Mzimuni family ft Q cheaf nyimbo inaitwa mpiga debe bonge la ngoma

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,279
1,942
Q CHIEF NI CHORUS KILLER WA TAIFA.

kupiga debe kwangu ilikuwa poa,
Fani katika maisha ikaja kuniokoa
Kwa radhi ya wazazi kijijini nikaoa
Mke nilimshusha hadhi kuwa na machangudoa

Mzimuni Family ndio kundi lililomtambulisha mwamba Savimbi, Chillah ukipenda muite Q Chief mtoto wa mzee Katilwa.

Chorus aliyopita kwenye wimbo wa FANI KATIKA MAISHA ulifanya na kutamani kila shabiki wa muziki wa kizazi kipya atake kujua ni nani kaim ba kwenye chorus ya huu wimbo.

Sauti nzuri na tamu masikioni ilibeba ujumbe mzito na mzuri toka kwa mashairi makini kwa vijana wa Mzimuni Family.

Q Chief alipata bahati ya kutoka kimuziki kipindi game ya muziki wa bongo ikiwa sana yani kila mtu(msanii) aliyetoa wimbo miaka yake ambayo anatoka jua wimbo ni mkali sasa wewe unayekuja inakubidi uje na wimbo mkali kuliko ambao umetoka.

Sauti ya Q Chief ilikuwa sauti moja kali yenye kuvutia masikio ya wasikilizaji wengi wa muziki ikiambatana na mashairi makali mazuri yenye jumbe nzuri pindi anapoimba. Wengi walipomsikia kwenye wimbo wa FANI KATIKA MAISHA wakajua ni mwanamke kutokana na sauti yake ilivyo tamu na nzuri masikioni.

Sauti ya Q ilinipa utata kama ilivyonipa utata sauti ya mkongwe Eddie Sheggy nilipomsikia katika wimbo wa MILIMA YA KWETU miaka ile nilijua ni mwanamke anaimba nilipokuja kupata ufahamu wa kutosha nikajua ni mwanaume kaumiza kwenye milima ya kwetu.

Chilla sasa baada ya kutoka kupitia Mzimuni Family ndipo mwaka 2002 kama sijakosea ndipo alipotupa baraka kupitia sauti yake kwa kutupatia album iliyobeba jina la MWANA MNYONGE japo huu wimbo kuna utata flani kuwa haukuwa wimbo wake alifanya wizi wake ukawa wake.

Temana nayo ayo. Kutoka fani katika maisha akaja na wimbo unaitwa ASEME huu kwangu mimi ni moja kati ya nyimbo kali toka kwake kwa muda wote, huu wimbo ulimsogeza karibu zaidi na wadau mpaka likaja wazo la album ya mwana mnyonge.

Baada ya album mambo mengi yalipita kati apo katika maisha ya umaarufu na mengine mengi yalikuwa ni mapito. Hii tutaendeleza siku nyingine nikiwa na mizuka.

Rudi kwenye tittle ya chagizo la Beberu. Q Chief ni mkali wa chorus wa muda wote Tanzania kuanzia

Mpiga debe
Tutaonana wabaya FT Soprano
Muda ft Chid Benz
Goodbye ft Chege
Zamani ft Jide
Asubuh ft Ay and Fa

Ukiamka asubuh muombe Mola anilinde/
Unakitu moyoni usinifiche nieleze/

Nipo ft Mr blue
Tuvumiliane ft Priva P
Natawala ft Dataz
Malume ft Moni Centrozone
Malume ft Rapcha

Leo inatosha siku nitakuja tupite na wimbo mmoja mmoja kuona mauaji ya Chillah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom