Kufuatia mapitio ya orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (National Essential Medicine List -NEMLIT) yaliyofanywa na Wizara ya Afya Aprili 30, 2024 kwa kujumuisha muunganiko,muundo na nguvu kwa dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye Mwongozo wa Taifa wa Matibabu lakini hazikuwemo kwenye NEMLIT na hatimaye kusaini nyongeza (addendum), Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa umejumuisha dawa hizo katika Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.
Hatua hii inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini. Kutokana na maboresho hayo, fuko wa Taifa Bima ya Afya unawahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa nchi nzima.
Endapo kutakuwa na changamoto za kiutekelezaji Mfuko unashauri vituo vya kutoa huduma viasiliane na ofisi za Mfuko kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa wateja wao.
Kwa nyongeza, iwapo mwanachama atakutana na changamoto yoyote katika upatikanaji wa huduma tafadhali asisite kuwasiliana na Mfuko kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga simu bila malipo namba 199.
Pia soma: 'Dawa 178 na Vifaa Tiba 15 vilivyoondolewa kwenye Kitita kipya cha NHIF'