yash_ed
Senior Member
- Jan 9, 2020
- 146
- 391
INASIKITISHA SANA TENA SANA ðŸ˜
WALIOOKOLEWA WAKANA KUSAIDIWA NA MAJALIWA, WADAI WALITUMIA JUHUDI ZAO KUJIOKOA.
Furaha ya Majaliwa Shujaa aliyeokoa watu kwe ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba mkoani Kagera huenda ikageuka huzuni baada ya abiria waliookolewa kwenye ajali hiyo kudai walitumia juhudi zao wenyewe kufungua mlango na kisha kutoka.
Akizungumza mmoja wa abiria hao amesema yeye ndiye angeweza kuwa kinara wa tukio hilo kwani baada ya ndege kutua kwenye maji, yeye na muhudumu mmoja wa ndege hiyo waling'ang'ana kufanya jitihada za kufungua mlango wakati huo mitambo ya umeme ilikuwa imezima na mlango ulikuwa umejilock.
"Baada ya ndege kutua kwenye maji nilianza kutapatapa kutafuta mlango wa kutokea, haikuwa rahisi lakini kwakuwa mimi nilikuwa viti vya nyuma nilijitahidi kutafuta namna ya kutokea, tulikuwa tunaenda kufa, nikawambia wenzangu "kwahiyo tunakufa huku tunajiona" hapo maji yalikuwa yamejaa, lakini baadae niliona mlango unajifungua kidogo baada ya muhudumu wa ndege kuuchokonoa kwa chini ndipo nilipotumia upenyo ule kuusukuma mlango nikatoka nje"
Abiria huyo ameongeza kwa kusema "baada ya mimi kutoka nilianza kuwaokoa wenzangu, na kila aliyekuwa anatoka alikuwa anakaa juu ya ndege maana maboti ya wavuvi yalikuwa bado kufika, nilijawa na ujasiri mkubwa ingawa hali yangu ilikuwa mbaya, nikawa nawavuta watu kuwatoa nje akiwemo mama mmoja na mwanae ambao pia niliwaokoa mimi nikisaidiana na mchina, baadae watu waliisha kwenye ndege nikajua wote wametoka ndipo wavuvi walipoanza kuja kutuchukua kutupeleka hospitali";- ameeleza mmoja wa waliookolewa.