Mzazi mwenzangu wangu mvivu

flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,861
6,371
Habari zakupotezana ndugu zangu Wana JF wenzangu,

Mwezi wasita mwaka huu mzazi mwenzangu aliniomba aje aishi kwangu maana haileti picha nzurii yeye kuendelea kuishi kwao hali yakuwa anamtoto namda huohuo mimi mzazi mwenzie nipo hajisikii vizuri. Nikaona nikweli alafu ukizingatia anamtoto wangu, nampenda, na nina malengo naye, kwahiyo nikaona nivizuri aje tuishi tu.

Mwanzo mzuri kila mtu akawa anasimamia majukumu yake vyema. Ila nikagundua anaasili yauchafu, vilevile nimvivu sio kidogo.

Akaanza tabia yakuniwekesha net, nikaona sio mbaya ila hali ilipozidi siku moja nikamgomea, alichonijibu kuwa 'kila siku awe anaweka yeye tuu'. Hiyo kauli ilinikera sana ila aliweka tukalala kila mtu nahamsini zake.

Maisha yakaendelea ila kwakusumbuana sana kuhusu usafi wandani. Kwahiyo Amani haipo yakutosha maana akiambiwa kuhusu usafi, kupanga vitu vizuri anakuwa mbogo.

Sasa wiki iliyopita nimetoka zangu katika mizunguko yangu, akaniuliza unakunywa Chai nikamjibu ndio, maana toka aje hapa ishamwambia usiku chai awe anahakikisha inakuwepo kama sio maziwa yaani kati yahivyo viwili. Kumbe mda ananiuliza kuhusu kunywa Chai mda huo Chai hamna kwahiyo alichonijibu kuwa makazi yamemchosha amepika vingi. Kwahiyo akapika chai ila kwashingo upande.

Mda mwingi amekuwa analalamika makazi mengi, wakati tunaishi chumba kimoja na sebule namtoto tunaye mmoja tu! Sasa hizo kazi nyingi anazolalamikia najiuliza zipo wapi? Yaani anajihisi kama vile nimtumwa kufanya majukumu yahapa nyumbani wakati anashinda nyumbani. Nasio kusema ninamaisha mazurii labda ninahemeaga mboga 7 ila mara nyingi huwa nahemea mboga moja naukikuta tunakula mboga mbili ujue hiyo nyingine ilibakia mchana...... Sasa hapo kazi zipo wapi? Kama kufua huwa anafua mara moja kwawiki ila yeye nikaribia siku zote zawiki analalamika kuchoka.

Huyu nimwanamke wangu wakwanza kuishi nae na nilikuwa ninashauku yakuishi nae ila najihisi kukinai kuishi namwanamke. Imefikia hatua hata hisia nae zimekata kutokana navimanenomaneno, namigogoro yahapa napale maana hazipiti siku 3 bila kukwaruzana.

Kutokana natabia zake nimedhamiria/nahitaji kumswaga ila mara nyingi nikitaka kufanya hivyo amekuwa akigoma nakuomba msamaha ila mtaishije maisha yakuombana misamaha kila siku?

Ee Mungu niepushe nahuu msalaba. Nakama hayupo tayari kujirekebisha namuomba Mungu tuachane kwaamani yaani akubali matokeo arudi kwao maana mimi kwaupande wangu ishajipima kuwa siwezi kumvumilia na hizo tabia zake.

RIP Benjamin williamu mkapa.
 
Anyway,,,,umefanya kosa kubwa kumuita kimada, mtu ambaye Ni mzaz mwenzio, amekupa heshima ya kuitwa baba !!

Back to the point,,,, tafuta ndugu au watu wazima wamkalishe chini kujua Nini thamani ya mume na ndoa kwa ujumla ! Inaonekana ni mdogo kiumri huku akiwa na akili kizibo
 
Anyway,,,,umefanya kosa kubwa kumuita kimada, mtu ambaye Ni mzaz mwenzio, amekupa heshima ya kuitwa baba !!

Back to the point,,,, tafuta ndugu au watu wazima wamkalishe chini kujua Nini thamani ya mume na ndoa kwa ujumla ! Inaonekana ni mdogo kiumri huku akiwa na akili kizibo
Sawa mkuu nisamehe ila sijamwita kimada kwania mbaya

Nimependa ushauri wako
 
Pole sana, inawezekana alifikiri mkianza kuishi pamoja maisha yatakua full kushinda 'kitandani' sasa amekuta ni vice versa.
Usichoke kumrekebisha au ongea na watu wazima wamuelekeze ili muishi kwa amani maadam mna mtoto tayari sio vizuri kuanza kuhangaika na watu wengne wakati bado mnaweza kurekebishana na mambo yakaenda vema.
 
Pole sana, inawezekana alifikiri mkianza kuishi pamoja maisha yatakua full kushinda 'kitandani' sasa amekuta ni vice versa.
Usichoke kumrekebisha au ongea na watu wazima wamuelekeze ili muishi kwa amani maadam mna mtoto tayari sio vizuri kuanza kuhangaika na watu wengne wakati bado mnaweza kurekebishana na mambo yakaenda vema.
Sawa mkuu nimekuelewa sana tafanya hivyo...... Ila asipoelewa somo sitakuwa najinsi
 
Uzi wa tatu huu ndani ya wiki moja wakilalamikiwa wadada tabia za uchafu, uvivu na kutokuwa waaminifu.
Huyo bila shaka ni Bonge, mademu mabonge ni wavivu sana.
Kaoe Mbeya wadada wachapakazi. Wife wangu kila nikimwambia nikuletee house girl hataki anasema kama nina pesa nyingi nimlipe yeye. Anapiga majukumu yote kila siku bila malalamiko.
Huyo huenda utoto unamsumbua au alilelewa vibaya kwao.
Mvumilie
 
Back
Top Bottom