 👉 https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzhclandd/2021/418/eng@2021-08-20/source). Lakini maamuzi haya hayakuwafuraisha wanakijiji 681 kati ya wale 707 wa Tondoroni na kuwapelekea kukata rufaa namba 494 ya mwaka 2021 katika mahakama ya rufani. Lakini kabla ya uamuzi kutoka, mgogoro huu ulizidi kuwa tatizo mpka kupelekea aliyekua mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Nickson Simon (Nikki wa Pili) kwenda kujaribu kutatua mgogoro huo September mwaka 2022 ambapo wanakijiji waliomba mgogoro huu kumalizwa njee ya mahakama.

View: https://youtu.be/tk2konIr0Jg?si=7h7cedWUkMRFEmEo.

November 2023, maamuzi ya rufaa namba 494 ya 2021 mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mwandambo yalitoka ambapo yalifuta maamuzi ya Jaji Makani wa mahakam kuu kwa makosa ya utaratibu (Procedure Irregularities) na kuirudisha kesi namba 85 ya 2016 katika mahakama kuu kwaajili ya kusikilizwa upya na jaji mwingine kwa namna jaji huyo atavyoona inafaa. https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzca/2023/17876/eng@2023-11-22/source).

Hapa sasa ndipo kesi namba 85 ya 2016 ilipoangukia mikononi mwa Jaji Luvanda ambae maamuzi yake aliyatoa Juzi (28.03.24) ambapo kwanza amesema HAKUNA TENA kijiji kinachoitwa Tondoroni. Hapa nigusie jambo, tukumbuke watu walianza kuishi Tondoroni 1970s na kupelekea serikali kulichukua eneo hilo mwaka 1986 kwa maslahi ya umma (kujenga kambi ya jeshi), kwaio mwaka 1986 ndio rasmi Tondoroni ilichukuliwa na serikali (JWTZ), hivyo ni kweli wakati TAMISEMI inakisajili Tondoroni kama kijiji mwaka 1993 wakati TAMISEMI tayari eneo hilo lilikua ni la jeshi. Lakini tukumbuke haya ni makosa ya serikali yenyewe (TAMISEMI) na hakuna chakuwalaumu wanakijiji wa Tondoroni katika hili.

Kuhusu kesi ya serikali kuingilia (trespass) eneo lao (wanakijiji) na fidia, Jaji Luvanda amasema hayo ni makosa ya Tort na yanatakiwa kufunguliwa ndani ya miaka mitatu (Item 6 Part I of Schedule of LLA) na huku kesi hii ilifunguliwa 2016 ikiwa ni zaidi ha miaka 30 kupita toka mgogoro utoke (yani 1986), na mwisho kabisa akaitupilia mbali kwakuwa njee ya muda. (Full Judgment 👉 Said H. Lipite & 4 Others vs The Ministry of Of Defence & Another (Land Case No. 85 of 2016) [2024] TZHCLandD 142 (28 March 2024).
Lakini Je, Chanzo cha mgogoro (cause of action) kilichopelekea kesi No. 85 kufunguliwa mwaka 2016 kilitokea miaka 30 nyuma kama Jaji Luvanda alivyoamua? Nadhani kama umefatilia vizuri story nzima hapo juu basi jibu la swali hili tayari utakua nalo. Lakini maswali ambayo majibu yake bado magumu ni pamoja na
JE, Ni kweli wanakijiji wa Tondoroni walilipwa fidia zao🤔?
JE, Ni nini na lini ni mwisho wa mgogoro huu🤔?


 

Attachments

  • Ally Juma Mwangomba Others vs The Attorney General (Civil Appeal 60 of 2009) 2010 TZCA 21 (29...pdf
    308 KB · Views: 1
  • Said H Lipite and 4 Others vs The Ministry of Defence and Another (Land Case 85 of 2016) 2021 ...pdf
    1 MB · Views: 2
  • Said H Lipite 4 Others vs The Ministry of Of Defence Another (Land Case No 85 of 2016) 2024 ...pdf
    685.6 KB · Views: 2
Kesi ya ardhi namba 85 ya mwaka 2016, iliyowahusisha wanakijiji zaidi ya 700 wa Tondoroni dhidi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Leo mahakama chini ya Jaji Luvanda imetupiliwa mbali kwa kufunguliwa nje ya muda (Time barred'). Mgogoro huu wa ardhi wa Tondoroni na JWTZ ni miongoni mwa migogoro ya ardhi iliyo na historia ndefu nchini, ukiwa umedumu kwa zaidi ya miaka 35 na kuendelea kushughulikiwa mahakamani kwa zaidi ya robo karne.

Mwanzo wa mgogoro huu unarudi nyuma hadi mwaka 1986, wakati serikali ilipotoa agizo kwa wanakijiji wa Tondoroni kuondoka kwenye maeneo yao kwaajili ya maslahi ya umma, huku ikiwaahidi fidia. Hata hivyo, ahadi ya fidia haikutimizwa, na katika mwaka 1996, wanakijiji 144 waliamua kufungua kesi dhidi ya serikali kudai haki yao ya fidia. Katika kesi hiyo, serikali haikupinga madai hayo ya fidia, na mahakama ilitoa hukumu ya kuwataka kulipa fidia ya jumla ya Tsh. 3.5 bilioni. Pamoja na hukumu hiyo, hadi kufikia mwaka 2008, serikali ilikuwa imelipa sehemu ndogo tu ya fidia hiyo, Tsh. milioni 50.

Wanakijiji hao waliamua kufuatilia utekelezaji wa hukumu hiyo mbele ya Jaji Mihayo, ambaye katika hali ya kushangaza, aliamua kwamba serikali ilikuwa imetekeleza hukumu kwa kuwalipa wanannchi hao fidia. Hata hivyo, wanakijiji hao hawakuridhika na uamuzi huo na walikata rufaa katika Mahakama ya Rufani. February 2010, Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Kileo, waliamua kwamba serikali haikuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha malipo ya fidia, na hivyo, serikali iliamriwa kulipa sehemu ya fidia iliyobaki. (Full Judgment 👉 https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzca/2010/21/eng@2010-01-29/source.)

Ili kuelewa huu mgogoro. Kabla sijaendelea zaidi ngoja nizungumzie historia ya eneo lenye mgogoro kodogo. Ipo hivi, inaonekana katika miaka ya nyuma eneo hilo lilikua halina watu na ilikua ni virgin forest tu. Ni mpaka miaka ya 1970s ndio watu walianza kusafisha mapori na kutengeneza maeneo yao ya makazi. Waliendelea kuishi kwa amani mpka ilipofika miaka ya 1980s baada ya vita ya kagera kumalizika na wanajeshi kurudi Tz. Kwaio baada ya wanajeshi kurudi, moja ya maeneo serikali iliyachukua kwaajili ya kufanya kambi za kijeshi ni pamoja na Tondoroni kwakutoa tamko la kuwataka wakazi wake wa hame kwajili ya maslahi ya umma mnamo 1986 kama ambavyo tulikwishaona hapo mwanzo.

Tuendelee na story sasa. Baada ya maamuzi ya maakama ya rufani mwaka 2010 hakuna uthibitisho kama serikali iliwalipa wanannchi hao ama laa, lakini wannchi hao waliendelea kubaki kuishi katika maeneo hayo bila ghasia yeyote mpaka mambo yalipobadilika October 2015 baada ya JWTZ kuwavamia wanakijiji hao wa Tondoroni, kubomoa na kuwafukuza katika makazi yao, kwamadai kuwa wanakijiji hao walikua wamevamia katika eneo hilo lililokua linalo milikiwa na jeshi.

Uvamizi huu ulisababisha mgogoro kuanza upyaa na kupelekea wanannchi zaidi ha 700+ kufungua kesi namba 85 ya mwaka 2016 katika mahaka kuu Dar Es Salaam, Division ya Aridhi dhidi ya Wizara ya Ulinzi na mwanasheria mkuu wa serikali (AG), wakiitaka mahakama itamke kwamba wao (wanakijiji) ndio wamiliki halali wa eneo hilo la mgogoro na kuitaka JWTZ kuwalipa fidia zao kutokana na uaribifu uliofanywa ikiwemo kuvunja nyumba. Upande wapili serikali ilikuja na hoja mbili ambazo ndo zimekua utata mkubwa mpake leo hii, huu mgogoro kufikia hapa. Hoja hizo ni:​
  1. Tondoroni si kijiji tena kwani kilisajiliwa kimakosa mwaka 1993 katika eneo la jeshi na TAMISEMI hivyo kupelekea kufutiwa usajili huo mnamo mwaka 2002 na kutolewa kenye gazeti la serikali rasmi 2014.​
  2. Tasmini zilifanyika kwanzia 1988 - 1999 na wanakijiji wote walilipwa fidia na stahiki zao katika miaka hiyo mpaka 2002 ambapo serikali ilitoa jumla ya Tsh. 712 Milion kwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe (wakipindi hicho) ili kulipa fidia hizo na zililipwa in full na kupewa notisi ya kuhama (notice of vacate).​
Hoja hizi mbili zilimvutia Jaji Makani na kupelekea kuitupilia mbali kesi hii mnamo August 2021. (Full Judgment 👉 https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzhclandd/2021/418/eng@2021-08-20/source). Lakini maamuzi haya hayakuwafuraisha wanakijiji 681 kati ya wale 707 wa Tondoroni na kuwapelekea kukata rufaa namba 494 ya mwaka 2021 katika mahakama ya rufani. Lakini kabla ya uamuzi kutoka, mgogoro huu ulizidi kuwa tatizo mpka kupelekea aliyekua mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Nickson Simon (Nikki wa Pili) kwenda kujaribu kutatua mgogoro huo September mwaka 2022.
View: https://youtu.be/tk2konIr0Jg?si=7h7cedWUkMRFEmEo.

November 2023, maamuzi ya rufaa namba 494 ya 2021 mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mwandambo yalitoka ambapo yalifuta maamuzi ya Jaji Makani kwa makosa ya utaratibu (Procedure Irregularities) na kuirudisha kesi namba 85 ya 2016 mahakama kuu kwaajili ya kusikilizwa upya na jaji mwingine. (Full Judgment 👉 https://tanzlii.org/akn/tz/judgment/tzca/2023/17876/eng@2023-11-22/source).

Hapa sasa ndipo kesi namba 85 ya 2016 ilipokabidhiwa kwa Jaji Luvanda ambae maamuzi yake yametoka Juzi tareh 28, March 2024 na kuachiliwa mtandaoni (Tanzlii) leo. Ambapo kwanza amesema HAKUNA TENA kijiji kinachoitwa Tondoroni na kuhusu kesi na fidia, Jaji Luvanda amasema hayo ni makosa ya Tort na yanatakiwa kufunguliwa ndani ya miaka mitatu (Item 6 Part I of Schedule of LLA) na huku kesi hii ilifunguliwa 2016 ikiwa ni zaidi ha miaka 30 kupita toka mgogoro utoke, na mwisho kabisa akaitupilia mbali kwakuwa njee ya muda. (Full Judgment 👉 Said H. Lipite & 4 Others vs The Ministry of Of Defence & Another (Land Case No. 85 of 2016) [2024] TZHCLandD 142 (28 March 2024)).

JE? Ni nini na lini ni mwisho wa mgogoro huu🤔?
JE? Ni kweli wanakijiji wa Tondoroni walilipwa fidia zao🤔?

Hilo lilikuwa pori, nyie matapeli km matapeli km matapeli mengine mnatakiwa mkamatwe
 
Idadi ya watu Tanzania ina double kila miaka 23.

Kwa sasa tunaongeza kadiri ya watu milioni 2 kila mwaka. Annual population growth ya 3% kwa watu milioni 69 - 70.

Kila miaka 5 Tanzania inaongeza watu zaidi ya population ya Sweden ya sasa ya watu milioni 10.

Kwa kasi hii, kufikia mwaka 2050 Tanzania itakuwa na watu zaidi ya milioni 140. Dar es salaam inakadiriwa kufikisha watu takriban milioni 14 mwaka 2035. Karibu mara mbiki ya idadi ya sasa.

Hii migogoro ya ardhi itazidi tu.

Halafu utaambiwa "nchi kubwa hii, tunahitaji watu".
 
Back
Top Bottom