Mradi Kabambe wa Ujenzi wa Maabara Kwenye Sekondari za Kata za Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,038
974

MRADI KABAMBE WA UJENZI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI ZA KATA ZA MUSOMA VIJIJINI

Jimbo la Musoma Vijijini limeamua kutatua tatizo sugu la ukosefu wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zake za kata.

Lengo kuu:
Kila Sekondari ya Kata ipate maabara nzuri na za kisasa za masomo matatu ya sayansi - physics, chemistry & biology labs.

Wachangiaji wakuu wa mradi huu ni:
1. Wanavijiji
2. Serikali Kuu
3. Mbunge wa Jimbo
4. Mfuko wa Jimbo
5. Baadhi ya wazaliwa wa Musoma Vijijini

Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushauriwa nayo ianze kuchangia mradi huu kwa kutumia mapato yake ya ndani!

Takwimu za maabara tulizonazo:

(A) Sekondari zenye maabara tatu (3):
1. Bugwema 2. Kiriba
3. Ifulifu 4. Mugango
5. Bwai (zinakamilishwa Jan 2024)

(B) Sekondari zenye maabara mbili (2):
6. Bulinga 7. Kigera
8. Nyakatende 9. Makojo
10. Nyambono 11. Nyegina
11. Rusoli 13. Suguti

(C) Sekondari zenye maabara moja (1):
14. Bukima 15. Dan Mapigano (Bugoji)
16. Etaro 17. Kasoma
18. Mabuimerafuru

(D) Sekondari zizokuwa na maabara hata moja
19. Nyegina 20. Busambara
21. Mtiro 22. Murangi
23. Nyanja 24. Seka
25. Tegeruka

Sekondari za binafsi zimejenga maabara zake
26. Bwasi (Kanisa la Wasabato/SDA)
27. Nyegina (Kanisa Katoliki/RC)

Karibuni tuendelee kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zetu za kata za Musoma Vijijini

Tafadhali sana usisahau Harambee ya ujenzi wa maabara za Etaro Sekondari utakaofanyika Ijumaa, 15.12.2023 (tangazo la Harambee linatolewa leo)

Sayansi ni kila kitu
&
Kila kitu ni Sayansi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 13.12.2023
 
Back
Top Bottom