- Source #1
- View Source #1
Huwa navutiwa sana Historia za wanamke shupavu ambao walifanya mambo ya kuacha alama kwenye jamii zao na kukumbukwa mpaka sasa.
Katika pitapita zangu kwenye machapisho nikavutiwa na historia ya mtawala kutoka katika kabila la Waha wa Jamii ya Kitutsi, ukanda wa Kasulu sehemu za Heru Juu.
Imezoeleka kuwa wanaume ndio huwa machifu katika jamii mbalimbali za Kitanzania kabla na baada ya Uhuru. Sikuwahi kusikia mwanamke yeyote kuwa Chifu wa jamii fulani tofauti na Theresa Ntare. Tukiachana na Chifu Hangaya ambaye ni Chifu wa Heshima wa kabila la Wasukuma, naweza kuhitimisha kwa kusema Chifu Theresa Ntare ni Chifu pekee mwanamke katika historia ya nchi yetu Tanzania.
Mwami Theresa Ntare
Katika pitapita zangu kwenye machapisho nikavutiwa na historia ya mtawala kutoka katika kabila la Waha wa Jamii ya Kitutsi, ukanda wa Kasulu sehemu za Heru Juu.
Imezoeleka kuwa wanaume ndio huwa machifu katika jamii mbalimbali za Kitanzania kabla na baada ya Uhuru. Sikuwahi kusikia mwanamke yeyote kuwa Chifu wa jamii fulani tofauti na Theresa Ntare. Tukiachana na Chifu Hangaya ambaye ni Chifu wa Heshima wa kabila la Wasukuma, naweza kuhitimisha kwa kusema Chifu Theresa Ntare ni Chifu pekee mwanamke katika historia ya nchi yetu Tanzania.
Mwami Theresa Ntare
- Tunachokijua
- Kumekuwapo na maswali miongoni mwa Wanahistoria kuhusu Mwami Theresa Ntare kuwahi kuwa mwanamke Chifu Mkuu wa Machifu Tanganyika. JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vinavyoeleza historia ya Mwanamke huyu ambapo kwa ujumla wake vyanzo vyote vinaelekea kukubaliana historia za Mwanamke huyo kama ifuatavyo:
Mwami Theresa Ntare Alizaliwa Mnamo Mwaka 1922, Alikua Ni Mtoto Wa Chifu Ntare Heru (Kigoma). Theresa alipata Nafasi Ya kwenda Kusomea Sheria Barani Ulaya kwa sababu zamani Kulikuwa na Nafasi Maalumu Za Watoto Wa machifu. Inasemekana kuwa alikua ni mtoto Wa Kike Pekee kwa chifu Ntare. Baada ya kuhitimu mafunzo ya sheria alipata nafasi ya kuwa mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla ya Uhuru.
Kwa kuwa Chifu alikuwa na mtoto wa kike pekee Mwami Theresa Ntare Alikuwa Kiongozi wa Jamii ya Heru huko Kasulu, Kigoma na aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni Mkuu wa Machifu wote Tanganyika, akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958 ambapo makabidhiano yalifanyika shule ya sekondari ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare likipewa jina hilo ili kumuenzi mwanamke huyu.. Inaelezwa kwamba Mwami Thereza Ntare alitawazwa uchifu baada baba yake Mwami Ntare kukosa mtoto wa kiume.
Zama hizo jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake katika masuala ya Uongozi lakini hilo halikumfanya Mwami Theresa Ntare asiweze kuongoza vizuri na kishupavu. Mwami Theresa Ntare aliheshimika kama chifu wa Kasulu yote na sio tu Heru.
Alisimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru. Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja wa Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika.
Baada ya Tanzania kupata uhuru, serikali ilifutilia mbali tawala za Kichifu hivyo Theresa Uchifu wake ukakoma mnamo mwaka 1962. Hata hivyo, yeye aliendelea kuwa Mbunge hadi mwaka 1980.
Aidha inaelezwa kuwa kwa mara ya mwisho aliishi Magomeni Mikumi, ilipokuwa Ikulu ya kwanza sehemu inayoitwa Usalama, ndipo Ikulu ya kwanza Tanzania.
Kwa msingi huo, kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyopitiwa na JamiiForums, hoja inayomuhusisha Mwami Theresa Ntare kuwa Chifu Mkuu wa machifu Mwanamke Tanganyika ni za kweli. Hata hivyo, baada ya uhuru japo utawala wa Kichifu kusitishwa, lakini bado Machifu wameendelea kutambulika na kuheshimiwa. Mathalani, mnamo Septemba 21, 2021 Rais wa kwanza Mwanamke Samia Hassan Suluhu alitawaza kuwa Chifu wa Machifu alipohudhuria tamasha la utamaduni Mwanza.