Mwl. Nyerere alisema heri Mjinga kuliko Mpumbavu. Sasa najiuliza huenda Mpumbavu ni bora kuliko Chawa

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,702
19,818

Najiuliza Kama kipindi hicho angekuwa na Maono ya Hawa machawa sijui angesemaje - Sababu Kama Mjinga akiambiwa / akijifunza anaelewa;

Na Mpumbavu ni Kipaji yeye anabisha tu na akiambiwa haelewi nadhani ni Bora kuliko anayejua lakini anaendelea kufanya anchofanya huku akijua kina walakini (nadhani tumbo lake linatawala kichwa chake)

By the way Mdau hapo chini Jasmoni Tegga (amesema kwamba Nyerere alimaanisha Kifaji na sio Kipaji kama wengi tulivyokuwa tunafikiri - Mimi ili nisiwe mpumbavu na nilikuwa Mjinga nalichukua hilo na kulifanyia Kazi....
 
Ccm imezalisha machawa hasa kipindi cha awamu iliyopita uchawa ulilipa sana naona wanaendeleza walipoishia
Amini nakwambia uchawa hauna Chama wala Itikadi - Uchawa umetapakaa kila mahali watu wamekosa mshipa wa aibu au unataka kusema chawa akivua kijani na kuvaa Gwanda anakuwa sio Chawa?
 
Siku hizi maisha yetu tumeyageuza kamari tu, hao unaowaita machawa wanafanya hivyo ili ku-bet waone kama kelele zao za kusifia zitawapatia chochote toka kwa mtawala.
 
Actually, Juliasi alimaanisha kifaji (liability, limitation, dhima, upungufu, udhaifu, kasoro, dosari, deni, ukomo, ulemavu), na wala siyo kipaji kama wengi wanavyodhani.

Wengi huchanganya sana matamshi ya maneno husika.
Asante kwa Kujibu hilo na kunifahamisha hilo ngoja nilifute hili swali tuendelee na la hawa Chawa, hapo unasemaje ndugu Mjumbe.....
 
Siku hizi maisha yetu tumeyageuza kamari tu, hao unaowaita machawa wanafanya hivyo ili ku-bet waone kama kelele zao za kusifia zitawapatia chochote toka kwa mtawala.
Na unaona hio ni price worth paying ?, The end Justifying the means ?!!! Hawa watu hawana conscious ?

Unadhani waasisi wa mataifa yote duniani wangekubali kufanya hata yasiyo sawa basi tu ili wapate chochote tungekuwa na wanamapinduzi ?

Narudi tena Huyu Chawa ni adui kuliko Ujinga, Umasikini na hata Magonjwa (sababu mgonjwa akizidiwa atakufa huyu chawa anaedelea kuishi na kuchafua hali ya hewa)
 
The Emperor has no Clothes - (Hatari ya Uchawa kwa mustakabali wa Taifa)

the-emperor-has-no-clothes-310649_1080x675.jpg
 
Nyerere alikua na chawa wengi mnooo
Hivi sio nyerere aliyesema tuache upuuzi wa kuitana waheshimiwa bali ndugu au yeye mwalimu ? Sasa hivi kuna mpaka Mtukufu Rais....
 
Hata pamoja na hayo alikua anaongoza kwa machawa
Machawa ambao badala ya kuelezea Sera za Kujitegemea walikuwa waanelezea na kumshukuru Kambarage kila wanapofungua vinywa vyao ? Watu wa zamani walikuwa na principles na ilikuwa ni aibu kwa mtu mzima kuanza kutoa sifa zisizo na mwisho labda kazi hio ilifanywa na watoto wa shule na watunga nyimbo kwa kutunga nyimbo za kusifia.....

By the way hao machawa waliokuwepo kwa kipindi hicho walijulikana kwa jina gani ?
 
Hahahahaaa

Zidumu fıkra sahihi za mwenyekiti wa CCM

ULISHIRIKI CHIPUKIZI MIAKA YA MWISHO YA 70 na early 80s?

Unakumbuka kuambiwa Kama husifii basi shhhhhhh wapelelezi watakusikia?

Unakumbuka tuliomba nyimbo nyingi sana ? Ma mzee Nnauye alikua master wa cheerleading
 
Kwamba Nyerere above Utanzania, Wananchi na Walipa Kodi...., Kwamba Nyerere ndio amewaletea hili Daraja au huu Mradi.., Ndio Nnauye alikuwa mzee wa kuipamba Tanzania na sio Nyerere..... kama alivyokuwa Komba na wana-propaganda wengine..., Kwanza kabisa ilikuwa Nchi alafu Chama, wananachi.....

Alafu ilitokea tu kwamba ile Myth na legendary status kila baya akawa anasingiziwa Kawawa na zuri anapewa Nyerere hizo zilikuwa ni story za mitaani watu kulishana matango pori..., Ingawa bado watu walimwita mzee haambiliki, mchonga meno, kwamba ni mzee wa juju na ile fimbo yake.... Lakini sio mzee mzima unapewa muda wa kushusha nondo unaanza kuleta mambo ya Muheshimiwa fulani (Jamaa alisema Hapana niiteni ndugu au Mwalimu)

Nyimbo nyingi zilikuwa zinatungwa kutokana ni nini amesema kwamba Nyerere amesema Kodi ianze n.k. (quotable quotes) Na hapa nasema haya kwa kuonyesha kwamba wazee wa zamani wana-siasa walikuwa wanasiasa kweli na principles zao sio hawa wa sasa na matumbo yao.... Mbunge badala ya kushusha nondo kuhusu shida zako unaanza kusifia kiongozi....
 
Tuna imani na nyerere… oyaaaa oyaaa oyaa

Wa lini wewe?
 
Tuna imani na nyerere… oyaaaa oyaaa oyaa

Wa lini wewe?
Tuna Imani na Karume Oyaa Oyaa Oyaaa..., Karume Kweli... KWELI..., Karume Kweli Kweli kweli kweli Karume.... Karume Kweli Kweli......

Tuna Imani na Kawawa... Oyaa Oyaa Oyaaa...,

Hizo ni nyimbo mashuleni kuonyesha solidarity.., tofauti na Kiongozi anachukua mike amepewa dakika tano atanumia sita na nusu kuleta sifa hivyo kukusa muda wa kuongea cha kuongea.....
 
Back
Top Bottom