#COVID19 Nini hasa lilikuwa kosa la Hayati Magufuli kwenye ishu ya COVID-19 ?

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari JF,

JPM aliamini corona itaendelea kuwepo na tutaishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine, kiuhalisia ndivyo ilivyo corona ipo na idadi ya watu waliopata chanjo ni ndogo sana na watu walishapata kinga asilia sasa hivi sio tishio tena. Lakini bado watu wakiwemo madaktari wanalaumu approach yake kwenye ishu.

Swali langu ni lipi lilikuwa kosa lake?

Je, ni kutoweka lock down?

Je, ni kupinga chanjo?

Je, ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine ?

Kwangu Mimi mnyonge mnyongeni katika hili alistahili tuzo.
 
Juzi nimemsikia Samia akimsifia eti uchumi wetu haukushuka kwa sababu ya shujaa Magufuli hakufunga nchi kipindi cha COVID 19 huko nyuma aliungana na BAVICHA kumsema eti tumetengwa, Samia hana anachojua kwenye nchini hii

USSR
 
Reaction ya JPM kwny gonjwa la Corona anastahiki alama zote I.e mia fil mia

Allah alimpa ilhamu ya hali ya juu sana …alipata ujasiri na uthubutu wa hali ya juu sana kuliko wasomi, watabiri na waganga na waganguzi

Kile chuma kilikuwa na flavor yake ya kipekee sana hata Julius angekuwepo kuna mambo angetakiwa ajifunze kwa yule Mwamba

nime miss sana zile hotuba za kutoka moyoni ambazo ndio hasa za Rais

Ma Rais wote walikuwa wanahutubia Hotuba za Ikulu kasoro John peke yake ndo alikuwa anatoa hotuba zake mwenyewe …hata Julius Hotuba zake nyingi zilikuwa zinehaririwa na yule Katibu wake Bibi wa Kiingereza
 
Corona ilikuwa threat kwa watu wenye magonjwa nyemelezi, kwa hiyo alitakiwa kuwaambia watu endapo utajisikia hovyo wafike haraka hospitali kupata matibabu badala ya kuhimiza watu kutumia miti shamba kujitibu aka nyungu, badala ya kusema "hivi vi mafua fua lini viliuaga mtu wagoshaaa hiiii...."
 
Kwa kuzuia kuvaa barakoa tuu yeye Kijazi na watu wengi tuu wamekufa kwa ujuaji wake usio na mantiki

Chanjo imeleta herd immunity kwa nchi zote duniani na kupunguza rate of infection

Muulize Dr Mpango alirudia wapi kwenye ambukizo
 
Reaction ya JPM kwny gonjwa la Corona anastahiki alama zote I.e mia fil mia

Allah alimpa ilhamu ya hali ya juu sana …alipata ujasiri na uthubutu wa hali ya juu sana kuliko wasomi, watabiri na waganga na waganguzi

Kile chuma kilikuwa na flavor yake ya kipekee sana hata Julius angekuwepo kuna mambo angetakiwa ajifunze kwa yule Mwamba

nime miss sana zile hotuba za kutoka moyoni ambazo ndio hasa za Rais

Ma Rais wote walikuwa wanahutubia Hotuba za Ikulu kasoro John peke yake ndo alikuwa anatoa hotuba zake mwenyewe …hata Julius Hotuba zake nyingi zilikuwa zinehaririwa na yule Katibu wake Bibi wa Kiingereza
Kingekuwa Chuma kisingeoza na kingekuwepo hai hadi leo.
 
Kwa kuzuia kuvaa barakoa tuu yeye Kijazi na watu wengi tuu wamekufa kwa ujuaji wake usio na mantiki
Chanjo imeleta herd immunity kwa nchi zote duniani na kupunguza rate of infection
Muulize Dr Mpango alirudia wapi kwenye ambukizo
Unajua herd immunity ni mini ?
 
Nikuulize Swali Unajua Russian Roullette...

Unachukua pistol unaweka risasi moja unazungusha ile cyclinder chamber alafu mnapeana zamu kila mtu kujipiga risasi kichwani...,

Hata ukibahatisha usipokufa lakini gamble kama hio ni hatari ukiendelea namna hiyo uwezekano mkubwa kuna siku utateleza....

Maana yangu ni kwamba kuna mambo hayawezekaniki (total lockdown especially kwa nchi kama Tanzania) LAKINI tahadhari haimaanishi Total Lockdown pekee bali kuwa serious na kuacha mzaha......; In Hindsight kilichofanyika huenda kilikuwa better option, ila sababu hatukujua reaction itakuwa vipi kwahio haikuwa busara ku-gamble na jambo hatari ingawa baada ya kupata more facts ndio inabidi tu-act accordingly ila kabla ya facts kwa mambo ya afya ni vema kuwasikiliza wataalamu na hapa kwenye hili wataalamu ni watu wa afya na sio wanasiasa
 
Back
Top Bottom