Muufti akabidhi tiketi kwa wanafunzi 41 wanaokwenda kusoma elimu ya dini ya kiislamu Morocco

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,247
4,779
Wadau hamjamboni nyote

Taarifa kamili hapo chini:

Hatimaye Samaha Mufti wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir Ali Mbwana jana Jumanne amekabidhi tiketi kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma elimu ya Dini ya Kiislamu nchini Morocco kupitia Skolashipu alizoziomba kwa mfalme wa Morocco.

Ukumbi wa Mfalme Mohammed VI BAKWATA Makao Makuu uligubikwa na furaha ya aina yake kwenye hafla maalum ya kuwaaga wanafunzi hao iliyohudhuriwa na viongozi wa taasisi mbalimbali za kiislamu nchini

Wanafunzi hao ambao ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi mia mbili wanaotarajiwa kwenda nchini Morocco wataondoka mapema leo Jumatano tayari kwa ajili ya kuanza masomo ya miaka mitatu

Baadhi ya wanafunzi walishindwa kuongea kwa furaha na mwanafunzi mmoja kutoka Kigoma alipoulizwa anavyochukulia skolashipu hiyo akasema kwa ufupi ....

"Sasa Mufti ameanza Kazi.. Naam ! Kwa sababu kutayarisha masheikh ndiyo kushika hatamu" Amesema

Skolashipu hizo zinajumuisha Tiketi ya kwenda Morocco, Tiketi ya Kuja Tanzania na kurudi Morocco kila Mwaka wakati wa Likizo, Posho ya Dola mia Mbili kila Mwezi, Chakula, malazi, matibabu, Vitabu na vifaa vingine vya masomo, masomo na huduma zingine za jamii.
....

Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Jumatano 8.5.2024
Dar es salaam
 

Attachments

  • 1715166054813.jpg
    1715166054813.jpg
    393.7 KB · Views: 1
  • 1715166052430.jpg
    1715166052430.jpg
    459.1 KB · Views: 2
  • 1715166042607.jpg
    1715166042607.jpg
    603.7 KB · Views: 2
Wanaenda kusomea ili wawe masheikh, kuja kuhadaa akili za watu na abrakadabra za kidini. Bora wangepelekwa kusomea utaalamu wa mambo ya kueleweka ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii yao. Kuna udaktari, uhandisi, ualimu wa shule za kueleweka, kilimo na ufundi. Sasa kwenda kusomea dini nani anataka dini karne hii ya sayansi na teknolojia?
 
Back
Top Bottom