Ni kwanini tasnia ya bongo movies haeindelei mpaka leo ukilinganisha na bongo fleva?

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,420
14,632
Hali inazidi kutisha sana katika upande wa bongo movies, kwani hiyo tasnia haiendelei na wala hailipi. Ukija kutafta watu maarufu na wenye hela utakuta ni wa bongo fleva, je huko bongo movies shida ni nini?

The late Kanumba alijaribu kuipambania sana hiyo tasnia baadaye JB naye akaipambania lakini ni kama hailipi na hawana creativity kabisa.

Una ushauri gani au maoni gani ya namna ya kuisogeza mbele hi tasnia yetu ya bongo movies!
 
Ukifuatilia wasanii wengi wa bongo movies hawana hela kabisaaa na wanaishi kwa majina tu na wengine wanaishi kwa kudanga. Take example king majuto namna alivokuwa icon wa kuchekesha lakini je alikuwa na hela? Hi tasnia ipo nyuma sana haswa kwenye uwekezaji na teknolojia.
 
Wawekeze kwenye teknolojia, watu siku hizi wanatumia graphics za maana kutengenezea picha kama yale madude ya kijani sijui yanaitwaje.

Halafu waache kurekodia kamera za kiduwanzi, wakaazime hata zinazotumiwa na kina Kiba na Mondi.

Waigizaji na watengeneza muvi waingie darasani kusoma ili walete vitu vya kijanja, vyenye ufikiri mkubwa na sio kila siku mapenzi na komedi. Watupe radha tofauti kama ujasusi, utawala na siasa, wizi kama money heist n.k

Natambua hali zetu kipesa sio nzuri sana lakini muvi kali uwekezaji wa kifedha haukwepeki. Hatutaki kuona mnavunja glasi na sahani, muharibu hata harrier tako la nyani mnalitia kiberiti😅.

Watambue ushirikiano na wengine ni muhimu, wajitahidi kujimix na wanaijeria au waghana waliofanikiwa labda watatuambukiza harufu ya mafanikio katika tasnia ya bongo muvi.
 
Tasnia ilivamiwa, na kugeuzwa chaka la uhuni si burudani, mnamsifu kanumba ila ndie aliyeiharibu hii tasnia kwa kuokota okota mabinti wenye muonekano ambao hawana ile spirit ya sanaa so walipopata julikana na wakajua kuna mambo mengine nje ya sanaa so sanaa imebaki kama kivuli tu ila umalaya ndio mkubwa
 
Asante mkuu
 
Kwa hilo sidhani mbona uwoya alikuwa na kipaji tu?
 
Cinema ni tofauti na muziki mkuu, Filamu zinataka uwekezaji mkubwa pamoja na taaluma kubwa kwa watu ambao wanakua behind scene. Hapo Bongo ndipo tunapokwama.
 
Back
Top Bottom