mwanamke unahitaji nini kingine ikiwa unahudumiwa kila kitu na mpenzi wako kuanzia chakula, malazi hadi mavazi?

MFALME WETU

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,708
6,546
Pole kama hauko sawa, Mungu akufanyie wepesi.

Moja kwa moja kwenye mada

Binafsi nina mchumba wangu namhudumia kila kitu ambacho mwanamke yeyote aliyekamilika ataitaji pamoja na kuwa ni mwajiriwa sekta binafsi.
kiufupi Madem zangu wengine nawatesa kwa kutowazingatia sana kwa sababu ya huyu main maana nilikua nampango wa kumuoa mwakani, ndugu zake wananifahamu ingawa sijaenda kujitambulisha rasmi.

Mara nyingi tukikutana au tukiwa tunaongea kwenye simu mada zake nyingi ni za jinsi ya yeye kujikwamua kiuchumi hali iliyopelekea hivi karibuni nimsaidie mtaji wa kuanza kilimo cha mahindi huko mkoani kitu ambacho nilikipinga sana sababu nimewahi kuinvest kwenye kilimo nikaambulia hasara kubwa sana ila alinishinikiza nikasema isiwe kesi, pesa makaratasi.

Sasa leo nimekaa nafikiria apa nikawa najiuliza ivi inakuaje mwanamke unaehudumiwa kila kitu na mumeo/mpenzi wako kuanza kuhangaika na hustles za kujitaftia hela, what for?

Dada umeolewa, hamna kitu utamwambia Baba Gee asikutimizie ila bado unahangaika na pesa za Michezo, vikoba na mikopo ya kausha damu, come on.!!

FB_IMG_1716026466153.jpg
 
Naunga mkono hoja kwakuwa sisi wanaume tunapenda kuvutia upande wetu...ila ukija kiuhalisia mapenzi yana matokeo mengi kuna mwenza kufa,kuachana na kususiana mambo ni mengi hutokeaga hapa katikati hasa watu wakishazoeana humo kwa ndoa so lazima mwanamke anayejielewa akae mguu pande mguu sawa...kama ilivyokuwa kwa mwanaume ukiwa huna pesa unadharaulika na mwanamke na kwa wanawake ipo ivoivo....mwaname atakudharau na kukuendesha anavyotaka....wanaume wengine huenda mbali hadi kuomba mikwundu na ukimnyima unakufa njaa maana hauna kitu ni tegemezi utafanya nini???

Kwa tunapoenda ewe mwanamke sikushauri uwe golikipa utateseka sana,utakuwa kila siku unaongea mwenyewe na utakufa na kihoro nina ushuhuda na hili swala.
 
Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa "Boredom"
Binadamu huwa wanahitaji msikosuko/changamoto za hapa na pale
Akipata kila kitu baada ya mda anakua Bored


Ila huyo wako ana jambo lake baada ya mda atakupiga na chenye ncha kali usisahau kuja tukupe ushauri
Trust your spirit.
 
Kwenye maisha kuna kitu kinaitwa "Boredom"
Binadamu huwa wanahitaji msikosuko/changamoto za hapa na pale
Akipata kila kitu baada ya mda anakua Bored


Ila huyo wako ana jambo lake baada ya mda atakupiga na chenye ncha kali usisahau kuja tukupe ushauri
Trust your spirit.
Zingatia sentensi "nilikua nampango wa kumuoa"
 
Back
Top Bottom