Nafikiri hii ndiyo sababu ya matajiri kuitwa katili wasiyo na utu

Fanton Mahal

Senior Member
Mar 22, 2024
112
375
Habari wanajukwaa,

Heri ya Kwaresma kwa ndugu zangu wakristo.

Ramadham Kareem kwa ndugu zangu waislam.

Kama ilivyo kwa wengi, katika harakati za upambanaji unajikuta una team up na wadau kadhaa katika kujaribu kuona ni namna gani mnaweza mkayafikia malengo kwa ukubwa, haraka na unafuu. BAsi na mimi ni mmoja wapo.

Nafanya biashara ya kuuza huduma. Nilianza alone lakin baada ya muda nikaona ni wakati muafaka kuongeza nguvu kazi tusaidiane majukumu. Nikapata kijana ambaye yeye kazi yake kama alivyoji profile ni Sales person. Nikamchukua nikamuweka ofisini tuanze maisha ya kushirikiana majukumu.

Alikua anafanya kaz kwenye moja ya miradi maarufu tu inayoendelea hapa jijini Dar es salaam, project ya wachina. Baada ya ku discuss terms na conditions tukaanza kazi. Tulikubaliana kuwa ni jukumu langu;
  • Kumuwezesha vitendea kazi
  • Nauli kila siku akiwa sokoni
  • Mshahara kwa mwezi
  • Commission (kubwa sana)
  • Bonus /nyogeza ya mshahara kulingana na anavyo perform majukum na kwakua sales is about numbers so iko waz anaweza kabisa aka predict baada ya muda gani atakua na nyongeza kiasi gani
  • Mawasiliano
Hayo ni haki yake kabisa. Sambamba na hayo tukawekana waz kabisa kuhusu wajibu wake pia ikiwemo
  • Target (ndogo sana ya kupata maximum 2 sales per month - 30 days)
  • Ku submit report (daily and weekly), nk.
Niwe mkwel kijana hakuanza vibaya lakini pia hakua vizuri kama ambavyo nilifikiri au kama vile alivyojipambanua. Nikaona sio tatizo sana, nitam coach. Na tukawa tuna kwenda vizuri kawaida.

Sasa kiasili, mimi sio wale watu ambao ni "Bossy type" japo nina u serious wangu wa kutosha tu. Napenda sana as long as work is involvesld, kuwa karibu na team players wangu. Kwakifupi huwa si entertain gap between me and my guys (ninao wa 4, office admin, tech assistant, sales guy na mmoja ambaye ni oversea sio office based).

Sasa baada ya muda kupita naona kijana amekua haeleweki na performance yake honestly hainiridhishi kabisaaa and inside my heart am deeply dissapointed amd am really thinkimg of what to do.

Kijana wa sales
  • Ja meet target. Yan ni 0%
  • mchelewaji ofisini
  • Hapokei simu hata iweje na anajua simu zangu ni strictly ni za kazi, ukitaka kuwasilana nae ni text tu kama yuko nje ya ofisi
  • Hatoi taarifa kama atachelewa, kwakifupi anaweza ondoka leo jion kaniacha ofisin (maana ninkawaida yangu kufanya kaz mpaka late hours) na akaja kesho akanikuta (ni kawaida yangu saa 12 asubh niko ofisni) , na hapo yeye kaja kachelewa but hakuna maelezo anakupa, ofcz huwa siulizi.
  • Hatumi report za kazi, kuna time nakua na kaz nje ya ofisi au nje ya Dar hata kwa week 1, hivyo hatuonani lakin hutaona report mpaka upige kelele kwamba nataka report.
  • Na unapokua mkali (kitu ambacho sikipend japo nakiweza) , basi dogo sio muoga kabisaa anabishana na wewe kana kwamba wewe ni mtoto au mfanyakazi mwenzie tu, huna la kumwambia.
Sasa nimekaa sana nikawaza namfanyaje huyu kijana, ni mdogo tu around 23 years (maana ndivyo wadogo zetu wa leo hujiona, kwamba ni watoto).

Nimeshafanya juhudi sana za kujaribu kumsaidia nijue anashindwa wapi kufanya kaz akapata wateja, nampa maelezo na maelezo na maelezo lakin wapi.

Nilipoona labda maelezo hayatoshi nikaamua kufanya kwa vitendo ili aone kwamba haya ninayomueleza sio tu naongea toka hewan, yanafanyika ndio maana namsisitiza afanye hivyo.

Nikawa natenga siku 3 kila week naingia sokoni kufanya marketing, mpaka mwez unaisha mimi nikifeli sana naimgiza wateja wawil lakin huwa namba inasoma mpaka 3 au 4 sometimes. Yeye hana anacholeta ofisin zaid ya stori na maelezo.

Nikaona bado labda message yangu hajaipata vizuri, nikabadil utaratibu, badala ya kwenda sokoni /marketing kivyangu na yeye kivyake ,nikaamua kwamba acha tushiriki pamoja. So nika mwambia kila unapokwenda kwa mteja wako kama una meeting, nijulishe twende pamoja.

Lengo hapa nilitaka kujua na kuona, ana engage vipi, nijue pa kumrekebisha, na pia nikataka nimfanya ANIONE MIMI the way na engage na hao hao watu wake ili ajifunze.

Mwisho wa siku nikienda nae marketimg, tunapata sales na tukirud ofisn naendelea kumpa shule na mambo mengine ili ajue namna ya ku improve.

UKUMBUKE HAPO MIMI SIO SALES PERSON BY PROFFESION, am purely a technical person. ni mtaa tu na harakat za ujasriamali zinanibidiisha kujifunza mambo mengi nisije kufa njaa.

Wakuu, nimefanya yooooote hayo lakin wapi!!!! Bila bila Na kitu kinacho ni irritate zaidi ni lack of morals kwake, hiv sasa naona hali inazid kuwa mbaya, kijana hana heshima kabisa.

Ujue mimi kama mtu ambaye nilishafanya ajira pia huwa najaribu kumtazama kijana kama mdogo angu ambaye anatafuta maisha na hili hunifanya kusita kuchukua hatua za haraka kimaamuzi nikiwa namatumain huemda ata change ila wapi!!.

IKabid niende hatua ya mbali zaid kwa kuongea nae kibiashara zaidi. Hii siku nikamuita nje ya ofisi.
  • Nikamueleza ni muda kiasi gani yupo hapa ofisin kwangu
  • Nikamkumbusha ni mshahara kias gani namlipa
  • Nikamuonyesha record za ni gharama kiasi gani ambazo nazi invest kwake katika masuala ya kazi nje ya mshahara.
  • Nikamuonyesha statements za bank ni jinsi gani income yetu as a companya ima flow
  • Nikamuuliza kwa hii comparison mdogo angu umafikiri hii pesa nayolulopa kama salary na marketing transport na ofisin unakula lunch na internet za bure, UNADHAN HIZ COSTS mimi nazi recover vipi kama wewe huna unachoingiza katika mzunguko? HANA MAJIBU.
Nikafikiri baada ya hii discussion ndefu sana labda anaweza pata akil atabadilika, WAAAAPI!

Wakuu huyu dogo sio ndugu yangu, sio jirani yangu, simjui hata ndugu yake mmoja, hapa tuko kikazi tu.

Nisaidieni, kwa haya yooote nimefanya, kuna kipi ambacho sijatimiza wajibu?

UNAWEZA KUJIULIZA KWANINI NIMEFANYA YOOTE HAYA?

Jibu ni simple kabisa, HIKI NDICHO NILIFANYIWA PIA japo mimi sikufika mbali hiv. Ajira yangu baada ya kutoka chuo, nilikua sijui chochote kuhusu kazi. Nakumbuka boss wangu ali dedicate sana muda wake kujifunza kuhsu kaz na majukumu maana hata mimi nilianza kufanya kazi kwenye kampuni ikiwa ndogo sana mpka inakua kubwa kufikia hatua ya kufanya total project sum ya 1B kwa mwaka by that time, toka 150M total project kwa mwaka wakati mimi ndio naingia hapo ofisin, kampuni ikiwa na boss na muhasibu tu.

Boss ndio kila kitu. So nilipoingia mimi cheap labour na degree yangu, boss alinifundisha sana sana sana kaz kwa moyo ili nimpunguzie majukum. That was 2014. Tofauti yangu na huyu dogo ni kwamba, nilikua nazingatia sana mafunzo.

Sasa hii ndio imenifanya kumvumilia kipindi hiki chote lakin kwasasa wakuu nahisi nimefika tamati.

Kwakua yuko kwenye mfungo wa Ramadhani, nime plan nitamuacha mpaka mwez wa Ramadhani uishe kisha nitam expell,

Nitamuondoa kazini, kuangalia namna nyingine.

Nakaribisha ushauri.

Wasalaam.
 
Brother hapo ndo mahala unapopata ridhiki yako,usikubali mtu yeyote apachezee kwa namna yeyote ile,ikitokea umeishiwa huyo kijana hutakaa umuone hapo,Kuna watu ni ma agent wa shetani sisemi kuwa dogo ni agent,ila kaa nae kwa umakini watu wengine wanatumika kukuangusha pasipo wao wenyewe kujua hilo,kuwa makini ndg.
 
Brother hapo ndo mahala unapopata ridhiki yako,usikubali mtu yeyote apachezee kwa namna yeyote ile,ikitokea umeishiwa huyo kijana hutakaa umuone
Thanks chief. Kuna mtu juz kaniaambia statement hii exactly.
He just saidi "dont think that they are too loyal , wakipata kwingine kwenye mshahara mkubwa, unafikiri watakupa time upate mbadala na wewe au siku ukiishiwa unafikir watajiuliza mara 2 kama wabaki au waende?
 
Maana unachofanya sio kuelekezana tena ni kulazimishana
Kuanzia chini na watu ambao hamna vision moja ni mzigo sana maana wengi wanakuwa hawa angalii mbele hawaamini kwenye kuanza kidg na kukua
Uko sahihi. Maana isije ikawa naona kama namsaidia kumbe namkwaza kabisaa . Yeye yuko kimpango mwingine, na wewe unataka umpeleke uelekeo mwingineee 😂😂
 
Uko sahihi. Maana isije ikawa naona kama namsaidia kumbe namkwaza kabisaa . Yeye yuko kimpango mwingine, na wewe unataka umpeleke uelekeo mwingineee 😂😂
Dogo anaona kama sehemu yake ya kutokea tu hapo kwako 😄 akipata sehemu ya kupiga uwinga kkoo hutamuona hapo
Lkn pia kwani unamlipa kiasi gani na unahusika na nini maana tusije kuwa tuna mlaumu tu dogo
 
Dogo anaona kama sehemu yake ya kutokea tu hapo kwako 😄 akipata sehemu ya kupiga uwinga kkoo hutamuona hapo
Lkn pia kwani unamlipa kiasi gani na unahusika na nini maana tusije kuwa tuna mlaumu tu dogo
Ofcz i dont pay him much. Japo kibiashara ni pesa nying, maana uki compare his value na what am paying him bado ni pesa nyingi sana

  • 300,000/= monthly salary
  • 7,000= daily marketing transport
  • 40% commission on spot kwa kila sale anayofanya
  • 3-5% salary incrementt kwa kila sale anayoifanya
  • lunch
 
Na ndio mana wahindi wanatoboa, hawatuki upuuzi kabisa, sisi acha tuendelee kuwaita wabaguzi wao wanaendelea kupata maendeleo
2013 nilishafanya kaz chini boss namba 1 muhindi halaf chini yake bos namba 2 Mkenya sisi ndio wafanyakazi, ule mziki wake huwa siusahau. Ndio hapa nafikiri pakanifanya kuwa na huruma probably. Ujue mimi ni muumini wa "usichokipenda, usimfanyie mwenzio" 😂
 
Ofcz i dont pay him much.

  • 300,000/= monthly salary
  • 7,000= daily marketing transport
  • 40% commission on spot kwa kila sale anayofanya
  • 3-5% salary incrementt kwa kila sale anayoifanya
  • lunch
Duh ebhanaee uchumi wa kati juu kabisa huu kwa watz wengi dogo ana uchezea 😄
Aisee gharama zote ingekuwa mm nisingesubiri hata mfungo uishe
 
Back
Top Bottom