SoC02 Nimeamua kuingia mwenyewe shambani - Kilimo cha Parachichi

Stories of Change - 2022 Competition

ILULA HILLS

Member
Mar 19, 2022
31
65
Takribani saa tatu usiku sasa, tunamaliza pika Ugali – Dagaa, tunakula huku maongezi ya hapa na pale yanaendelea na mashujaa wangu hapa, wako mbali kabisa na makazi ya watu, ndio nawajuza mabadiliko ya mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi na wakuu wa mikoa, giza ni nene, baridi ni kali, hivyo wote kwa pamoja tupo tunaota moto.

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.16 PM (1).jpeg

Nachukua simu, kama kawaida kituo cha kwanza ni WhatsApp, kituo cha pili ni hapa jukwaani Jamiiforums. Siku nzima nilikuwa na shughuli za shamba, sikuweza vinjari Jamiiforums, sasa napumzika, napumzikia Jamiiforums, nimeperuzi kila kona na sasa nmedondokea Stories of change. Baada ya kutafakari kwa kina, nikaamua sambaza upendo kwa wana jukwaa. Kuangalia masharti ya mods, mods hawataki tutumie lugha tofauti na kiswahili ila wao wanajina la kingereza, nnaona hayanihusu, muhimu ni kusambaza moyo wa mwamko, vijana waamke.

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.35.20 PM.jpeg

Mwaka mmoja uliopita nilijikuta nimefika Njombe, nilisafiri kwa dhumuni la kwenda jifunza kilimo cha parachichi, maana mengi yanaandikwa kwenye mitandao kuhusu dhahabu ya kijani, kweli sikupoteza muda, nilichojionea kilinivutia sana, na niliondoka Njombe nikiwa na somo kubwa sana, nilidhani ningeandika nada kuhusu niliyojifunza mkoa wa Njombe, ila nmeamua kuandika kuhusu yatokanayo na niliyojifunza mkoa wa Njombe. Kwa kifupi nimetembea mikoa yote ya Tanzania, nadhani 70% ya wilaya zote za Tanzania nimewahi fika kwa majukumu yangu ya zamani ya ufundi minara ya Mawasiliano, katika kutembea kwangu kote, naweza sema Njombe ndio mkoa wenye fursa wazi za uchumi. Kikubwa zaidi ni namna watu wa Njombe walivyofunzwa kuwekeza na sio kufanya biashara. Yani mtu wa Njombe anawaza zaidi kupanda miti atayosubili miaka 13 kuivuna kuliko zao la muda mfupi lenye changamoto nyingi.

Baada ya miezi kazaa ya kujifunza kwa vitendo namimi nikaona muda muafaka wa kupata shamba umefika, kama kawaida, mashamba Njombe bei ipo juu, ukitaka ya bei rahisi utakutana na madali watakuuzia mashamba Lupembe, Mfiriga, Madeke, hadi Mlimba (Moro). Huko kote ni mbali sana na kila kitu pia urefu kutoka usawa wa baharí ni chini ya mita 1000, si salama sana kwa parachichi jamii ya Hass ambayo ndio dhahabu ya kijani yenyewe. Mungu mkubwa mwaka huu mwezi wa pili nikapata shamba Iringa, shamba lipo ndani kidogo, kilomita 35 kutoka barabara ya rami (si mbali sana kwa mpambanaji).

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.00 PM.jpeg

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.17 PM.jpeg

Kwa kifupi kilimo cha parachichi ni kama kilimo kingine chochote cha mazao ya muda mrefu, hapa naongelea mazao kama korosho, kahawa, maembe, machungwa, n.k, kilimo kinachohitaji miaka mitatu ya kujifunga mkanda, baada ya hapo ni kula kuku kwa Mrija, yani unaendelea vuna hata kwa miaka 50, huko Lindi na Mtwara mababu walipanda Korosho miaka ya 70 na 80, hadi leo hii wajukuu wanaendelea uza matunda ya mikorosho hiyo hiyo, sasa hata wakiambiwa imezeeka wapande mingine hawaelewi. Parachichi nayo ni ya hivyo hivyo, utavuna kila mwaka, kwa umri wetu huu, tutawaachia watoto nao wale mema ya baba zao, pengine hata wajukuu watakuja nufaika na kile kinachofanyika sasa.
WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.11 PM.jpeg

Parachichi yenye umri wa miaka nane na kuendelea inayo uwezo wa kukuzalishia kilo 150 za matunda na kuendelea, wapo watunzaji wazuli wanavuna hadi kilo 250 – 300 kwa mti mmoja, leo hii ukivuna kilo 150, ukaziuza kwa bei ya shambani ya Tsh 1,500/= kwa kilo, utapata Tsh 225,000/=. Kama umepanda miti 80 kwenye eka moja, utapata zaidi ya Mil 16 kwenye eka moja ya parachichi miaka 8 baada ya kupanda, inamaana mwaka wa 3 baada ya kupanda unaweza anza vuna hata mil Tsh milioni 2, mwaka wa nne itaongezeka, na itaenda inaongezeka hivyo hivyo hadi miti yako itakavyotambaa na matawi kuanza kukutana.

Nikiwa Njombe nilijifunza mambo mengi sana kwenye mnyoro wa thamani wa zao la parachichi, kuanzia namna unavyotakiwa chagua shamba la parachichi, miche ya parachichi, utunzaji wa shamba la parachichi, kwanini watu wanatelekeza mashamba ya parachichi kwa kukosa huduma, changamoto za wanunuzi wa parachichi, n.k (kama una lolote unalotaka jifunza unaweza uliza swali).

Moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wanunuzi wa parachichi ni namna wakulima wadogo wadogo walivyo mbalimbali, yani mnunuzi wa parachichi anatembea umbali mrefu kutoka kwa mkulima mmoja hadi mwingine, hii inapelekea pia wakulima kutokuwa na nguvu ya pamoja sokoni.

NI NINI CHA TOFAUTI NAFANYA?

Kwanza kabisa nimeamua kuondokana na gharama kubwa za kununua miche, hivyo tunaenda panda parachichi ilikwisha ota tu kwenye kitalu, hivyo zoezi la kupandikiza machipukizi (budding) litafanyikia shambani. Kuna faida kadhaa kwenye kufanya hivi, moja ni kuokoa gharama, mbili ni kuweza pandikiza machipukizi kwa zaidi ya tawi moja tofauti na miche ya kununua inapandokwizwa chipukizi tawi moja tu, tatu mche unakuwa kwa haraka na kusambaa kwa haraka sababu mizizi inapata nafasi ya kujitanua tofauiti na ikiwa kwenye kiliba.

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.10 PM.jpeg

Pili, tunaenda lima mazao ya muda mfupi kama mahindi, maharage, alizeti,n.k. Mazao haya ya muda mfupi kwa kiasi kikubwa yatatusaidia kuweza endesha shughuli zote za shamba. Uzuri ni kwamba sehemu tulipopata shamba kuna rutuba ya kutosha hivyo kilimo chochote cha zao la muda mfupi hakihitaji kulima kwa mbolea. Pia kuna vyanzo vingi vya maji visivyokauka mwaka mzima.

Tatu, eneo tunalopanda parachichi, tayari nimeshawishi watu 11 wengine kununua mashamba watayopanda parachichi pia, na zoezi hilo litaendelea hadi tutakavyokuwa majirani zaidi ya 70 tunaolima parachichi kwenye eneo lenye zaidi ya eka 1700, kila mmoja na shamba lake, mwisho wa siku tutakuwa na nguvu kubwa sokoni, yani mpango ni kuja kuweka kiwanda cha kuchakata parachichi hapa hapa shambani.

WhatsApp Image 2022-07-31 at 9.16.04 PM.jpeg

Sasa hapa sisi ndio tumeianza safari, 2022 ndio mwaka wetu wa kwanza, tukutane 2025 wakati wa mavuno.
 
ILULA HILLS nimekupa kura yangu, andiko lako lina tumaini kwa waliokosa tumaini, kwamba inawapasa kujaribu fursa kwingine...

Kama hutojali, bei ya mashamba huko ni kiasi gani?

Unaweza ukanijibia PM
 
Nianze kwa kukupongeza kwa kufika hatua hiyo.
Pamoja na pongezi ninayo machache ya kukushauli hasa kuhusu mbegu.
UTANGULIZI.

Watu wengi wamechukia kilimo kwa sababu yakujikuta wanahangukia kwenye mbegu mbaya (zisizo na ubora)

Hakuna shaka kua mbegu Bora ni gharama kubwa, hata hivyo Haina maana yeyote atakae kuitumia lasirimali fedha + muda na baada ya 3 ukavuna mazao yasio kizi ubora.

Umeeleza kua umefika Njombe bila shaka utakua ulisikia sehemu inaitwa ,,, Madeke"

Huko Kuna wakulima wananasi , mojawapo ni philimoni Luhanjo , katibu mkuu kiongozi mstafuu.
Wakulima hao wamekutwa na janga lambegu, zisizo kizi viwango vya kimataifa.

Waziri mwenye zamana ya kilimo Huseni Bashe , wakati anahitimisha hotuba yake Bungeni , alilisema hatutaki kufanya makosa kama yalio fanyika kwenye nanasi

Na mayembe.ambayo hayaitajiki kwenye viwanda vya ndani Wala vya nje.
Akaahahidi kusimamia ubora wa mbegu nakugawa Miche kwa wakulima kwa mfumo wa ruzuku.
Mche 1 waparachichi uliyo Bora= 5000Tsh

Hadi Sasa hatujafahamu ruzuku itawekwa Tsh ngapi?

Baada ya utangulizi huu naomba nikushauli ya fuatayo.
1. Nunua Miche Bora michache yakuanzia walau 300
hii itakusaidia.

a: ikitokea Miche Yako ulio andaa wewe ikipatwa na (hitirafu) kama, kunyauka , au kutoa matunda yasio kizi ubora.

b:huko mbeleni itakua chanzo Cha vikonyo vya kuzalisha mbegu Bora.

2 wakati unaendelea zowezi lakuanda Miche zingatia ya fuatayo
a: kutibu udongo
b:chagua vipeke vyenye afya kisiwe chini
mg4500
c:hakikisha Kila kipeke umekichunguza , kwa ku kikata pembeni na kuangalia rangi yake ya ndani , kikiwa na doa la aina yeyote , hiyo ni Darili ya ugonjwa usiwatike.

Zingatia hayo , kwa Mfindi ni taasisi moja inayo aminika kwa Miche Bora karibu kutafuta ushauli pale.

TAHA Wana mtaalaam Njombe nae waweza kumtembelea kwa ushaul .

Mwisho msinihukum kwa muandiko nihukum kwa maudhuwi .
 
Hakuna kilimo rahisi, lazima ujipange kwa "few failures", Kuna jamaa alianzisha uzi wa kilimo cha mahindi kwa mbwembwe, sasa hivi akiuona anasikia kichefuchefu.

Baadhi ya few failures ni pamoja na upatikanaji wa mbolea mboji ya kutosha shamba lako, kufa ovyo ovyo kwa Miche michanga, wanunuzi kuchagua matunda wanayoyataka wao, mengine kukuachia usijue cha kufanya, kuuziwa Miche ya uongo (kutapeliwa), gharama za palizi hadi Miche kufikisha miaka mitatu maeneo yenye mvua nyingi si mchezo
 
Back
Top Bottom