Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,884
- 12,134
Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha ufadhili kwa wanafunzi wanaohitimu Kidato cha Sita wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN) waliopata udahili katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba kwenye vyuo vya Elimu ya Juu nchini.
Ufadhili huu unajulikana kwa jina la SAMIA SCHOLARSHIP. Lengo la ufadhili huu ni kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili hatimaye taifa lipate rasilimali watu ya kutosha kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya nchi na watu wake.
Akizungumzia hilo Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Adolf Mkenda, leo, Julai 27, 2023 amesema wakati huu ambapo wahitimu wa kidato cha sita wakiwa wanajiandaa kwenda katika masomo ya juu kuna fursa hiyo ya kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili huo kwa asilimia 100 (100%).
Profesa Adolf Mkenda
Amesema Serikali ilitenga Tsh. Bilioni 3 kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 na jumla ya Wanafunzi 636 walinufaika na ufadhili huo, Wanawake wakiwa ni 231 (41%) na Wavulana 375 (59%), pia kulikuwa na Wanafunzi 12 wenye mahitaji maalum walifanyiwa tathimini peke yao nao walinufaika.
Ameeleza kuwa katika mwaka huo uliopita walisajiliwa na kudahiliwa katika Vyuo 18 Nchini ikiwepo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Akizungumzia mchakato mpya katika Mwaka wa 2023/2024, Serikali inatarajiwa kutoa ufadhili kwa wahitimu wa kidato cha sita takribani 640, jumla ya Tsh. Bilioni 6.7 zimetengwa kuwagharamia wanufaika wanaoanza na wanaoendelea na hivyo kufanya jumla ya wanufaika ambao watakuwa vyuoni kuwa 1,276.
Amesema "Ufadhili huu ni kwa masomo ya Shahada ya Kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika Mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2023 inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika tahasusi za Sayansi kama zilivyoainishwa hapo juu.
"SAMIA SCHOLARSHIP inagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Chuo Kikuu kwa Wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.
“Masharti ya ufadhili kwa wanaoendelea kusoma chini ya Ufadhili wa Samia, wanatakiwa wasishuke ufaulu wa GPA 3.8, watakaoshuka hapo wataondolewa kwenye ufadhili na kuingizwa kwenye mikopo ili waendelee kusoma.
“Tunahimiza wanaopata ufadhili waendelee kuonesha ufaulu wao wa kidato cha sita ulikuwa wa haki.”
Ameongeza kuwa majina ya watakaoteuliwa yatakuwa wazi, ufaulu wao utakuwa wazi pia, vigezo vipo wazi na majina yao yatawekwa kwenye tovuti ya Wizara.
Katika Wanafunzi 640 wapo ambao hawatataka kufanya masomo ya Sayansi watalazimika kuomba mkopo wa kawaida, watakaoenda nje ya nchi kwa sasa ufadhili huo haufiki huko, hivyo kukitokea nafasi watachukuliwa waliochini ya wale walioteuliwa awali.
Katibu aelezea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Prof. Carolyne Ignatius Nombo amesema vyuo vilivyonufaika kwa kuwa na Wanafunzi hao ni Vyuo Vikuu vya Serikali ni 13 wakati Vyuo Vikuu visivyo vya Serikali ni vitano.
Vyuo vilivyokuwa na idadi kubwa ya wanufaika ni MUHAS walikuwa na Wanafunzi 233 ambayo ni 36% huku UDSM wanufaika wakiwa ni 311 (48%).
Amesema “Ufadhili huo unazingatia Ada ya Mafunzo, Posho ya chakula na malazi, Posho ya Vitabu na Viandikwa, Mahitaji Maalum ya Vitivo, Mafunzo kwa Vitendo, Utafiti, Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na Bima ya Afya."
Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kuanzia Jumatatu, Septemba 25, 2023. Hii inatokana na ukweli kwamba katika kipindi hicho kila mwanafunzi atakuwa amepata udahili katika chuo cha Elimu ya Juu nchini.
"Wizara inahamasisha Wanafunzi wote nchini kuendelea kupenda na kujiimarisha katika masomo ya Sayansi na hatimae kujiunga na Elimu ya Juu katika programu za Sayansi, Teknolojia Uhandisi na Hisabati (STEM) ambapo watanufaika na mpango huu mahsusi," amesema.