SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,616
- 7,864
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa mchakato huu wa kuandika katiba mpya (kubadilisha katiba) ungetakiwa uanze kwa mjadala wa kitaifa na kisha kura ya maoni - referendum- (badala ya tume kukusanya maoni) juu ya uwepo wa muungano wenyewe na mambo ambayo tunataka kuungana/kushirikiana.
Lakini mchakato ndio hivyo tena umeshaanza kama ulivyoanza na sasa bunge maalumu la katiba linapitia na kujadili sura ya kwanza na ya sita za rasimu ya katiba. Kuna uwezekano mkubwa tu, bunge hili likashindwa kuvuka kizingiti hiki cha kwanza. Sura ya sita inafanya rejea kwatika mambo ya muungano ambayo yameorodheshwa kwenye "Nyongeza" (ya Kwanza?) ya rasimu ya katiba.
Bila ya shaka jambo kubwa na mijadala mingi juu ya katiba hii imejikita zaidi kwenye muundo wa muungano (serikali mbili ama tatu) . Tatizo ninaloliona katika mijadala mingi ni kuwa tumesahahu kabisa kujadili kwa uzito wake mambo ambayo tunataka kuungana ("Mambo ya Muungano"). Kwa maoni yangu mjadala ungeelekezwa kwanza kwenye mambo ya muungano kwa sababu ndio mambo ya msingi ambayo tunataka kushirikiana. Baada ya kukubaliana, kuridhiana na kuafikiana juu ya mambo yote tunayotaka kuungana/kushirikiano ndipo sasa tunaweza kuona ama kujadili vizuri zaidi muundo wa muungano ambao utakidhi kwa mambo ya muungano tulioafikiana.
Hii ni nukuu ya sehemu mojawapo ya hotuba ya Jaji Warioba kwa bunge maalumu la katiba:
Kwa sasa rasimu inataja mambo ya muungano yafuatayo:
Je, mambo haya yanayopendekezwa kwenye rasimu yanatosha? Nini kiongezwe? Nini kiondolewe? Kwa nini?
CC: Chabruma Skype Buchanan Ngekewa Nguruvi3 Pasco ...na wadau wengine!

Wakati Tume ilipokuwa inakusanya maoni, wananchi wengi wa Zanzibar kutoka makundi yote mawili, yaani wale waliotaka Muungano wa Serikali Mbili na wale waliotaka Muungano wa Mkataba, wote walipendekeza mambo mengi yaondolewe kwenye Orodha ya Muungano. Wale waliotaka Muungano wa Mkataba walitaka mambo yote yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano isipokuwa suala la ulinzi. Wale waliotaka Muundo wa Serikali mbili walitaka mambo yote ya uchumi yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.
Kwa sasa rasimu inataja mambo ya muungano yafuatayo:
1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
3. Uraia na Uhamiaji;
4. Sarafu na Benki Kuu;
5. Mambo ya Nje;
6. Usajili wa Vyama vya Siasa; na
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano.