Ni vipengele gani vya kimkataba vinapaswa kuwekwa unapompa mtu asimamie biashara yako Ili upate faida?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,168
50,042
Habari za hapa waungwana naombeni niongezeeni maarifa ya uendeshaji mzuri wa kibiashara case study ni hizi biashara zangu.

Nina jamaangu muaminifu sana kwenye maisha na ni mzawa wa hapa nilipo yeye ni fundi viatu sasa ana kijiwe chake sehemu nikaona ni center yaani tukiweka viatu vya mitumba tutapata hela maana sio biashara ya mtu kukukopa ile lazima aje amejipanga uzuri haiozi. Ingawa na yeye akashauri tujiongeze tubane na ganja tunanunua kisado tunapiga hela mimi hio naogopa tume ya kudhibiti Madawa hivyo bado ni ya mashaka.

Sasa mimi nimepata mtaji sehemu mzuri tu wa kutosha kununua Belo Zima la viatu ila pamoja na mpango huo bado nakuwa na wasiwasi na watu kuwaamini 100% na biashara peke yako haiwezekani najishtukia kupigwa hela si unajua Tena ukiwa mwizi unahisi kuibiwa na wewe.

Lengo langu la thread ni kujua Je niende naye vipi kimaandishi mimi nikawaza labda niwe Nampa viatu kama 20 Hivi vingine naviweka ndani je ni sahihi hivo na tuandikishane vitu gani je tuweke hela kwenye account ya namna gani ili mwisho wa mwezi tugawane faida na je yeye apate asilimia ngapi ya Hela naombeni mniongezee maujanja ya kuishi na msimamizi wa mradi wako ili iwe mnafaidika wote.

Mnaofanya biashara na watu wenu mnaojuana nao mnafanya kitu gani ili kuweka mambo vizuri kusiwe na mipasuko ya kifedha wala mianya inayoathiri biashara Kwa pande zote za Tajiri na mfanyakazi wake.
 
Back
Top Bottom