A
Anonymous
Guest
Kuna Mwalimu (jina linahifadhiwa) anayefundisha Shule ya Nanhyanga Sekondari iliyopo Tandahimba Mkoani Mtwara, anaweza kudhuriwa na jamii inayomzunguka kwa kuwa wanamtuhumu kwa mambo mbalimbali ambayo Uongozi wa Shule pia unajua.
Nimekaa na Wananchi wa hapa Nanhyanga nimebaini kuwa wanamtuhumu Mwalimu huyo kwa mambo kadhaa, ikiwemo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wanafunzi na wake za watu.
Mengine ambayo nimebaini anahusishwa nayo ni uchomaji moto kwa vyumba vya madarasa ya shule, hii ulitokea mwezi Mei 2023.
Pia jamaa anahusisha na wizi wa mali za shule.
Baadhi ya tuhuma hizo ziliwekwa wazi katika Kikao cha Wazazi kilichofanyika mwezi wa tisa Mwaka Huu (2023) lakini ajabu ni kuwa uongozi wa Shule umenyamaza kimya.
Nimeandika uzi huu kuushauri uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kuchukua hatua za haraka kwa usalama wa Mwalimu huyu na usalama wa Shule ya Nanhyanga.
Nayasema haya kwa kuwa kijijini hapa kuna minong'ono juu ya kutaka kumdhuru Mwalimu huyu, ninavyojua kama hatua hazitachukuliwa mapema basi kuna uwezekano wa hilo ninalosema kutokea.