Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 1,481
- 2,582
Wazo ni zuri na limelenga kuepusha contact zisikutane.Wakuu habari!
Leo nikiwa barabarani niliona magari mawili yaliyotaka kugongana uso kwa uso ghafla likanijia wazo ambalo limenisukuma kuandika uzi huu namna ya kuzuia ajali kama hizi.
View attachment 2958107
Picha nmetoa mtandaoni
Kikawaida ncha mbili za sumaku zikikutana hukwepana, mfano angalia hapa chini kwenye pichaView attachment 2958106
Sasa ikiwa magari yote yatatengenezwa kwa sumaku kwa mbele ktk mtindo wa ncha mbili zinazofanana yakikutana uso kwa uso yatakwepana (yatasukumana bila kugongana) yaani kama ule mchezo wa kusukumana lakini hapa itakua bila kugusana,
Chukulia mfano semi trailer inakutana uso kwa uso na V8, ili zisigongane zikwepane itahitajika sumaku kubwa sana iwekwe mbele ya gari mfano sumaku yenye ukubwa wa shina la mbuyu kwa kila gari yaani semi na V8, kitu ambacho kitaathiri uzito wa kila gari na balance haitakuwdpo,
Kwa vile chuma laini kikizungushiwa nyaya kwa mtindo wa coil kisha kuunganishwa na umeme huwa kinakua sumaku hii njia itafaa zaidi kutengeneza sumaku yenye nguvu kubwaView attachment 2958127
Zingatia pia ujio wa magari ya umeme.
Chini ntatoa ufafanuzi wa kimahesabu , Nakaribisha maoni kinzani.
Ok, zitapishana kwa force ambayo ni kali na pia kumbuka itakuwa haijahusisha concsiousness ya drivers, sasa hapo sio kwamba itasababisha madhara makubwa zaidi na ukizingatia nature ya lane za barabara zinawatumiaji wengi zaidi ya hizo machine mbili zitakazopishana?
Na vipi zikiwa katika mstari wa kufuatana je hazitovutana maana hapo gari ya nyuma itakuwa na magnetic na ya mbele itakuwa haina, hivyo chuma itakuwa attracted kwa magnetic.
Na vipi ikikutana na material mengine ya chuma, si ndio itavuta kila chuma kitachokuwa kwa range ya hiyo magnetic field ama hata yenyewe inaweza ikavutwa hapo itategemea na uzito wa chuma?
Hapo solition ni nini mkuu