Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
602
1,264
Habari za muda huu wana JF,

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya.

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji cha Baranga kata ya Sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndio kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu, jua kali ndio kwao, vurugu Sasa ndio chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa na mgogoro wa mpaka wa shamba kati ya ukoo na ukoo huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu nini?
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

images.jpeg
 
Kijiji cha Chimendeli, wilaya ya Bahi Mkoa WA Dodoma.

Sijui kule watu Wanaishi vipi. Unaweza Kudhani uko Somalia au Afghanistan.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Hahahaaaa kweli mkuu naunga mkono hoja hata ukiwa kwenye Basi njiani unasafiri utashuhudia vichaka vya miiba vilivyokauka hakuna miti mikubwa ya kivuli.
 
Back
Top Bottom