#COVID19 Nchi ya Australia, kwa mara ya pili imesitisha Visa ya Novak Djokovic kwa kutokuchoma Chanjo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,505
9,286
Nchi ya Australia, kwa mara ya pili imesitisha kibali cha kuingia nchini humo cha mchezaji maarufu wa tenesi, Novak Djokovic, kutokana na utata kuhusu haki ya kuendelea kubaki nchini humo bila ya kuwa amechoma chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Uamuzi huu uliotangazwa na waziri wa masuala ya uhamiaji wa Australia, Alex Hawke, amesema umechukuliwa kwa kuzingatia sheria ya afya ya taifa hilo, hatua inayomaanisha kuwa ana uwezo wa kumfukuza nchini humo. Hata hivyo licha ya uamuzi huu, Djokovic, raia wa Serbia bado ana uwezo wa kufungua jalada jingine la kesi kipinga kufukuzwa nchini humo.

Djokovic ambaye anashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora wa mchezo huo duniani, alikuwa amepangiwa kuanza lkucheza mechi yake ya kwanza ya mashindano ya Australian Open, yanayotarajiwa kuanza Jumatatu ya wiki ijayo.

Uamuzi huu una maana pia, huenda Djokovi akakabiliwa na adhabu ya kutoruhusiwa kupewa hati ya kuingia kwenye taifa hilo kwa muda wa miaka mitatu, licha ya kuwa adhabu hii inaweza kuondolewa.

Mshindi huyu mara 9 wa taji la Australian Open, alikuwa anatarajia kutetea taji hilo kuanzia wiki ijayo, ambapo ikiwa angeshinda, kungemfanya awe mchezaji tenesi wa kwanza mwanaume katika historia kushinda mataji makubwa 21 (Grand Slams).

Kwa mara ya kwanza hati yake ya kuwa nchini humo (Visa) ilibatilishwa saa chache tyu baada ya kuwasili kwenye mji wa Melbourne, Januari 6, baada ya mamlaka ya usimamizi wa mipaka kudai kuwa alishindwa kutoa uthibitisho unaohitajika ili kuonesha aliruhusiwa kitabibu kutokuchoma chanjo dhidi ya UVIKO 19.

Tangu igundulike kuwa mchezaji huyo hakuwa amechoma chanjo lakini akaruhusiwa kuingia nchini humo, kuliibua mjadala mkali miongoni mwa raia wa Australia.
 
Back
Top Bottom