Ni kweli kwamba mtu anayetumia vyema ARV kipimo cha kujipima cha damu huwa hakioneshi ni muathirika?

Aloo yani umemtoa mtu telegram huko, mkaenda lodge kuchapana.
Mkachukua tuvipimo twenu mkajipima mkajikuta mko -ve, basi wale mnachapana kavu...

Watu mnajiamini sana aisee.
Mkuu kwenye kulalana mode, wengi hupoteza fahamu asikwambie mtu.

Mtu anaweza akabeba condom kabisa, lakini akifika kwenye tukio havai, ama akivaa tendo likianza anaomba avue!

Na wengine kabla ya tendo huanza kunegotiate juu bei ya 'kwa ndom' na 'kavu kavu' na tozo la kavu kavu ni gharama ya kujenga darasa.

Kinachofanya hasa wanaume wataharuki zaidi ni huko kutozwa hongo kubwa za kufuru.

Sasa akijiuliza alivyomnunulia malaya gari, amemjengea nyumba na mambo mengine makubwa amemfanyia, kisha aje afanye kwa maigizo akili zinakataa isee, akifika hapo lazima ajitoe mhanga kwa kujivisha mabomu mwili mzima.

Mtu yeyote akitanguliza akili zake mbele, hawezi kuukaribia mzunguko wa matendo hayo, maana roho yake itamsuta na kujiona anajisaliti nafsi yake, anasaliti mke na anasaliti dini yake.

Akifikia kuwaza hivyo keshajitambua huyo, basi kitu chake hulegea kama kamba na kunywea nywiiii kisha hupiga ishara ya msalaba ama kutamka kabisa kwa maneno 'alahmdulilah' na kisha kusepa.
 
Sio kweli mkuu, kile kipimo cha ngoma kinapima antibodies (ni kemikali mwili inayotoa ili kujilinda na virusi). Ukishapata virusi hio antibody itakuwepo kwenye mwili wako siku zote hadi unakufa.

Mtu akitumia ARV vizuri kinachopungua ni Viral load ( yaani wale virusi ndio wanapungua) sasa kuna muda wanapungua hadi wanafikia kiwango cha kuwa undetected kwa kipimo cha PCR ( sio hicho unachotumia wewe) lakini ukipima kwa kipimo tunachotumia hiki cha rapid test utakuta inasoma positive kama kawaida, kwa sababu hata kama viral road ni ndogo sana kiasi cha kuwa undetected kwa kipimo cha PCR, mwili bado unaendelea kutoa antibody( ile kinga ya kupambana na hivyo virusi vichache vilivyobaki) hivyo kipimo cha rapid test (tunachotumia mara kwa mara kujipima) kitakuwa positive tu.

Kwahio mkuu ukipima mtu ukamkuta negative maana yake ni kwamba hana ngoma au ameambukizwa juzi kati tu na bado mwili haujatengeneza hizo antibody.

Ushauri wangu kama mtu humuamini mmekutana kwa mara ya kwanza ukampima ukakuta yuko negative, tumia Condom then baada ya mwezi mpime tena akiendelea kuwa negative ndio ule kavu .
Kwa mzunguko huo haujashauri kitu.

Huyo malaya anayempima pima, yaweza kufika kipindi cha matarajio ili amle kavu kavu, tayari akawa ameambukizwa kwingine, maambukizi mapya yasiyoonekana kwenye vipimo vyake hivyo, akafakamia kavu na akanasa vile vile.

Cha kujiuliza, kwa nini kwenye kulalana watu wanakuwa kama mbwa kwa chatu, kujipeleka kwenye hatari anayoijua ili akaliwe bila kupata mbadala wa kukataa?
 
Kwaiyo icho kitu kinachoitwa kitaalamu unditect hakiwezi kutokea kabisa Kwa mtumiaji mzuri wa arv.
Kitaalam, vipimo vya HIV (virus vya ukimwi) ni vya aina tatu.
1. Antibody test (vinapima vinasaba protein (glycoprotein) inayozalishwa na mwili ili kupambana na hamful substance iliyoingia mwilini)
2. Antibody/Antigen test (vinapima vinasabq glycoprotein (antibody) pamoja na hamful substance inayozalishwa na mvamizi (antigen).
3. Nucleic acid test (hii inapima DNA na RNA sequences za kirusi).

Vipimo vinafaa nini?
Hapa kwetu vipimo maarufu ni namba 1 na 2. Vipimo hivi vikigundua uwepo wa antibody (vinasaba vinavyozalishwa na mwili kupambana VVU), matokeo haya hayabadiliki maana vvu vimo mwilini. Antibody/antigen inapima uwepo wa hivyo vinasaba vya kinga mwili pia uwepo hamful substance...test ikiwa positive haibadiliki maana mgeni
ameingia na hatoki.

Hiyo undetected unayosema, inakinzana na sayansi inavyosema.
 
Nimeona nije nipate michango ya wanajamvi kutokana na kwamba jukwaa hili Lina wasomi na madaktari wengi.

Kwasasa vijana wengi tumeangukia kwenye wimbi la kujipima na Kula tunda kavu, ata huko Kwa Malaya utaratibu ni huo wao wanakuwa na vipimo vyao mnapima kisha mnakulana.

Sasa kuna mtu mmoja ameniambia kwamba watumiaji wazuri wa ARV inafikia stage ambayo kipimo hakioneshi ni MUATHIRIKA sasa nimejiuliza maswali sanà kwamba kama ndivyo maana yake watu wataambukizwa Kwa kuamini kipimo.

Kama hali hiyo ni ya kweli bhasi tutakuwa na wagonjwa wengi siku zijazo Kwa maana mtu ukimpima Leo unapomla kavu unakuwa huna wasiwasi hivyo michubuko hutojali na utatumia ujuzi wako kumuonesha kuwa unayajua mapenzi kumbe mwenzio dawa zimemkubali.

Naomba kama kuna mtu anao ufahamu kubusu hili atujuze maana naisi tutaisha Kwa kuamini kipimo, hapa nazingumzia siku umempima ndio siku umemla sio mahusiano ya muda hapana, Kwa lagha nyingine ni eat and run.

Asanteni.
Haiwezi kuwa hivo kiongozi,
Kile kipimo kina detect uwepo wa virus kwenye damu.
Kwahyo hata kam anatumia vizur dawa na Bado virusi vipo lazima vionyeshe.

Ninachojua kwa watumiaji wazuri wa dawa Huwa kuwaambukiza wengine ni ngum endapo tendo litafanywa kwa tahadhari.
 
Kama kipimo hakionyeshi inaitwa UNDETECTABLE.

Mtu akiwa katika hali hiyo hawezi kuambukiza.
Msijidanganye ipo hivi kinacho fanyika kwa mtu anaye tumia ARV ni kufubaza virus na sio kuviua, kwa misingi hiyo vinapunguzwa nguvu ya replication ndan ya mwili wake kwakuwa dam yake tayari ina pambana navyo ndio maana akiacha tuu kutumia dawa vina rud tena kwa sababu bado vipo ila vime zirai kwa kukosa support, sasa kwa wewe usiye tumia ARV endapo ukashirik na mwenye maambukizi na damu zenu zikichangamana basi virus wataamka tena ndani ya mwili wako na kuanza kuzaliana tena kwakuwa kwako hakuna chochote kinacho pambana navyo
Na vile vipimo vyenyewe vinapima Antigen tu na kwa kuwa hakuna replication yeyote inayo endelea na hakuna shambulio lolote basi ni rahis tu CD4 kuongezeka na kipimo kushindwa ku react lakini haimaanishi kuwa hana virus ndani ya mwili wake
 
Haiwezi kuwa hivo kiongozi,
Kile kipimo kina detect uwepo wa virus kwenye damu.
Kwahyo hata kam anatumia vizur dawa na Bado virusi vipo lazima vionyeshe.

Ninachojua kwa watumiaji wazuri wa dawa Huwa kuwaambukiza wengine ni ngum endapo tendo litafanywa kwa tahadhari.
Ni kweli, hatari ya maambukizi inapungua SANA.

Ushauri ni kuwa: mdharau mwiba...
 
Kwa mzunguko huo haujashauri kitu.

Huyo malaya anayempima pima, yaweza kufika kipindi cha matarajio ili amle kavu kavu, tayari akawa ameambukizwa kwingine, maambukizi mapya yasiyoonekana kwenye vipimo vyake hivyo, akafakamia kavu na akanasa vile vile.

Cha kujiuliza, kwa nini kwenye kulalana watu wanakuwa kama mbwa kwa chatu, kujipeleka kwenye hatari anayoijua ili akaliwe bila kupata mbadala wa kukataa?
Hapo nimemucha ajiongeze kwamba, kwa kila mwanamke atakaekutana anae whether kampima na yuko negative atumie kondom tu.
 
Nimeona nije nipate michango ya wanajamvi kutokana na kwamba jukwaa hili Lina wasomi na madaktari wengi.

Kwasasa vijana wengi tumeangukia kwenye wimbi la kujipima na Kula tunda kavu, ata huko Kwa Malaya utaratibu ni huo wao wanakuwa na vipimo vyao mnapima kisha mnakulana.

Sasa kuna mtu mmoja ameniambia kwamba watumiaji wazuri wa ARV inafikia stage ambayo kipimo hakioneshi ni MUATHIRIKA sasa nimejiuliza maswali sanà kwamba kama ndivyo maana yake watu wataambukizwa Kwa kuamini kipimo.

Kama hali hiyo ni ya kweli bhasi tutakuwa na wagonjwa wengi siku zijazo Kwa maana mtu ukimpima Leo unapomla kavu unakuwa huna wasiwasi hivyo michubuko hutojali na utatumia ujuzi wako kumuonesha kuwa unayajua mapenzi kumbe mwenzio dawa zimemkubali.

Naomba kama kuna mtu anao ufahamu kubusu hili atujuze maana naisi tutaisha Kwa kuamini kipimo, hapa nazingumzia siku umempima ndio siku umemla sio mahusiano ya muda hapana, Kwa lagha nyingine ni eat and run.

Asanteni.
Kama anatumia dawa vizuri hadi kipimo hakionyeshi basi hawezi kukuambukiza
Mbaya ni yule ambae yupo kwenye window period huyo ukigusa tu imo
 
pole sana ila nikwambie tu hata kama kipimo hakitaonyesha basi mdudu bado unae mwilini mzee hata ufanyeje ww jifariji usubiri siku yako ya kufa..... ova

hukutumwa ushobokee k chafu usizozijua
Kuugua ukimwi sio kufa, unaweza kufa wewe unaejiona mzima ukamuacha muathilika.
Hivi kuna magonjwa yanatisha kama Kansa na Figo wewe
 
Hicho cha kujipima mwenyewe hata utumie dawa vizuri namna gani kitasoma mistari miwili kama kawaida.

Kuna kipimo kingine kabisa maabara cha kubaini wingi wa virus (viral load) ndiyo huonesha hayo mambo ya detectability.
 
Mkuu kwenye kulalana mode, wengi hupoteza fahamu asikwambie mtu.

Mtu anaweza akabeba condom kabisa, lakini akifika kwenye tukio havai, ama akivaa tendo likianza anaomba avue!

Na wengine kabla ya tendo huanza kunegotiate juu bei ya 'kwa ndom' na 'kavu kavu' na tozo la kavu kavu ni gharama ya kujenga darasa.

Kinachofanya hasa wanaume wataharuki zaidi ni huko kutozwa hongo kubwa za kufuru.

Sasa akijiuliza alivyomnunulia malaya gari, amemjengea nyumba na mambo mengine makubwa amemfanyia, kisha aje afanye kwa maigizo akili zinakataa isee, akifika hapo lazima ajitoe mhanga kwa kujivisha mabomu mwili mzima.

Mtu yeyote akitanguliza akili zake mbele, hawezi kuukaribia mzunguko wa matendo hayo, maana roho yake itamsuta na kujiona anajisaliti nafsi yake, anasaliti mke na anasaliti dini yake.

Akifikia kuwaza hivyo keshajitambua huyo, basi kitu chake hulegea kama kamba na kunywea nywiiii kisha hupiga ishara ya msalaba ama kutamka kabisa kwa maneno 'alahmdulilah' na kisha kusepa.
Wewe bila shaka ni mmoja wao, pole sana.

Mkuu kinachotakiwa ni AKILI. Yaani akili pekee.

Huyo wa telegram umemtoa kwa gharama gani? Kuna gharama kubwa kuzidi uhai wako??
 
Wewe bila shaka ni mmoja wao, pole sana.

Mkuu kinachotakiwa ni AKILI. Yaani akili pekee.

Huyo wa telegram umemtoa kwa gharama gani? Kuna gharama kubwa kuzidi uhai wako??
Mkuu umeninukuu tofauti. Huo ni mzaha tu.

Ukimwi umeanza tunauona tena nikiwa mtu mzima zaidi ya miaka 40 sasa.

Ningekuwa sijichungi, leo hii ningelibakia kuwa ni historia tuu, maana ujana wetu wote tumeumalizia ndani ya kipindi cha madhara haya ya Ukimwi lakini ad nazeeka nipo mzima wa afya bila ya maambukizi.

Kwa kauli nyingine naweza kusema Mungu ameniepusha.
 
Back
Top Bottom