Muda gani ni sahihi wa kushiriki tendo la ndoa baada ya kujifungua kwa upasuaji?

chaz beezz

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
217
843
Je, ni muda gani sahihi kwa mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji anatakiwa kushiriki tendo la ndoa?

Ni miezi mitano sasa imepita tangu mke wangu ajifungue mtoto kwa njia ya upasuaji, hivyo katika kipindi chote hicho nimekua mvumilivu sana katika kumsuburi aweze kuwa sawa na kupona kabisa ili niweze kushiriki naye tendo (minyaduano).

Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda hisia kali zinanizidi, hamu ya kushiriki tendo inaniijia kila mara ukiangalia siwezi kumsaliti mke wangu, nampenda sana mama watoto.

Tatizo yeye nikimuuliza kuhusu anavyojisikia hali yake kama yuko tayari sasa ili tushiriki tendo anadai bado hayuko tayari kufanya mapenzi.

Hivyo nauliza wakuu ambao mshapitia kipindi kama hiki mlifanyaje au kwa wataalam, je, kiafya ni muda gani sahihi wa kufanya mapenzi kwa mwanamke ambae kajifungua kwa upasuaji?
 
Pole kaka yangu mm nilikaa siku 40 tuh mme wangu akawa anajilia haki yake.
Ila huyo Bishosti ana matatizo yake mapenz yote kahamishia kwa mtoto wakat wewe ndio unaye muhudumia
 
Nenda nae taratibu, kwa wengine ni kweli hizo hisia hua zinakata kabisa.Wana sayansi watusaidie hapa kwanini mtu akitoka kijifungua hisia hukata. Msaidie pia majukumu ya mtoto ujue ukiwa na mtoto mchanga alafu kilizi ni mtihani. Usiku kucha unakuta mama ndo anahangaika kukabembeleza hawezi kuwazia sex hata kidogo.
 
Ni swala la kujadiliana na mwenzi wako maana uzazi sio jambo rahisi na inatakiwa kuwa karibu naye bila kusahau zawadi za mara kwa mara ili kurudisha hisia zake.
 
Back
Top Bottom