Moja ya mambo yanayochangia migogoro kwenye ndoa nyingi ni wanaume kuingia kwenye ndoa wakitarajia wake zao kuwasaidia majukumu yao

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,089
1,276
Naamini kuna mambo mengi yanayochangia migogogoro na kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa wakati huu

Ila Naomba nielezee hii sababu majawapo ambayo ni
Wanaume wengi au vijana pengine niwaite wavulana kuingia kwenye ndoa wakidhani wanawake wao watawasaidia baadhi ya majukumu na wengine wajinga wakitamani wasaidie hata majukumu yote

Kigezo kikubwa kwa mwanaume na jukumu la kwanza ni kuoa mwanamke anayempenda na kumvutia kwa asilimia kubwa tabia sura na hata maumbile
Na hapa tunatofautiana Kila mtu ana tabia sura na maumbile yanayomvutia

Ukifanikiwa kwenye kigezo na jukumu la kwanza hayo mengine yote ni rahisi

Jukumu la pili na muhimu ambalo wanaume wengi haswa wa wakati wanalikimbia wakidhani watabaki salama ni
Kumuhudumia mke wako kwa Kila kitu kuanzia Nguo yake ya NDANI mavazi ya nje mahitaji yote muhimu kwa mwanamke ni jukumu la mwanaume kumuhudumia

Tatu mahitaji yote ya familia ni jukumu la mwanaume kuhudumia hata Kama mwanamke ana mshahara ana hiari ya kuchangia mahitaji ya familia au la

Hata akichangia weka akilini mwako kwamba anakusaidia majukumu yako usibweteke,
Siku akijisikia kutochangia Basi ukubaliane na hali na umshukuru walau kwa kile alichochangia

Kwenye maandiko jukumu la mwanamke kubwa ni uzazi na kumtii mume wake


Ukiona mwanaume ambae kigezo chake kikubwa anataka mwanamke mwenye kazi au mshahara au mpambanaji hiyo ni dalili ya hao wanaume

Nashauri hakikisha unakuwa na msingi mzuri wa kipato kabla ya kuoa Bora uchelewe kuoa ili
Uoe mwanamke unayempenda na mwenye uwezo wa kumuhudumia
Kwa asili
Wanawake hawaji kuongeza kipato Ila kutumia kile kipato chako

Uanaume ni kazi Sana na uwajibikaji wake ni mkubwa
Sio rahisi kuwa mwanaume na Wakati mwingine kuwa baba wa familia
 
1693938683241.jpg
 
Hilo suala la kutoa kanisani hela yote Sina uhakika nalo maana sadaka mara nyingi huwa na Siri
Na pia kimaandiko hakunaga utaratibu wa kutoa mshahara wote kanisani labda uwe malimbuko mshahara wa kwanza au MTU aamue mwenyewe

Pili naendelea kisisitiza huyo mwanaume Hana sababu yoyote ya kuumia maana hayo majukumu yote aliyoyataja ni ya kwake kama mwanaume ,
Ilipaswa ajipange kabla ya kuoa aone anaweza au la
Sio Kuja kumtegea mke wake majukumu yanayomuhusu
Matokeo yake ndo hayo Sasa unalia Lia
Na kwa taarifa hizo mali lazima wagawane na mke wake
Mke ana hiari ya kuchangia au kutokuchangia majukumu ya mwanaume
 
Tatu mahitaji yote ya familia ni jukumu la mwanaume kuhudumia hata Kama mwanamke ana mshahara ana hiari ya kuchangia mahitaji ya familia au la
Sasa yafaa nini wewe kwenda kazini ikiwa kipato chako akijumuishwi kwenye ustawi wa familia?
Ni suala la kukubaliana hapa kama tumeamua uwe mama wa nyumbani ni jukumu langu kubeba wajimu mzima wa ustawi wa kiuchumi kwenye familia kama tumekubaliana nawe unaenda kutafuta basi ni sharti ulete kitu mezani pia.
 
Bibi na mama zetu walikuwa wakilima kwa jembe la mkono shambani kuzalisha chakula cha familia na mazao ya kuuza kupata kipato cha familia yote. Hili la MWANAMKE KUHUDUMIWA KILA KITU NA MUME LIMETOKEA WAPIIIII!!!!??? Ni wazi ni falsafa ya kikahaba(prostitute) kuwa mwanaume ni wa kumlipa mwanamke. Wanawake wa nchi za Kiislam ambao hawaruhisiwi kuajiriwa, kufanya biashara wala kutoka nyumbani bila idhini ya wanaume ndiyo wana haki ya kudai kuhudumiwa na waume zao. Wanaume tusikubali kufanywa mabwege, kila binadamu afanye kazi, kama ngono ni biashara waombe leseni siyo kujifinya ktk kichaka cha kuhudumiwa ktk ndoa.
 
Sasa yafaa nini wewe kwenda kazini ikiwa kipato chako akijumuishwi kwenye ustawi wa familia?
Ni suala la kukubaliana hapa kama tumeamua uwe mama wa nyumbani ni jukumu langu kubeba wajimu mzima wa ustawi wa kiuchumi kwenye familia kama tumekubaliana nawe unaenda kutafuta basi ni sharti ulete kitu mezani pia.
Hapo kwenye kukubaliana mkuu ndo mahali mwanaume aliambiwa Aishi na mwanamke kwa akili

Hoja yangu tuondoe fikra za mwanamke kukusaidia majukumu yako
Kama mkikubaliana lazima ujue sapoti yake ni hiari sio lazima

Hii itakusaidia kuwa huru hata siku ambayo akiamua kujitoa kwenye makubaliano
Bado ndoa na familia itasimama
 
Yaani wewe unasubiri mwanaume aje akununulie chupi akili zipo timamu kweli wewe ?

Vitu vingine vya kipumbavu watu wanaandika humu, vinashangaza kweli juu ya utimamu wa akili zao.
Naona umeacha hoja ya msingi akafocus kwenye jambo ambalo una uwezo nalo
Rudia kusoma Tena
 
Back
Top Bottom