Muwe makini sana, yamenikuta

HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
31,553
48,153
Mwaka mmoja uliopita ilinilazimu kufanya shoo ili nijipatie pesa. Nilipomaliza kupafomu nikiwa natoka ukumbini kuelekea nyumbani kumbe nyuma yangu kulikuwa na Mrembo akinifuatilia tokea nlipokuwa jukwaani mpaka nilipopaki mkoko wangu Mercedes Benz SL.

Nilishtuka sana nilipomuona Mlimbwende nyuma yangu, na kwa jinsi alivyoumbika nilishindwa kabisa kujizuia nikajikuta namuuliza Mtoto, unaitwa nani? Na yeye bila kuchelewa akanijibu kwa sauti moja nyororo sana na yenye kuchombeza "Naitwa MONICA"

Sio siri Mtoto mrembo sana, amekamilika idara zote kuanzia juu hadi chini.

Nikamuambia panda kwenye gari twenzetu tukapate msosi, akaanza kuniambia "wewe HARUFU sukari ya warembo kwa jinsi ninavyokuzimika nilikuwa nashindwa kabisa namna ya kuwa nawe, kwa kweli leo ndoto zangu zimetimia".

Alipomaliza kuniambia maneno hayo matamu, Mchizi nikaona nafasi si ndio hii. Bila kuchelewa hapohapo nikaomba mchezo, Mlimbwende si akanitolea nje(akanikatalia) au kwa lugha nyingine naweza sema akanitosa, na kuanza kusema "yeye sio maharage ya Mbeya"

Mimi nikaona isiwe tabu, yote kheri. Ikabidi niwe mpole sikulazimisha penzi.

Wiki nzima ikapita bila ya yeye na mimi kufanya mawasiliano yoyote.

Mara bila kutegemea siku moja usiku akaniibukia Geto huku mimi nikiwa nimelala fo fo fo nikastukia mlango unagongwa(mtu anabisha hodi). Kwa kweli alinikata stimu zote za usingizi wangu.
Nikamfungulia mlango, unajua nini kilichofuata? Kwa kweli tulikula sana raha za Dunia.

Tulipomaliza nikamrudisha nyumbani kwao na nikamisisitiza siku inayofuata(kesho yake) anipigie simu.

Basi huwezi amini ni baada ya takribani mwezi mmoja kupita ndio akanipigia simu na kuanza kuniletea habari ambazo hazina kichwa wala miguu.

Eti madai yake ana ujauzito wangu.

Huu si uzushi jamani!

Inawezekanaje?
 
Mimi mwenyewe imekuwa ngumu kukuelewa unachoongea bwana mdogo...

Naomba nikuulize, JKT umeshaenda au we form four tu?
 
Back
Top Bottom