Mshike sana huyo mke uliyenaye usirogwe ukamuacha

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,588
22,149
Ulikuwa na orodha ndefu ya wanawake wa kuoa, Ila uliwatupilia mbali wengine wote na ukamchagua hiyo uliyenaye leo. Ni hakika ulichagua saizi yako, ulichagua binti ambaye alikamilisha utu wako, ulichagua binti anayelingana na mambo yanayokuvutia.

Ulipokutana naye kwa mara ya kwanza, ulivutiwa na uzuri wake, tabia na ndoto zake. Nini kimekupata muda mfupi tu baada ya kuoa hadi ulalamike kuhusu chaguo lako mwenyewe?
Biblia inasema.... "Mfurahie mke wa ujana wako". - Mithali 5 :18.

Kutofautiana kila na mkeo kunaweza kuzuia maombi yako yasifike kwa Mungu (1 Pet 3:7).

Unapiga kelele "kwanini Mungu hajibu maombi yangu"? Mungu anajibu "Kwa sababu umekosa uaminifu kwa mke wako. Amekuwa mwaminifu kwako. Uwe mwaminifu kwake, maana nachukia talaka." Malaki 2:14 - 16.

Mke mwenye furaha, maisha ya furaha. Furaha ya pamoja kwenu nyote ni furaha maradufu;huzuni ya pamoja ni nusu ya huzuni.

Usitafute mwanamke sahihi, bali kuwa mwanaume sahihi. Unaye mwanamke sahihi kwa sasa. Perfect women don't exist this side of heaven.

Mshike sana huyo uliyenaye.

Ubarikiwe.
 
Shida huwa inakuwa kuhesabiana mabaya ndio kunafanya hata umuone mwenzio hafai, uone amepungua kitu, kusikiliza maneno ya wengine juu ya ndoa yako, kulinganisha ndoa yako na ndoa ya wengine hayo ndio yanaharibu kila kitu
 
Eti wanashauri wanandoa wawe wanashirikishana mambo yote, ikiwemo mali/fedha. Nasema hiviiiii si kwa huyu mwanamke niliyenaye!

Ana akili za ki-Delilah Delilah, mimi siyo Samson wa enzi zile. Mwanamke kichwa box kama huyu siwezi kudumu naye.

Walikuchagulia au lilikuwa chaguo lako
 
changamoto hazai sasa 🐒
 
Eti wanashauri wanandoa wawe wanashirikishana mambo yote, ikiwemo mali/fedha. Nasema hiviiiii si kwa huyu mwanamke niliyenaye!

Ana akili za ki-Delilah Delilah, mimi siyo Samson wa enzi zile. Mwanamke kichwa box kama huyu siwezi kudumu naye.
Shida itakuwa kwako jiulize ulipomchagua hukuona hizo akili za kidelila Delilah?

Komaa naye huyo ni wako.
 
Shida huwa inakuwa kuhesabiana mabaya ndio kunafanya hata umuone mwenzio hafai, uone amepungua kitu, kusikiliza maneno ya wengine juu ya ndoa yako, kulinganisha ndoa yako na ndoa ya wengine hayo ndio yanaharibu kila kitu
Kuna wanaume hawanaga misimamo kwenye machaguo yao hivyo hujikuta wanapata shida changamoto zikianza wanatafuta ushauri kwa wanaume wenzao walioshindwa
 
Back
Top Bottom