Nguvu Moja ndio imeiua Azam leo wala si mbinu za Mgunda

Mwishokambi

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
312
1,190
Simba inakabiliwa na tatizo la umoja, tukiwa wamoja hakuna wa kuisumbua Simba, kuna watu wako Simba ndio wanaoamua kama Simba ishinde au ifungwe au itoke sare, mnaweza msiamini lakini hebu tuangalie kitalaamu, unawezaje kuibadilisha timu ndani ya siku moja ukiwa na akina Balua, Chasambi halafu mwenzako alieachia timu alikuwa na wachezaji wazito akina Chama, Saido, Babacar, Micquisone lakini hakuwa akipata matokeo mazuri.

Nimeshangaa sana leo Ngoma anawapelekesha akina Akaminko, Yahya Zayd na Feitoto, Ngoma anateleza sio kawaida, Mzamiru kawa mwepesi, Che Malone anasafisha ukuta wa yericko sio kawaida, Ayoub huku golini hana kazi.

Yaani Fredy Michael Koublan pamoja na ubovu wake na uchezaji nyoronyoro lakini ameonekana mtu leo.

Kuna jambo limetokea ndani ya uongozi na hili sio lingine aidha akina Jaribu Tena wamekubali yaishe na wale wajanja wamepewa timu na wameonyesha kweli kazi wanaijua.

Azam hii namna ilivyokuwa na watu wa hatari awali sikutaka kabisa kuangalia mpira maana ukiangalia kikosi chao na cha simba unaona kabisa leo tunakula kono la nyani, lakini wale wajanja wenye password ya simba wamepea timu na kama hali itaendelea hivi wanabeba nafasi ya pili.
 
Kama Wewe ni Shabiki Kazi yako ni Moja tu...Kushangilia baasi.

Kilomolomo tuache..!

Sasa inatokea Shabiki wa timu anakashifu timu na Wachezaji, Wapinzani nao Wanakashifu Wachezaji wako pia.

Sasa Saikolojia ya wachezaji inakuwaje..?
 
Simba iko nafas ya 3, ila vinyesi kama nyie mnaumia simba kua nafas ya 3...sjui hii tunaiitaje ..
 
Simba iko nafas ya 3, ila vinyesi kama nyie mnaumia simba kua nafas ya 3...sjui hii tunaiitaje ..
Hakika wewe ni kolo og, na umejaa sumu kwa kukandwa wiki na uto, mimi huwa ninawajua kwa kusoma kauli zenu za matusi mazito, sisi uto hatuna matusi, huwa tuna kauli za kukera mfano simba ni my wetu, Azam mdebwedo kauza mechi nk.
 
Back
Top Bottom