Msaada: Friji linajizima na kujiwasha, tatizo nini?

Wakuu nina friji langu aina ya HAIER nimelinunua miez 6 iliyopita nilikua nalitumia vizuri tu bila tatizo ila mgao wa UMEME ulipoanza basi umeme ukirudi linakua linachelewa kuwaka

Linakua linawajiwasha na kujizima hivyo hivyo hadi baadae sana umeme ukishatengamaa ndo linajiwasha moja kwa moja

Sasa shida imekuja juz umeme ulikatika ukaja kurudi likachelewa kujiwasha sana hadi jana asbuhi ila saa jana 5 umeme ukakatika tena na kuja kurudi hadi leo tokea hyo jana friji linajiwasha na kujizima tu kwa sekunde kadhaa

Hadi muda huu halijawaka zaidi ya kujiwasha tu na kujizima kwa sekunde mbili, nashindwa kuelewa changamoto ninini maana friji yenyewe ni ndogo ya mlango mmoja tu na huwa inatumia umeme kidogo sana unit moja unatumia siku 3 na hapo umeliwasha masaa 24

Tatzo litakua ninini?Ila huwa situmii friji guard wala stablaiza....
Eneo lako lina tatizo la umeme mdogo. Low voltage.
 
Juzi nilitaka kumwita fundi wa fridge acheki nilikuwa na shida kama yako kumbe baadae nikaja kugundua umeme ni mdogo hasa maeneo yetu ya chamazi kunasumbua umeme huwa unatulia kuanzia usiku SAA 6.
Jaribu kuwasha usiku Sana umeme umetulia pengine tatizo ni umeme mdogo pia kama inasumbua tafuta fundi tu
Cha kushangaza tokea juzi joto lilivyopungua na mvua kunyesha lilianza kugandisha vizuri tu kama kawaida linafanya kazi vizuri tu

Sasa nashindwa kuelewa kwanini lifanye kazi kipindi cha mvua tu au joto likiwa limepungua??
 
Weka stsbilizer mkuu

Mh inategemea,Mimi friji huwa inawaka na ikishapooza Sana inazima yenyewe,na baada ya muda hujiwasha sijawahi kuhisi ni tatizo.
Pia pump ya maji hufanya hivyo inawaka,maji yakijaaa kwenye tank, automatic pump itazima,yakipungua itawaka
Sasa kwangu linajiwasha kwa sekunde moja na kujizima linafanya hivyo tu hata wiki bila kugandisha wala kupooza
 
Cha kushangaza tokea juzi joto lilivyopungua na mvua kunyesha lilianza kugandisha vizuri tu kama kawaida linafanya kazi vizuri tu

Sasa nashindwa kuelewa kwanini lifanye kazi kipindi cha mvua tu au joto likiwa limepungua??
Joto lilikuwa Kali kama jehanamu ndiyo maana watu wengi walikuwa wanalalamika kuhusu mafriji yao
 
Mrejesho:Mlinishauri wengi humu ninunuwe stablizer hatimaye Nimenunua stablizer matatizo yote kwishaa sina la kusema kwa jinsi nilivyofurahi hapa,maana hadi juisi za mtoto na maziwa mansap alikua anaweka humo, tumepata adha sana maana ilikua inatugharimu mimi na mama mtoto wangu.... Nawashukuru sana wanabodi sijui kusingekua na JF maisha yangekuaje?Mungu awabariki sana
 
Back
Top Bottom