Ngumu kumeza

madeinmusoma

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
322
387
Kuna mdada alikutana na mkaka wakiwa safarini. Yule kaka akamuomba mdada namba ya simu, na njiani akamnunulia kila kitu alichotaka. Walipofika stand mkaka akamlipia usafiri mpaka home kwao alikokuwa anaelekea. Basi wakawa wanawasiliana kila siku. Siku nyingine wanatoka out, wanakula na kunywa na hela anampa.

Yule dada akawaambia marafik zake, "Nimepata bonge la bwana jamani, nitake nini mimi nisipewe?" Shoga wakamwambia, "Weee, tutaaminije!" Yule dada akampigia jamaa simu akamwambia, "Leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saluni. Nimemisi sana kwenda Club na marafiki zangu." Jamaa akamtumia laki 3 ya saluni na kumwambia kama isipomtosha aseme.

Wenzie wakasema, "Lo! shoga bwana umepata." Ilipofika jioni yula mwanaume akapiga simu kwa yule binti akamuuliza Club gani mnakwenda? Mdada akataja Club wanayotaka kwenda, jamaa akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue na yeyewatamkuta huko.

Baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake. Walipofika wakanywa, wakala na kucheza. wakarudishwa home kama walivyoahidiwa.

Kesho yake jamaa akamwambia yule dada, "Nataka kuzungumza na wewe ila please njoo peke yako". Yule dada akajikoki akaenda. Alipofika yule kaka akamwambia;

Jamaa: Nimempenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe, naomba ukamwambia hisia zangu hizi. Wala sina plan ya kumchezea, nitamuoa kabisa. Sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndie anaestahil kupajua nyumbani kwangu.

Dada: Mimi je?
Jamaa: Wewe nini?
Dada: Mimi utanipeleka wapi? Kwa hiyo mimi ndo unaniacha?

Jamaa: Mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi. Nilikuchukulia kama rafiki yangu, ndo mana sijawahi kuzungumza na wewe swala la mapenzi. Mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo. Tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele. Kama kuna kitu nimekifanya kwako ni kukushika mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya.

Dada (huku analia): Mbona ulikuwa unanihonga?

Jamaa (huku anacheka): Sikuwahi kukuhonga! Mimi nilikua nakupa kama rafiki yangu. Sina sababu ya kukunyima kama ninacho. Sijafundishwa hivyo. Na usidhani kama nitamuoa rafiki yako halafu wewe ukiniomba nitakunyima, hapana! Nitakupa kama ninacho, ila katu sitokupa kipaumbele kuliko mke wangu. Mke wangu akiridhika kwa nilichompa basi nawe utapata.

Dada: Siwezi kumwambia rafiki yangu, watanicheka mnooo! Wote wanajua wewe ni bwana wangu. Siwezi, naomba unipende mimi kaka yangu.

Jamaa: Siwezi kukupenda wewe kama mke wangu, sina hisia hizo kwako! Na usiogope kumwambia. Ni bora ukasema ajue wewe uliuelewa upendo wangu vibaya watakubembeleza na kukufariji, kuliko kukaa kimya. Maana mimi nitakapokutana na rafiki yako popote nitamwambia haja ya moyo wangu, nae atakaponikataa kwa kudhani mimi ni shemeji yake nitamuelewesha jinsi gani mimi tulivyo. Tena kujitetea ili kumpata nimpendae, nitaingia ndani zaidi na kumweleza kuwa nilikutuma wewe ujumbe huu na hukuufikisha. Hapo ndipo rafiki zako watakudharau na kukukebehi. Watakuletea maringo ya wazi wazi na utajiona huna thamani. Kuelewa vibaya sio taitzo ila tatizo linakuja pale ulipogundua kuwa ulichokielewa sicho nawe ukang'ang'ania.

Dada: Sasa kwanini hukunipenda mimi wakati ndo ulitangulia kuniona?

Jamaa: Sio kila kilichopo mwanzo kinastahili. Kuna vyenye kufaa lakini vipo kati au hata mwisho pia. Kikubwa usiwe na haraka katika kufanya maamuzi. Nikuulize sawali dada?

Dada: Ndio niulize.
Jamaa: Hapo ulipo una usichana wako?
Dada: Hapana.
Jamaa: Ni nani alieutoa?
Dada: Mpenzi wangu wa kwanza.
Jamaa: Yupo hai au amekufa?
Dada: Yupo hai na mpenzi wake mwengine.

Jamaa; KWANINI HUKULAZIMISHA NDOA KWA MTU ALIYETANGULIA KUUJUA UNDANI WAKO NA UJE KULAZIMISHA NDOA KWANGU MIMI MTU NILIETANGULIA KUZIJUA TAMAA ZAKO? Rafiki zako wote uliokuja nao sike ile Yule niliekuagiza kwake alikua mstaarabu sana kati ya marafiki zako wote, hakunywa pombe, hakuupenda mziki mlimlazimisha tu kuja mara nyingi alikua ni mtu wa kukaa chini, mara kwa mara alisisitiza tirudi nyumbani. Hata tulivyokua tukiondoka alinambia ni vema na wewe uneenda kupumzika maana umechoka pia sisi nyumbani tutakwenda wenyewe sio mbali na hapa tukichukua Tax. Wote mlimbeza na kumwabia ebuuuuu huko hiyo ndo kazi ya mwanaume tupeleke sie utupe na hela ya supu kesho. Hivi mlimpata wapi rafiki kama yule mbona haendani na ninyi?

Dada: (Huku akilia akajibu) Yule ni house girl wetu. Huwa napenda kutoka nae ili baba na mama wasihisi nakwenda kufanya mabaya huko niendako.

Jamaa: Basi nenda kamwambie house girl wenu kuwa NAMPENDA SANA. AJE KWANGU AFANYE KAZI YA KUNIPENDA KWA DHATI NAMI NITAMLIPA UPENDO.

DEATH GETS EASY WHEN LIFE GETS TOUGH.
 
Mapenzi ya kuanzia kwenye mabasi ni shida! Nakumbuka mwaka 2016 Lecture wangu alifanyiwa kitumbaya na demu pale Mbeya!
Kwenye basi kamuunga demu vizuri wakafikia wote Guest moja. Demu kamuomba amrushie vocha ya 2000 kwa Mpesa, kumbe alitaka tu kujua PIN yake.
Kisha demu kampa jamaa maraha ya kurusha roho ni balaa!, kuchanganya na uchovu wa safari jamaa akalala kama maiti, Looh! Usiku demu kapakua pesa yote tangu mfukoni mpaka kwenye simu, akasepa gizani! Lecture wa watu mpaka leo ukimueleza habari za mademu ni mbalimbali!
 
Back
Top Bottom