Mwanamke zake sifa, usiache kumsifu

Jan 24, 2015
29
20
MWANAMKE ZAKE SIFA.

Kipindi wamtokea, ulimsifia kwanza.
Ndipo kakukubalia, leo ndio wake mwenza.
Upendo unafifia, kusifu ukipunguza.
Mwanamke yake sifa, usiache kusifia.

Sio mali kutumia, eti utamtuliza.
Nyumbani ukiingia, kama bubu wanyamaza.
Mkeo anaumia, au mume namkwaza?
Mwanamke zake sifa, usiache kusifia.

Msifu anapo vaa, bibie umependeza.
Baada tendo ongea, wife unaniweza.
Big up my dear, changanya na kingereza.
Mwanamke zake sifa, usiache kusifia.

Asante langu ua, kwa kola kutengeneza.
Kwa urembo waniua, kila siku waongoza.
Mwingine hatotokea, kwako wote ni viraza.
Mwanamke zake sifa, usiache kusifia.

Sifa hizi ziambatane na neno "ASANTE WIFE" hata kama kakufanyia kitu kidogo namna gani, mfano kakutoa kinyuzi kwenye nywele mwambie asante.

Pia neno lingine ni "SAMAHANI" hata kama utaona kosa lenyewe ni dogo.

Wanaume wengi tunaona kujishusha na kuomba msamaha kwa wake au wapenzi ni kujidhalilisha, tujue wanawake wanautashi na hisia kama sisi kwa hiyo kile tunachopenda tufanyiwe na wao hupenda wafanyiwe na wapenzi wao.

Ukipuuza haya akatokea mtu ima maeneo ya kazini kwake au mtaani au hata shamba boy wako akawa anamwambia ataona huyo mtu anaijua thamani yake, anamthamini na kumjali, kwa udhaifu wa kibinadamu basi mapenzi yake yatahamia kwa huyo mwanaume mwenye ujasiri wa kuomba msamaha, kusifu na na kushukuru.

N:B Neno "NAKUPENDA" lisikauke kinywani kwa kuwa neno hili kila siku huonekana jipya na huongeza radha zaidi kama utakua unalitaja kwa lugha tofauti tofauti na namna tofauti tofauti, mfano kwa kumnong'oneza sikioni kipindi kingine kwasauti kubwa wakati mwingine hata kwa kuandika kwenye karatasi kisha ukaweka kitandani au kwa sms na namna nyingine utakazo zibuni.
 
Back
Top Bottom