SI KWELI NHIF yarejesha utaratibu wa kusajili watoto kupitia Mpango wa Toto Afya Kadi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na taarifa inayosambaa mtandaoni ikionesha kuwa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) umerejesha mpango wa kusajili watoto kupitia kifurushi cha Toto Afya Kadi.

nhif-packages.jpg
Taarifa hii ina ukweli kiasi gani maana naona kuna mvutano mkubwa, baadhi wanadai ni kweli na wengine wanasema si kweli.
 
Tunachokijua
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulianzishwa ili kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa watumishi wa Serikali, Umma, Binafsi, Wanafunzi na makundi mbalimbali ya watu ili kupata huduma za matibabu kupitia vituo vya Serikali, Madhehebu ya dini, Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa na Mfuko.

Machi 13, 2023, habari zilianza kusambaa mtandaoni kuwa Mfuko huo ulikuwa umeondoa kifurushi maarufu cha Toto Afya Kadi ambacho kilikuwa kinapatikana kwa gharama ya kiasi cha Tsh. 50,400/=

Habari hizi zilichapishwa pia JamiiForums kupitia andiko lenye kichwa cha habari “NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi"

Taarifa hii ilifafanuliwa na mfuko huo kwa kudai kuwa walikuwa hawajaufuta mpango huo, bali walikuwa wanaufanyia marekebisho.

Sehemu ya taarifa hiyo ilisema;

“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutangazia Umma kuwa, unafanya maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya "TOTO AFYA KADI". Hivyo, katika kipindi hiki cha maboresho, wazazi wanashauriwa kusajili watoto wao kama wategemezi kupitia Vifurushi vya Bima ya Afya au kupitia shule wanazosoma.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi fika katika ofisi za Mfuko zilizo karibu au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kupitia namba ya bila malipo 199.”


Malalamiko mengi yaliibuka baada ya kutolewa kwa taarifa hii iliyopokelewa kwa masikitiko makubwa na watu wengi.

Kufuatia hali hii, JamiiForums iliandaa mjadala wa wazi kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) ili wadau waweze kutoa maoni yao juu ya suala husika. Aidha, uzi wenye kichwa cha habari Maoni ya wadau wa JamiiForums juu ya kusitishwa kwa Bima ya TOTO AFYA KADI uliandaliwa kwa ajili ya mjadala huo.

Tangu wakati huo hadi sasa, maoni mengi yamekuwa yanataka mpango huo urudishwe ili kupunguza gharama kwa idadi kubwa ya watoto wasio na uwezo wa kupata matibabu kwa utaratibu wa kawaida au kupitia bima za familia ambazo gharama yake ni kubwa.

Madai ya kurejeshwa kwa mpango wa Toto Afya Kadi.
Agosti 4, 2023, taarifa za kurejeshwa kwa mpango wa Toto Afya Kadi zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Barua yenye taarifa hiyo ilifafanua;

“Uongozi wa mfuko wa bima ya afya (NHI) Chini ya Wizara ya Afya una watangazia wananchi kurejeshwa kwa utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto walio kuwa wana sajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya Toto Afya Kadi.

Hivyo usajili utafanyika chi nzima kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) kwa gharama ya 64,500/= kwa moto mmoja

Mtoto ana hitajika kuwa na cheti cha kuzaliwa au kadi ya kliniki yenye taarifa zote za wazazi wake.

Usajili utafanywa kwa mfumo wa kutuma taarifa sahihi kupitia namba ya WhatsApp: +255 758 327 374

Mwisho wa usajili ni tar: 08 Septemba, 2023”


Taarifa hii ilikanushwa Agosti 7, 2023 kupitia barua rasmi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

img_8239-jpeg.2715598

Barua ya NHIF ikikanusha uvumi wa kurejeshwa kwa Toto Afya Kadi
Pamoja na mambo mengine, taarifa hiyo iliwataka wananchi kupuuza madai hayo na kwamba Mfuko unaendelea kusajili watoto kwa utaratibu wa kujiunga na familia zao au kupitia shule wanazosoma na usajili unafanyika kwenye ofisi za NHIF zilizo mikoa vote. Aidha, kwa wale wanaojisajili kupitia shule, shule husika itawasiliana na NHIF kukamilisha usajili huo.

img_8255-jpeg.2715597

Barua iliyokanushwa na NHIF kuwa sio ya kweli
Pia, mfuko huo uliwakumbusha wananchi kwamba mawasiliano baina yao hufanywa kwa kutumia njia sahihi ambazo ni namba ya huduma kwa wateja 199 na taarifa za Mfuko hutolewa kwenye tovuti ya Mfuko ambayo ni www.nhif.or.tz na akaunti za mitandao ya kijamii ya X, Instagram na Facebook yenye jina rasmi la NHIFTZ.

Attachments

  • IMG_8238.jpeg
    IMG_8238.jpeg
    41.3 KB · Views: 3
Labda Kuna harufu ya utapeli kwa Nini wapweke mwisho wakati Kila siku watoto wanazaliwa na Kila siku watu wanafunga miaka 18, itakuwa ni wapigaji hao
 
Labda Kuna harufu ya utapeli kwa Nini wapweke mwisho wakati Kila siku watoto wanazaliwa na Kila siku watu wanafunga miaka 18, itakuwa ni wapigaji hao
Kwanz Definition ya mtoto wizara ya Afya ni tofauti na ile ya serkali mtoto ki matibabu anaishia miaka 14 au 16 na sio 18
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom