Nimepigwa na wanaojinadi wanauza sure bets fixed matches, hakuna kitu kama uhakika kwenye kubeti, ni mbinu ya kula pesa zetu tunaoingia tamaa

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
375
1,064
Nilitembelea website flani wanaposti mikeka imetiki yani sure odds fixed matches, nikalipa dola 30 takribani shilingi elf 80 kuungwa kwenye group, humo ndani ni upuuzi mtupu game wanazoweka ni chache zenye odds za 1.01 yani ukiweka laki ushinde buku lakini ukija kwenye website zao wanadanganya wanaweka mikeka ya mechi zilizokuwa na odds kubwa kwamba imetiki.

Nikaja hapa bongo kuna mdau alikuwa anapost hizi sure bets na mikeka, na kuna watu wanasifia kabisa wameshinda kumbe ni yeye mwenye anajichatisha, nililipa elf 15 ili niungwe group, muhuni sana huyu anapost odds baada ya mechi kuisha ukienda page yake anaweka mikeka imetiki itakuwa ana edit
 
Kama hakuna fixed match kwanini baadhi ya wachezaji wanakutwa na hatia ya upangaji matokeo?
sasa hao ni wachezaji wamo ndani ya team inakuwa siri ya wachache sana haipaswi kuvuja nje maana ikivuja tu ni kesi nzito sana hii,

sio vitu vya kuvujisha kwa watu mtaani waviuze kwa elf 20,

Mfano ile mechi ya Simba kupigwa 5G unakuta ilikuwa ni siri ya Manula na watu watatu tu, sio vitu vya kuvujisha mitandaoni hivi, ukijulikana huna kazi.
 
zinavuja hadi nje ya timu.
 
zinavuja hadi nje ya timu.
Tupe mifano zilivuja lini mitandaoni mfano humu jamiiforums kwenye jukwaa la michezo ?

Hapa bongo penyewe tunajua kuna wachezaji wanacheza hii michezo ya kujifungisha huwezi kuzikuta hizi siri zinazagaa mitandaoni, ikitokea hivyo Fifa wakijua wanaweza kufungia mpaka timu.
 
Back
Top Bottom