Naomba mawazo yenu kozi ya kusomea ufundi magari

Mimi ni kijana wa miaka 19, nipo Kigoma, nilimaliza kidato cha nne mwaka jana. Na nilipata div 4 ya point 33. Nilienda Veta nikasoma udereva na nina cheti pamoja na leseni daraja D, na tayari nimeshakuwa dereva mzuri tu, kwakuwa nilianza kuendesha gari kabla hata ya kwenda Veta kusomea. Lakini kwasasa nina mpango wa kwenda Veta kusomea kozi za ufundi magari.

Sasa naomba kuuliza ndani ya kozi za ufundi wa magari ni upande upi ambao unaweza kuwa na soko nzuri baada ya kumaliza mafunzo.. mf.. Umeme wa magari, kunyoosha bodi za magari n.k.

Kwa yeyote anayefahamu naomba kufahamishwa pia. Asanteni!!!
Umeme wa magari
Mechanics

Zina Dili Nyingi sana ila ni kazi Mbili tofauti

Chukua Auto electrician

Mechanics tuachie wenyewe


Ila hakikisha unaijua vizuri umeme jifunze kusolve gari mbali mbali haswa hizi za kizungu (ford.benz.daf.bmw.man.volvo.scania.man.) hakikisha unapiga gari ndogo na Kubwa

Good luck mdogo wangu.

Kaza sana fuvu uwe fundi mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeme wa magari
Mechanics

Zina Dili Nyingi sana ila ni kazi Mbili tofauti

Chukua Auto electrician

Mechanics tuachie wenyewe


Ila hakikisha unaijua vizuri umeme jifunze kusolve gari mbali mbali haswa hizi za kizungu (ford.benz.daf.bmw.man.volvo.scania.man.) hakikisha unapiga gari ndogo na Kubwa

Good luck mdogo wangu.

Kaza sana fuvu uwe fundi mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani sana big bro
 
Back
Top Bottom