Ijue biashara ya nywele bandia faida na changamoto zake

nyaggad

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,160
692
Habari wadau!

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza,ijue biashara ya nywele faida na changamoto zake,kwanza kabisa naweza kusema biashara ya kuuza nywele za bandia ni kama biashara zingine,inakuhitaji ufanye tafiti kabla ya kuingia kwenye biashara hiyo ili uweze kujifunza namna ya kuifanya kwa faida na kukwepa hasara zisizo za lazima,sasa za basi nywele za bandia zipo katika makundi matatu maarufu (weavings,crochet na rasta),aina zote za makundi hayo ya nywele hizo zinalipa ila mpaka ujue mbinu bora ya kuzinunua na kuziuza kwa faida,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kufanya biashara ya kuuza nywele.

(1) Sehemu ya kufanyia biashara:awali ya yote kama unatafuta fremu ni vyema kuzingatia sehemu yenye mzunguko mkubwa wa watu hasa wanawake,maeneo kama masokoni,uswahilini ,karibu na vyuo ni bora zaidi kwa biashara hii lakini pia hata maeneo mengine inafaa itategemeana na eneo husika na aina ya watu waliopo.

(2) Aina za nywele zinazoweza kuuzika kwa maeneo uliopo:kama nilivyo sema awali aina za nywele zipo aina tatu maarufu (weaving,crochet na rasta)hivyo basi ni muhimu kuzingatia wateja ulionao ni wa aina gani na wapo katika hali ipi ya uchumi,kwa mfano uswahilini wanapendelea kusuka rasta za kawaida kwa sababu ni bei nafuu huwezi kulinganisha na crochet.

(3) Washindani wako: mahali unapotaka kufanya biashara ni vyema kuwatambua washindani wako wapo wangapi,wanauza nywele zipi na kwa Tsh ngapi?,hii itakupa picha kamili namna ya kujipanga kushindana nao,hili la kutambua wanauza nywele zipi ni muhimu sana kwa sababu nywele bandia zipo katika makundi matatu(weaving,crochet na rasta)lakini ndani ya hayo makundi zipo za mitindo aina nyingi kutegemeana na wakati huo.

(4) Bei za nywele: hutegemeana na mambo matatu (aina ya kampuni,Idadi ya nywele anazochukua,majira ya wakati na aina ya mteja),kila kampuni ina bei yake ya nywele zake,kila kampuni imeweka kiwango cha bei kulingana na ukubwa wa mzigo anao hitaji mteja,bei za nywele hubadilika kutegemeana na majira ya wakati flani,kwa mfano inapofika wakati wa sikuu nywele hupanda bei,wakati mwingine bei ya nywele hutegemeana na mahusiano ya mteja na kampuni husika pengine ni mteja wa mda mrefu na muaminifu(loyalty customer),kwa mfano kuna baadhi ya wateja hupelekewa mzigo wa 10M hadi 20M kwa mali kauli na kulipa kidogokidogo pale wanapofanya mauzo,hapa Tanzania tuna viwanda zaidi ya vitano vya nywele sababu hiyo basi ili ufanikiwe kwenye biashara hii,unahitaji mtandao wa watu sahihi na uaminifu wa hali ya juu,unaweza ukaanza na mtaji wa 2M ukiwa na nidhamu ya biashara baada ya mda mfupi unaweza ukajikuta unamtaji wa 10M na zaidi.

(5) Changamoto ya biashara ya nywele:watu wengi huingia kwenye biashara hii kwa kuona wengine wakifanya biashara hii na kwa utafiti wa hisia pasina uhalisia,kwa mfano mtu ana 5M anaamua kwenda kununua nywele bila kujua soko la nywele na kwa bahati mbaya wauzaji wa nywele viwandani na kwa jumla hawawezi kukwambia ukweli kuwa nywele hiyo unayonunua hai uziki sokoni sana,wao wanachotaka wauze na stock yao ipungue,ukiwauliza nywele ipi nzuri?watakuambia zote tu,kasheshe linapoanza pale unapoziweka dukani kwako unashangaa miezi 6 inaisha mzigo hau jaisha na kodi unadaiwa,na unashangaa wenzio biashara zao zinaenda vizuri,ili kuepuka hasara kabla hujanunua nywele unahitaji kujua nywele zinazo uzika sokoni ni zipi kwenye kila kampuni?,na wakati mwingine nywele inaweza kufanya vizuri sokoni Mwanza na isifanye vizuri sana Daressalaam,anyway kuna vitu vingi vya kujifunza kama unahitaji ushauri zaidi wa kufanya biashara hii au kununua nywele tuwasiliane +255654983243.

image (33).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom