Ni ushamba na kutojitambua kuendekeza matamanio ya mwili

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
2,015
3,925
- Unamsikia mtu anasema "Yaani mimi ikipita siku sijapata walau savanna moja mwili unakuwa mzito HADI nipate japo kidogo moja aisee ndo nakuwa sawa".

- Au mwingine unamsikia akisema "Yaani mimi ipite siku sijakunywa chai au japo kikombe kimoja cha kahawa naona kama siku yangu BADO haijakamilika. Lazima nipate japo kakikombe kamoja mwili ukae sawa".

- Au SIWEZI kupitisha siku bila kunywa soda fulani au kinywaji fulani.

Kuna watu hayo ndio maisha yao ya kawaida ya kila siku. Yaani wamejitungia kanuni mimi naita ni za kishamba kama sio kijinga kabisa za kutegemeza maisha yao kwenye vitu, ni dalili ya mtu aliyeshindwa kuutawala mwili wake na badala yake karuhusu mwili kumtawala.

Kibaya zaidi vitu vyenyewe ivyo havikuongezei kitu cha maana mwilini zaidi ya kuuharibu na kuuchoka tu mwili kwa vitu visivyo na maana.
 
Atasikika Mlaibu mmoja akisema
"Tusipangiane maisha pesa ni zangu"

Na mimi Naongezea
"Ulaibu wa kitu chochote ni Utumwa"

In Advance "Bichwa kama furushi la ushirombo".
 
Sasa mtu kuwa na matamanio yake ambayo hayavunji sheria wala kukuchubua ngozi yako nayo ni nongwa kwako?Ina maana hata wakiwaza au kutamani kuamka wakiwa wazima kesho napo watakuwa washamba?Waache watu waishi mawazo yao!
 
Yaani mimi isipite siku sijaingia Jamiiforums sina raha kabisa mwenzenu

Siwezi kabisa..

Ila ni kanuni za kila mmoja alizojiwekea ..

Ni sawa mtu anayeamka kila siku swalaha kwenda kuswali

Huwezi ukamwambia eti ni Ushamba na kutokujitambua

Inapendeza kuishi kwa ratiba na utaratibu

Usitupangie maisha
 
Ngoja nitafakari kwanza na mimi nije kutoa mchango wangu ila nafikiri tunatakiwa kuzitawala hisia zetu na sio hisia kututawala
 
Mental illness is so real,
Acha kupangia watu maisha, mxxxxiiiieeeew.
 
Back
Top Bottom