Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,304
- 46,118
Kwa bahati mbaya, watu wengi, na wengine wapo ofisi za juu kabisa katika nchi, wanajua historia ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kinadharia kwa kuegemea tu yale yaliyoandikwa, japo siyo ukweli.
Binafsi nilibahatika nikiwa bado nasoma chuo kikuu kupewa historia ya kina kabisa kilichosababisha na kilichotokea mpaka kukamilika kwa Muungano. Maelezo hayo niliyapata toka kwa marehemu Ibrahim Kaduma, ambaye wakati wa Muungano, alikuwa miongoni mwa wasomi wachache sana wa Tanganyika, na alikuwa kwenye circle za serikali ya Tanganyika kama mtaalam wa uchumi wa Serikali ya Tanganyika. Baadaye alikuwa waziri wa wizara 4 tofauti, ikiwemo mambo ya nje, wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere.
Ukweli ni kwamba si Nyerere wala Karume, miongoni mwao alikuwa na wazo la Muungano, wala aliyehitaji Muungano. Muungano ulifanywa kutekeleza ombi la US.
Mwaka 1964, Henry Kissinger, Fireign secretary wa Marekani, myahudi anayetajwa kuwa mwenye very high IQ, alimwendea Hayati Jomo Kenyatta, na kumwambia kuwa aichukue Zanzibar kwa sababu asipofanya hivyo, Zanzibar inaweza kwenda Eastern Block. Mzee Kenyatta akasema, hawezi kwa sababu mtu ya kule ni goigoi sana.
Kissinger alimwendea Mwalimu Nyerere, tena wakati huo Mwalimu akiwa rafiki mkubwa wa Rais wa Marekani, akamwambia hivyo hivyo. Mwalimu akauliza itawezekana vipi kwenda kumwambia Karume kuwa naichukua nchi yako. Kissinger akasema kuwa Karume ana jeshi dhaifu sana, yeye ataongea naye. Ndipo Kissinger akaenda akamwona Karume na kumwambia kuwa taarifa za kiintelijensia inaonekana sultani aliyefurushwa anaandaa jeshi, na kwa vile jeshi la Karume ni dhaifu, hataweza kupambana na jeshi la sultani, hivyo njia pekee ni kuungana na Tanganyika ili apate ulinzi wa jeshi la Tanganyika. Karume akasema atawezaje kwenda kwa mwalimu na kumwambia nataka tuungane halafu jeshi lako lije Zanzibar. Kissinger akamwambia kuwa yeye atamsaidia. Kissinger akarudi kwa Mwalimu, document ikaandaliwa haraka, Bunge likakutana usiku, udongo wa bara ukabebwa ukachanganywa na ule wa Zanzibar, Muungano ukawa umekamilika.
Wakati wa utawala wa Nixon, Mwalimu hakufurahia sera za Nixon, Tanzania ikachukua msimamo wa kuegemea Mashariki, lakini ikisema hawaegemei upande wowote.
Baada ya uhasama wa Dunia ya Magharibi na Mashariki kukoma, japo haiwekwi wazi, Mataifa ya Magharibi yanaendelea kuuunga mkono sana Muungano huu kwa sababu wanazoziita za kiusalama.
Mazingira hayo yaliyotuunganisha, yamepita. Si vema sasa kuutengeneza huu Muungano kwa mahitaji ya sasa na kwa namna inayoeleweka vema kuliko kuendelea kuwa katika Muungano wenye muundo uliotaka kutatua tatizo specific, ambalo nalo kwa nyakati hizo halikuwa letu?
Matatizo yetu ya muungano, kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na msingi wa Muungano wenyewe, tena ulioundwa kwa hali ya dharula baada ya Karume kutishiwa kuwa nchi yake itavamiwa.
Tafadhali mod, naomba ubadilishe heading, isomeke Muungano na siyo muingano.