BiMkubwa
JF-Expert Member
- Jan 9, 2007
- 529
- 97
Nivea, story yako ni ya upande mmoja ila pia mumeo naye yaonekana anamkwepa mama yake. Kuna jambo na kuna walakini. Mtu huwezi kumpita mama yako mzazi sebuleni kwa salaam za hi! Hata siku moja! Imagine ingekuwa mama yako? Usije chekelea hapo pengine mama amegundua kitu kilichojificha kwa mumeo na kumkanya wewe unashabikia wakati hujui? Au labda anataka kuwaaga nyie mnajifanya mko busy? Kuna namna nyingi wazee huwa wanahitaji kuchukuliwa. Kuna binti hivihivi kama wewe akawa anamnanga mama mkwe kumbe mama alimbamba mwanaye mjini akitokeq gesti. Sasa mtoto aibu. Bqsi siku ya siku binti alimtolea mbovu mama mkwe ndipo mama mkwr akamweleza kuwa siku zote unaniona hapa namsubiri mumeo nataka niobgee naye jambo na ananikwepa na jambo lenyewe ndio hili. Binti aligwaya! Mama mkwe kumbe alishapaki vitu na aliondoka usiku uleule.
Kwa hiyo binti punguza munkari. Wapo wazee wenye matatizo na kuna namna ya kuwachikulia. Huyo ni mama mzazi wa mumeo. Hajaja kuchukua penzi lako. Kuwa mature na umwonyeshe kuwa pendo la mwanaye bado lipo na linawatosha wote. Mwanaye atamjali na atakujali na wewe. Usiharibu uhusiano wenu mapema. Safari bado ndefu ktk ndoa.