Ni muda muafaka sasa Tanzania kurejesha Wizara ya TEHAMA

w0rM

Member
May 3, 2011
73
177
Rais Samia alipoingia madarakani alikuta mtangulizi wake akiwa ameanzisha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ikiongozwa na Dkt.Faustine Ndugulile. Wizara hii ingawa ilikuwa katika hatua za awali, ilikuwa imeanza kujenga ukaribu na wadau na ndipo mchakato wa kuanzisha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ulianza.

Bahati mbaya, katika panga pangua, Wizara hii iliunganishwa upya baada ya Rais Samia kufumua Baraza lake na kuunganishwa na Wizara ya Habari.

Kuna mkanganyiko mkubwa pale Waziri wa Habari anaposhughulikia pia Mawasiliano na Tehama. Wadau tumekuwa tukiona mengi na pamoja na kushauri, aidha tunapuuzwa au kuchukuliwa poa kitu kinachokatisha tamaa.

Mh. Rais Samia, katika kupanga na kupangua safu ya Uongozi, usiishie tu kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi, ni muda sahihi sasa Tanzania tukatenganisha Mawasiliano ta Teknolojia ya Habari kutoka Wizara ya Habari.

Kwanini natoa ombi hili; Kwanza kabisa kila uchao TEHAMA inakuwa na inahitaji uangalizi wa kipekee kwani inaenda kulikomboa Taifa letu. Lakini pia anahitajika Waziri anayeijua TEHAMA kuisimamia kwa uzuri akishirikiana na wadau.

Ukiangalia mataifa jirani (mfano Kenya na Rwanda); yamepiga hatua kubwa katika masuala ya Teknolojia na TEHAMA baada ya kuwa na Wizara zinazosimamia masuala hayo pekee.

Mheshimiwa Rais kumbuka TEHAMA sasa inaenda mbali, Wizara hiyo inaweza kusimamia hadi masuala ya Uchumi wa Kidigitali ambapo sasa Dunia inaelekea huko lakini pia uikua vipaji vya Watanzania katika dijitali.

Katibu Mkuu wake itapendeza akiwa Dkt. Jim Yonazi.
 
Back
Top Bottom