Ni ipi adhabu ya kutukana?

Matusi,kutukana limekuwa jambo la kawaida mitaani na mitandaoni.Ni ipi adhabu ya kutukana bila kujali wadhifa wa anayetukanwa?
Ni kipi mtu anatakiwa kufanya endapo atatukanwa?
Kutukana ni kosa kisheria kwa mtu yeyote yule !
Haijalishi ni mtu mwenye wadhifa au mtu wa kawaida mtaani !
Ukitukana mtu kukapatikana ushahidi mhusika ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria !!

Ila ni vizuri tukajifunza kwamba hakuna mwenye haki ya kutukana au kutengenezea wenzie kashfa !!

Kama wewe huwa unaumizwa unapotukanwa au unapotukaniwa mtu wako basi ni vyema na wewe pia usiwe unatukana tukana watu au kuwatengenezea kashfa mbaya watu ambao unawachukia kwa sababu zako unazozijua mwenyewe !
Kumtukana mtu yeyote yule bila kujali ana wadhifa au ni hohe hahe mtaani ni makosa ni lazima ushahidi ukiwepo utaadhibiwa !!
Hakuna mwenye hati miliki ya kutukana na kukashifu wengine !!
 
Matusi yamegeuka viunganishi vya maneno kwa vijana wengi, hii ni tabia ya hovyo sana. Kuna wale wazazi wanaotukana mbele ya watoto na hawaoni kama wamekosea sijui wanawafundisha nini watoto.
 
Back
Top Bottom