Naomba msaada tafadhali

Jumakwamba

New Member
May 18, 2024
2
8
Habari, mimi nimeoa nina mke na nimezaa nae watoto wa nne, mke wangu ni mzaliwa wa tanga, kuna mistake ambayo nilifanya nilijikuta natoka nje ya ndoa yangu na kuanzisha mahusiano na binti mwingine (mchepuko) ambae ni mzaliwa wa kondoa (mrangi) na huyu mchepuko pia nimezaa nae watoto wawili. Mke wangu amegundua kuwa nimechepuka na nimezaa nje ya ndoa yangu, furaha imetoweka ndani ya nyumba na mke wangu anataka nimpe talaka tuachane. Kiukweli nashindwa kumuacha mke wangu kwasababu ni mwanamke mwenye kujielewa sana, mpambanaji na pia ndie nilieanza nae tangu sina kitu mpaka Leo hii mungu kajaalia nina maisha mazuri

Niliteleza kuchepuka na kuanzisha mahusiano na huyu mwanamke mwingine wa kirangi na kuzaa nae

Kitu sahihi ambacho nimewaza au naona ni sahihi ili kunusuru ndoa yangu ni kuachana na huu mchepuko ili nibaki na mke wangu tulee watoto wetu kwasababu huyu mchepuko kwanza hana akili ya maisha anachojua ni starehe na kupenda vitu vya thamani ambavyo havina maana katika maisha yani hawazi maendeleo yoyote zaidi ya starehe na kuvaa nguo mpya tu

Nimewaza niwajengee watoto niliozaa na huyu mchepuko kisha nimpe msingi afungue biashara ili hiyo biashara atakayofungua ndio iwe inapatikana pesa ya kulisha watoto, na nimepanga kuwakatia Bima ya afya watoto ili iwasaidie pindi wakiumwa kwa maana mimi nibakie na jukumu la kuhakikisha tu watotoe wanasoma na kulipiwa Ada shule.

Sihitaji connection yoyote na huyu mchepuko ili niweze kukaa na mke wangu kwa amani na yeye nimuache na maisha yake.

Naomba kujua, nikimfungulia biashara ili iwe inasaidia kulisha watoto niweze kuepeka suala la kutoa pesa za kila siku za matumizi ya watoto ni sahihi au si sahihi?! Naomba ushauri wenu na mawazo yenu nini sahihi nikifanye maana naona tayar nishachanganya Unga na cement kwenye maji mpaka sasahivi, nishauri chochote ambacho unahisi kitanisaidia
 
Kuwa mpole
Anahasira muache kwanza akapumue maana ulilomfanyia hakutegemea

Ndiyo Huwa tunawaambia wanaume hakikisha mkeo anapaswa hisia ya kuwa una mwingine ikija tokea unamtoto nje hatapata shida sana ila kama anajua wewe ni mchungaji wa kwake tu hiiiiiiii siku akija kujua kua una mtu mwingine utajuta

Safari nyingine ueleweke kama hueleweki vile
Hivyo ndo maisha ya wanaume halisi
 
Ndo wewe ulikuwa unaandika Uzi wako huo
FB_IMG_1715888954881.jpg
 
Pole sana Mkuu Kwa changamoto unayopitia...

Umefanya vizuri kurudi nyuma na kujisahihisha baada ya kugundua makosa yako

Jambo la muhimu ni kuangalia namna sahihi ya kuhakikisha hao watoto Kwa nyumba ndogo pia wanapata haki zote za mtoto Kwa Wazazi ikiwemo kusoma/bima ya Afya/mahali Pazuri pa Kulala/mavazi n.k

Nikupongeze Kwa kuanza kufikiria kuhusu kuwafungulia Mradi utakaowasaidia kuwaendesha maisha.

Kuachana na Mama watoto wako(huyo nyumba ndogo isiwe kigezo cha kuwanyima haki zao za matunzo)

Kama hutaki kabisa mawasiliano na Mama watoto wako, muombe uwachukue na uwalee mwenyewe
 
Cha kufanya hapo rudi kwa mkeo, achana na mchepuko we jali watoto ulozaa naye hakikisha wanapata mahitaji ya msingi. Usijiroge kumfungulia biashara utapigwa pesa bure, kama hajui maisha ataweza biashara?
 
wakati unamtomba na kumkojolea ndani ulikua unatomba kitanda hata ugundue leo kua hana akili?? wewe ni mwehu umevuna ulichokipanda bora usingezaa at least kesi ingekua ndogo na watoto wawili juu!! hamtaachana kamwe mna dam inayowaunganisha ambayo n watoto wenu, unalo umelikoroga jepesi kunywa hivohivo
 
Unasema uliteleza?

Uliteleza na umezaa na mchepuko watoto wawili! Sasa hivi ndio umekuja kugundua kua mchepuko hauna akili ya maisha na mkeo ndio bora sio?

Mkeo alikuvumilia toka huna kitu mpaka ukawa na maisha ila malipo yako kwake ukaenda kwa mchepuko na kuzaa nae watoto wawili,

Huna hadhi ya kuendelea kuishi na mkeo,ulipata mke mwema ila upumbavu wako unampoteza,hapo hakuna ndoa tena,

Jambo jema na la maana unalotakiwa kulifanya ni kumpa talaka huyo mkeo ili akaishi maisha yake,na wewe nenda kwa mchepuko wako coz uliuona nibora kuliko mkeo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom