Je, ni kweli kuwa watu wenye stress hula sana na matokeo yake huwasababishia uzito kupita kiasi?
- Tunachokijua
- Msongo wa mawazo ni hali ya mtu kuzongwa na mawazo hasi ambayo mara nyingi hupelekea matokeo mabaya Kwa muhusika hasa pale asiposaidiwa au asipojisaidia kutoka kwenye changamoto hiyo.
Kula sana ni kitendo cha kula chakula kupita kiasi cha kawaida ambacho mwili wako unahitaji kiasi cha kukufanya ujisikie vibaya.
Kumekuwa na madai kwamba mtu anapokuwa katika msongo wa mawazo huweza kuchochea kuzalisha tabia ya kula sana isivyo na kuweza kupelekea kuongezeka uzito.
Upi ukweli kuhusu madai haya?
JamiiCheck imepita vyanzo mbalimbali ili kubaini ukweli wa madai haya. Chuo cha Afya cha Havard na Tovuti ya Medical news Today wanakubaliana na madai haya kwa kufafanua namna namna ambavyo Msongo wa mawazo huweza kuchochea kuzalisha tabia ya Kula sana na hatimaye kupelekea kuongezeka kwa uzito.
Kwa upande wao Chuo cha Afya cha Havard wanaelezea homoni ambayo huzaliwa mtu anapokuwa katika Msongo wa mawazo na kusababisha kuzaliwa kwa tabia ya kula isivyo kawaida. Wakifafanua jambo hilo katika makala yao wanasema:
Mtu anapokuwa na msongo wa mawazo, tezi za adrenalini huzalisha homoni iitwayo cortisol ambayo kazi yake kubwa ni kuuchochea mwili kufanya mambo mbalimbali. Miongoni mwa vichocheo vinavyoweza kuibuka wakati huu ni pamoja na kichocheo cha hamu ya Kula sana. Aidha, kuhusu kuongezeka uzito Chuo cha Afya cha Havard wanaeleza kuwa Watafiti wamehusisha msongo wa mawazo na ongezeko la uzito. Utafiti wa Chama cha Kisaikolojia cha Marekani uibaini kuwa kati ya watu 10 wenye msongo wa mawazo watu 8 waliongezeka uzito.Kwa upande wao Medical news Today wanafafanua kuwa kula kwa msongo wa mawazo ni kitendo cha mtu kula sana chakula kama njia moja wapo ya kuondokana hali aliyonayo. Wanasema:
Watu wengi hukumbana na kula kihisia kwa namna moja au nyingine. Tabia hii huweza kuonekana pale mtu anapochoka au anapofanya kazi ngumu na kuamua kujinunulia au kula chakula kizuri kwa lengo la kujipoza au kuwa sawa.Hata hivyo, hali hii ikitokea mara kwa mara huweza kuathiri afya ya muhusika hata kupelekea mtu kupata uzito uliopitiliza.Zaidi ya hayo, JamiiCheck imewasiliana na George B Chacha - Mwanasaikolojia wa Afya na Jamii ambaye naye amekubaliana na madai ya kwamba msongo wa mawazo huweza kupelekea kuzaliwa kwa tabia ya mtu Kula sana na hatimaye kuonezeka mwili na uzito. Akifafanua zaidi jambo hili Mwanasaikolojia Chacha
Suala hilo ni la kweli japokuwa inategemea na changamoto husika ya msongo wa Mawazo, jambo hilo lina uhusiano mkubwa na changamoto ya Afya ya Akili na Afya ya Mwili, ni vitu tofauti japokuwa vinaendana.kuhusu Msongo wa Mawazo kusababisha mtu kula sana, ipi hivi kuna Homoni inayotengeneza njaa inaitwa Ghrelin Hormone au Hunger hormone, hii ndio inadhibiti kiwango cha ulaji, hivyo Homoni hiyo ikizidiwa inakuwa si rahisi kwa mhusika kuweza kudhibiti chakula anachotakiwa kula kwa kuwa Homoni inakuwa imeshavurugika na inaweza kumfanya mhusika kuwa na tabia ya kulakula.Pia Msongo wa Mawazo unaweza kumfanya mtu awe anakula mara kwa mara sio kwa sababu anataka kuridhisha mahitaji ya tumbo, bali anaweza kufanya hivyo kama sehemu ya kujifariji, hiyo inaitwa Stress Eating.Stress Eating inamfanya mtu anakula zaidi kwa hisia na sio kwa ajili ya kushiba bali ili tu awe bize, mara nyingi inawatokea wanaokuwa wapweke, wakiwa na hasira au ambao hawana cha kufanya.
Hivyo ni kweli kuwa Stress Eating inaweza kumfanya mtu akanenepa zaidi kwa kuwa anakula chakula kingi kuliko uhalisia, pia inaweza kumfanya mtu akonde kwa kuwa atakula chakula kingi ambacho si sahihi, sio muda sahihi na pi sio katika muda sahihi matokeo yake afya yake haitakuwa sawa na kumfanya akonde.Hivyo, kutokana na ufafanuzi kutoka kwenye vyanzo hivyo hapo juu, JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa Msongo wa Mawazo hupelekea kuongezeka kwa hamu ya kula na hatimaye kuongezeka uzito ni ya kweli