Napinga Mikel Arteta kupewa mikoba ya Wenger sababu hana uwezo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,899
218,683
Kumpa kijana huyu mikoba ya kufundisha Arsenal itakuwa kamari ya kijinga sana kuicheza na nachukua nafasi hii kupinga kabisa njama hizo .

Arteta aliyezaliwa 26/3/1982 hana uzoefu wa maana wala ujasiri wowote wa kuipa Arsenal mataji , katika kipindi alichoitumikia Arsenal pamoja na kupewa Arm band hakuwahi kutoa mchango wowote wa kusaidia timu yake , hata kwa kuhamasisha kwa maneno tu kama wafanyavyo Ma Captain wa vilabu vingine , aliitwa Man City kuwa kocha msaidizi July 3 2016 , mpaka sasa ni chini ya miaka miwili , huyu si wa kupewa timu tajiri kama Arsenal

Arsenal inahitaji kocha mzoefu mwenye mafanikio yasiyotiliwa mashaka, Au la kama viongozi wanapenda kumpa kazi hiyo yule aliyechezea klabu yao basi nafasi hiyo wapewe wachezaji wenye uchungu mkubwa waliotoa jasho na damu kuipa timu mataji, wachezaji hao wapo na majina yao yanafahamika, lakini si Arteta.

Nakala imfikie Arsene Wenger.
 
Acha kupiga ramli wewe,

Ipo siku huu uzi utafufuliwa kukuumbua, kama baadhi ya nyuz zako type ya hii zinavyokuumbuaga

Hao makocha wazoefu wamepewa man u wameisaidia nini? Unajua hata arsene alipokuja arsenal, waandishi walikebehi, ARSENE NI NANI?

Zidane aliishusha had daraja madrid B, lkn kafanya vzr Madrid A

Fergi alianza vibaya, had akataka afukuzwe,

Usitoe garantii kuwa atafail, wanaweza kuja hao Wazoefu wakapoteana sana tu, tumeona kwa van gall kwa man u,

Kavurunda,

Wabongo tunawajua kila mtu kocha kila mtu mchambuz wa mpira, lkn mmeshindwa kuisaidia taifa starz kwenda hata CHAN
IMG-20180516-WA0005.jpg
 
Kumpa kijana huyu mikoba ya kufundisha Arsenal itakuwa kamari ya kijinga sana kuicheza na nachukua nafasi hii kupinga kabisa njama hizo .

Arteta aliyezaliwa 26/3/1982 hana uzoefu wa maana wala ujasiri wowote wa kuipa Arsenal mataji , katika kipindi alichoitumikia Arsenal pamoja na kupewa Arm band hakuwahi kutoa mchango wowote wa kusaidia timu yake , hata kwa kuhamasisha kwa maneno tu kama wafanyavyo Ma Captain wa vilabu vingine , aliitwa Man City kuwa kocha msaidizi July 3 2016 , mpaka sasa ni chini ya miaka miwili , huyu si wa kupewa timu tajiri kama Arsenal

Arsenal inahitaji kocha mzoefu mwenye mafanikio yasiyotiliwa mashaka , Au la kama viongozi wanapenda kumpa kazi hiyo yule aliyechezea klabu yao basi nafasi hiyo wapewe wachezaji wenye uchungu mkubwa waliotoa jasho na damu kuipa timu mataji , wachezaji hao wapo na majina yao yanafahamika , lakini si Arteta .

Nakala imfikie Arsene Wenger .

Arsenal wamebadili mfumo wa uongozi wa meneja baada ya Arsene kuondoka.

Wanataka Arteta awe kocha mkuu yaani head coach na sio meneja ambae anahodhi kila kitu.

Hiyo ni baada ya kumlata Sven Mislintat kutoka Borussia Dortmund ambae ndiye anaeshughulika na usajili wa wachezaji.

Hiyo ni moja ya sababu kubwa ya Wenger kuondoka Arsenal baada ya kuja huyo mjerumani ambae ndiye aliefanikisha kumleta Obamiyang.

Hivyo ikiwa Arteta akakubali nafasi hiyo ya Head Coach basi Santi Cazorla atakuwa msaidizi wake pamoja na jopo lake la makocha au backroom staff.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom