NADHARIA Mtu akikung'ata ukapaka mavi ya kuku meno yake yanaoza

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu,

Kipindi tulipokuwa watoto nilikuwa nasikia hii sana kwamba uking'atwa na mtu ukienda kupaka kinyesi cha kuku basi yule aliyekung'ata meno yake yanaoza yote!

kuku.jpg

Ni kweli hii au ilikuwa njia ya kufanya watoto wasiwe wachokozi kwa wengine?
 
Tunachokijua
Kuku (Gallus gallus domesticus) ni ndege anayefugwa na binadamu nyumbani tangu miaka 8,000 hivi. Kwa sababu hiyo ni miongoni mwa ndege wa kitoeo waliosambaa zaidi duniani na ndio ndege walio wengi zaidi duniani ambao Watu hutumia nyama yake na mayai kama chakula.

Meno ni viungo vya mwili vilivyopo kinywani vyenye kazi ya kutafuna yaani kumega chakula. Kazi kubwa ya meno kwa binadamu ni katika umeng'enyaji wa chakula anachokula na mara chache katika kusaidia kukata vitu mbalimbali, kung'ata vitu kwa lengo la kumega nk.

Mavi ya kuku ni kinyesi anachokitoa kuku kama taka mwili.

Je, Ni kweli mtu akikung'ata ukapaka mavi ya kuku meno yake yanaoza?

Jamiicheck, imetafuta machapisho ya watafiti au historia ya ushahidi wa aliyewahi kuoza meno kwa kumng'ata mtu kisha aliyeng'atwa akapaka mavi ya kuku ili kubaini kama ni kweli kama isemavyo nadharia hii.

Tumebaini kuwa hii ni nadharia ambayo haina ushahidi wa mtu yeyote aliyewahi kuoza meno kwa kupakiwa mavi ya kuku wala uwepo wa ushahidi wa tafiti yoyote ya kisayansi au kihistoria, hata hivyo hakuna mahusiano yoyote ya sehemu aliyong'atwa mtu na meno ya aliyemng'ata. Hii ni nadharia tu iliyotumiwa na watu tangu zamani kuwajengea hofu watoto ili wajiepushe na tabia ya kung'ata wenzao ili wasijeruhiane.


images

Jamiicheck imekosa machapisho ya watafiti wala ushahidi wowote wa mtu aliyewahi kung'ata na baadaye meno yake kuoza kisa aliyeng'atwa alipaka mavi ya kuku hivyo hii inabaki kuwa nadharia.
Jambo lolote linalo include mambo ya imani lazima liwe na mkanganyiko.

Lakini kwa hili ulilolileta hapa haina haja ya jamii check kushughulika nalo kwa sababu directly jibu ni HAPANA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom