msaada jinsi ya kusajili biashara ,leseni pamoja na gharama zake

southernboy

JF-Expert Member
Sep 27, 2015
826
1,018
habari waku,nina mpango wa kuanzisha biashara ya kuuza mazao ya chakula kama mahindi,maharage na mengine .kwasasa nimeshafanya michakato ya kupata fremu ya kuuzia ila sijajua naanzia wapi kufanya usajili ,leseni yake pamoja na gharama zake. mwenye kujua anisaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari.
ENDAPO UTAANZA KAMA MTU BINAFSI.
Utatakiwa kuwa na TIN ya biashara na endapo una TIN ambayo haikua ya biashara badi utatakiwa kwenda TRA kuibadili iwe ya biashara.
Endapo TIN yako uliichukulia wilaya X na sasa unataka kufanya biashara katika wilaya Y basi utapaswa kuihamisha TIN hiyo ije katika wilaya Y.
Baada ya hapo utapata frame ya kufanyia biashara yako na utatakiwa kuwa na mkataba wa pango wa hiyo frame ambao utaupeleka TRA kwa ajili ya kulipa kodi ya zuio(ambayo huwa ni 10% ya thamani ya mkataba) pia kulipia ushuru wa stempu (huwa ni 1% ya thamani ya mkataba wa pango kwa mwaka).
Baada ya hapo utafanyiwa usaili na afisa wa TRA ili uweze kujadiriwa kodi utakayolipa kwa mwaka husika wa kodi na kodi hii hulipwa kwa kuvawanya kwa robo nne za mwaka kwa maana ya Machi, Juni, Agosti na desemba. Baada ya kulipa hayo yote hapo juu utapewa Tax Clearance tayari kwa kuchukua leseni ya biashara.
Baada ya hapo utajisajili katika mtandao wa TAUSI PORTAL na utaomba leseni ambako utatakiwa kuwasilisha mkataba wa pango, nk na hapa bei ya leseni ya biashara husika inategemea na Halmashauri uliyopo.
Ukilipia leseni usisahau kulipia na service levy na sasa unaweza kufanya biashara yako kwa amani pasipo usumbufu.

Kila la kheri
 
Kwa upande wa kuomba leseni ya biashara ninafanya, kwahiyo tunaweza wasiliana kukusaidia kupata leseni yako.

Kama utahitaji masuala ya kusajili majina ya biashara BRELA pia nafanya.

Karibu WhatsApp 0752026992
Tausi leseni za biashara mtandaoni kupitia mfumo.jpg
 
Back
Top Bottom